Wana CCM walio katika vyuo vya juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wana CCM walio katika vyuo vya juu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FortJeasus, Jan 19, 2012.

 1. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Yafahamika kuwa ni haki ya kisiasa kwa mwananchi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa nchini.Pamoja na ukweli huo,ni dhahiri kuwa nia, malengo na misukumo ya baadhi vijana kujiunga ama kushabikia chama cha CCM hayako sahihi,hata kama kwa kufanya hivyo hawavunji katiba ya chama chao na hata katiba ya nchi kwa ujumla wake.
  Wengi wao, katika mioyo yao, wanadhani kadi ya ccm ni hakikisho la kupata nafasi mbalimbali serikalini na katika chama siku za usoni. Yawezekana kusema kuwa hiki ni kielelezo cha kiwango cha juu cha ubinafsi miongoni mwa vijana hawa kwa kuzingatia kiwango chao cha kufikiri kinachotokana na ngazi yao ya elimu.
  Ingetazamiwa, basi, wenzetu hawa wasukumwe na malengo, imani na mwelekeo wa chama .Muhimu wafanye hivyo baada ya kuwa wamejiuliza iwapo bado chama hiki kama taasisi ya kisiasa ama mienendo ya viongozi wake yanalingana na malengo ya waasisi wake na iwapo maisha ya wananchi wenzao yameboreshwa vya kutosha au uwepo wa matumaini ya kuboreshwa huko mbeleni chini ya chama hiki.
  Kwa sasa nina mashaka na mitazamo,nia na malengo yao nyuma ushabiki kwa chama hiki.Nina mashaka makubwa dhidi yao.
   
 2. m

  mariantonia Senior Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 135
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiwa wewe bado ni mwana ccm ndani ya university itakuwa elimu haikukomboi bora uachane na masomo
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Bora msingesoma
   
 4. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Pengine wanaingia huko ili kukibadilisha chama kwa kuwa inasemekana si rahisi kukibadili chama ukiwa nje bali ukiwa ndani.
   
 5. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,915
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Hayo ni mawazo mgando, kila mtz ana haki ya kujiunga na chama chochote. Usijione wewe ni bora kwa vile upo CDM, unatakiwa utumie demokrasia ya kuingia unaporidhika na sera husika
   
 6. kombati

  kombati Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kingunge yupo, msekwa yupo, lusinde snr yupo, makinda yupo n.k hawataki kubadlika wanaojua asili ya chama kuwa sio hii wanayotumikia sembuse wasiojua na wanaosukumwa na utumwa wa fikra??:shock:
   
Loading...