Wana Diaspora, naomba ushirikiano wenu; tukutane, tujadili Tanzania ikusaidieje ili uisaidie nchi yako?

Lazima kuwe na mkakati unaoleweka wa kupeleka vijana nje ya nchi kwa njia zinazokubalika kisheria.

Mfano India kuna collaboration kati ya Diaspora na walionyumbani kuwatoa nje ya India ikiwa ni kukabiliana na tatizo la ajira, Utaalamu na elimu. Hili hata wakenya, Waghana, Nigeria, Ivorians almost West Africa yote wana tabia hiyo. Je Diaspora wa Tanzania wanajisikia fahari kuunganisha nguvu kuwatoa vijana nje ya nchi? Hapa wahindi unawaona wengi wameletwa na wenzao .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAKUNA Cha diaspora hapo uhuni TU, yaan watu wapo nje wanabeba mabox hawana pa kulala hawana Cha kufanya wanakimbizana Na mamlaka za uhamiaji kule hawana vibali ndo wataleta mabadiriko yapi, tumien akili.
 
Sidhani hata kama ilihitajika tena hili kongamano lifanyike, yatakuwa ni yale yale, na binafsi sipendi kuona mambo yanayosemwa yakijirudia rudia, tunakuwa kama tuna matatizo akilini! Nasema hivi sababu Diaspora walishaomba na kushinikiza pointi zao muhimu.

Uraia pacha, mapendekezo mazuri jinsi ya kuitangaza TZ huko, kushirikishwa katika upigaji kura, kusaidia na kuiendeleza nchi yetu kwa kutumia ujuzi wa hawa Diaspora.

Yapo mengi mno ya kushirikiana kati yetu na hawa wenzetu walio ughaibuni, lakini imekuwa semina, warsha na mikutano isiyozalisha matunda ya aina yoyote yale!

Tutashukuru kama hili kongamano litakuwa tofauti na yale yote yaliyopita, ilikuwa kama tunajipotezea muda na kuwapotezea wao muda, hasa wao, maana wenzetu huko ni [HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG] sisi kupiga domo ndio kawaida yetu.
WHY DIASPORAS ARE IMPORTANT

Why Diasporas are Important

Africa's secret weapon: The diaspora @CNNI Africa's secret weapon: The diaspora - CNN

Why Would Countries Want to Befriend Their Diasporas Abroad? Why Would Countries Want to Befriend Their Diasporas Abroad? | Expatriatus

The Economist explains: What countries want from their diasporas What countries want from their diasporas via theeconomist
 
SOS, kama kuna mwana Diaspora yoyote yuko Dar saa hizi na sio muoga yuko bold enough kuzungumzia issues za diaspora naomba tuwasiliane urgently 0784 270403

Pascal
 
HAKUNA Cha diaspora hapo uhuni TU, yaan watu wapo nje wanabeba mabox hawana pa kulala hawana Cha kufanya wanakimbizana Na mamlaka za uhamiaji kule hawana vibali ndo wataleta mabadiriko yapi, tumien akili
Mtu ambae anakimbizana na mamlaka na hana pakulala anawezaje kuja Tz na kurudi Ulaya kila anapotaka kufanya hivo? Wacha upoyoyo kichwa debe tupu mxiisiu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Money Transfer inayoeleweka maana Diaspora wengi wanatuma hela vichochoroninkwa wasomali. Unakwenda kkoo pale unakutana na msomali anakupa fedha imetoka ughaibuni.
Tunahitaji waombe kodi iwe ndogo ili wafanye money transfer zilizo kubalika kisheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mayala waambia waruhusu uraia pacha na waache kuwaona diaspora ni wapinzani, na mara hii ni mara ya nne conference ya aina hiyo kufanyika lakini hakuna hata kitu kimoja cha maana kilichoamuliwa na serikali zote mbili,
Nchi zote zilizoendelea kupitia diaspora wake zimefanya maamuzi magumu sana lakin tz wanafkir kea kufanya makongamano ys aina hiyo ndio yataleta tija, acheni siasa zisizoivusha nchi kiuchumi ikasonga mbele leo mtz alioko ulaya anabeba box na kulipwa mshahara wake wa kumtosheleza aendelee kuishi na asave viposho vyake kwa ajili ya kujenga kaj[/URL]
Diaspora fanyeni mambo ya maana, hakuna nchi yoyote INAYOJIVUNIA RAIA WACHAMBAJI na WABEBA BOX.
- Mkiona nchi haiwataki mjue HAMNA FAIDA YA YOYOTE, Mngekuwa WATU wa FAIDA wala MSINGETUMIA Nguvu nyingi kushawishi mambo yenu. TATIZO LA DIASPORA wa Tanzania ni KUTAFUTA UPENDELEO na KUONEWA HURUMA
 
waste of time
waste of money
waste of intellect

Serikali ya Tanzania haioni umuhimu wa diaspora
sasa why leo maoni ya wana diaspora yanahitajika?

diaspora yoyote atakeywekda kwenye mikutano hii naye hana cha kufanya

solution iko kwenye katiba mpya ambamo ilitakiwa kuwepo hiki kipengele

sasa kama hakuna katiba mpya then forget about hizi PR STUNTS za serikali
 
Dual citizenship/urai pacha ndo msaada mkubwa kwa diaspora ambao nchi inaweza kuwafanyia wananchi wake waishio nje ya mipaka. Kwa kufanya hivyo diaspora watakua huru na motivated kuwekeza nyumbani.

Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea zinaruhusu uraia pacha isipokuwa TZ.
Ulichoongea ni ukweli, lakini wanasiasa wa hapo nyumbani hawana imani na Diaspora, kwa kuwa siku za karibuni wanadiaspora wameshambulia zaidi chama tawala na serikali yake badala ya kutoa ushauri nini kifanyike.
 
That would do.
Bufa imekuja muda sisi tulio nje lazima tukubali kuwa serikali zilizoko madarakani na chama chao imechaguliwa na watanzania, kwa hiyo tutumie uzoefu wetu kushauri nini kifanyike ili taifa lisonge mbele, lakini tunatumia sana mitandao kushambulia na kukosoa, hapa ndipo tunajifungia milango.
 


Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Diaspora Zanzibar. TV Program 1 ...
https://youtu.be/zNYS_0z9-G4
Press Conference ya Uzinduzi Wa Kongamano la Nne la Diaspora ...
View attachment 566354


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.
Wanabodi.

Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
DIASPORA: Home Page
or
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

Natanguliza Shukrani.

Pascal Mayalla
+255 784 270403
pascomayalla@gmail.com



Kaka Mayalla hiyo mikutano ya kufanyikia Zbar hatuipendi, tunatamani sana mikutano ifanyikie kwenye nchi ambazo tupo kama hapa USA, Uk na nyinginezo. Mabalozi wetu waandae makongamano kama wanavyofanya wakenya hapa USA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom