wana-CCM, sasa hizi ndizo siasa gani??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wana-CCM, sasa hizi ndizo siasa gani???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, Apr 9, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mjadala Katiba hila zatawala
  Na Waandishi wetu  9th April 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni
  [​IMG] Watoto wajazwa ukumbini Dar
  [​IMG] Mmoja apigwa, angolewa meno  [​IMG]
  Baadhi ya vijana wakifuatilia mjadala wa wazi wa Katiba mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana.  Katika kile kinachoonekana kama njama za kuvuruga, vijana wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana ‘waliuteka’ mkutano wa kutoa maoni kuhusu muswada wa mapitio ya Katiba wa mwaka 2011, baada ya kumwagwa katika ukumbi wa mkutano kwa nia ya kuwazuia wafuasi wa Chadema kuingia katika ukumbi wa mkutano na kuwazomea wote waliojitokeza kuukosoa muswada huo.
  Vijana hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 12-25, wakiwamo wanaume na wanawake, wanadaiwa kukusanywa na baadhi ya viongozi wa CCM kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji.
  Walimwagwa eneo hilo na kujaa karibu ukumbi mzima wa mkutano, kuanzia saa 12 asubuhi jana na kusababisha watu wengi waliofika baadaye, kukosa nafasi ndani ya ukumbi huo. Mkutano huo ulianza rasmi saa 3:00 asubuhi jana.
  Hatua hiyo, inadaiwa kuchukuliwa na baadhi ya viongozi wa CCM kwa kile kinachodaiwa kuwa kuwapiku wafuasi wa Chadema, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, wanaodaiwa ‘kuuteka’ mkutano huo juzi.
  Baada ya kuuteka mkutano huo, wafuasi hao wa Chadema wanadaiwa kumzomea kila aliyeonekana kuunga mkono muswada huo.
  Miongoni mwa walioonja machungu ya kuzomewa na kusababisha mkutano huo kuvunjika juzi, ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Richard Hiza Tambwe.
  Mwingine aliyezomewa jana, ni aliyekuwa mgombea wa CUF Jimbo la Temeke mwaka jana, Lucas Limbu, ambaye mbali ya kuzomewa, pia alipokwa kipaza sauti na wafuasi wa CCM na kuzuka vurugu iliyotulizwa na askari polisi baada ya kuingilia kati.
  Mkutano huo ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, ulifanyika kwa siku mbili mfululizo, kuanzia juzi, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya vijana hao waliozungumza na waandishi wa habari, walithibitisha kupelekwa katika eneo hilo na baadhi ya viongozi wa CCM, ambao hata hivyo, walikataa kuwataja kwa majina.
  Hamisi Beimbaya, mkazi wa Buguruni Kwa Madenge, Wilaya ya Ilala, alisema juzi mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM aliwataka kufika katika mkutano huo kuanzia saa 11.00 alfajiri jana.

  Magreth Mwakasege (19), mkazi wa Mabibo, alitamka wazi kuwa walitakiwa na mwenyekiti wao wa chama kufika katika mkutano huo jana ili kulipiza kisasi dhidi ya kitendo alichodai kuwa cha wafuasi wa Chadema kutawala mkutano huo na kuwazomea viongozi wao wakuu wa chama.
  Kitendo cha vijana hao kutawala ukumbi huo wa mkutano, kilionekana kuwaudhi watu wengi, wakiwamo waliopata nafasi ya kuchangia maoni katika mkutano huo.
  Miongoni mwa watu hao, ni pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye alisema kuna watu waliokuwa wamepelekwa jana eneo hilo kwa lengo moja tu la kuvuruga shughuli ya kutoa maoni.
  “Wanavuruga, huku polisi wamejaa, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa. Kamati iliahidi kuwa atakayefanya fujo ataondolewa, lakini watu hao wanalindwa. Wote wanaozomea hakuna anayeinua mkono kutoa hoja,” alisema Lissu.
  Lissu, ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo, alikatiza na kususa kuendelea na mkutano huo kwa maelezo kwamba, haridhishwi na hali iliyokuwa ikiendelea, ambayo alisema imelenga kutaka kupitisha muswada huo kwa mtindo wa “Vodafasta”, kama ilivyowahi kufanyika katika kusaini Muungano na kupitisha Katiba ya sasa ya mwaka 1977.
  Kutokana na hali hiyo, Lissu alisema kwa vile imeshindikana katika mkutano huo, watahakikisha wanaupinga muswada huo mitaani.
  Mbali na vijana hao kufurika ukumbini hapo, pia watu wanaosadikiwa kuwa ‘mabaunsa’ wa CCM, walionekana wakivinjari katika viwanja vya Karimjee kwa nia ya kumshughulikia mtu yeyote aliyeonekana kuupinga muswada huo.
  Miongoni mwa walioshughulikiwa, ni pamoja na mhitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), jijini Dar es Salaam, Faki Mwakisu, mkazi wa Gerezani kota za reli, ambaye alishambuliwa kwa ngumi na mmoja wa mabaunsa wa CCM na kuvunjwa meno ya mbele.
  Mwakisu (28), alisema alishambuliwa na mtu huyo kwa madai ya kuchukizwa na kauli yake wakati akichangia maoni katika mkutano huo ya kumtaka Lissu, kuachana na shughuli ya kamati hiyo kwa vile imepoteza maana iliyotarajiwa.


  source: http://www.ippmedia.com/
   
 2. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ni upuuzi mkubwa katika ishu ya maana kwa Taifa hili kufanya vitu vya kijinga kiasi hicho,ni dalili tosha hawako tayari kuliendeleza Taifa hili kwa faida ya watanzania wote.,ndo maana hawakuandika kiswahili ili wachangiaje wawe wachache..

  Nawaonea huruma hao watoto laiti kama wangejua wanachokifanya ni kwa manufaa ya nani..?
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Dawa yao ni maandamano hapo ndio watatia akili.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanachojaribu kufanya ni kusimamisha mshale wa saa wakati mbio zinaendelea................watachelewa kushtuka.....
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,909
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Kweli sasa nimeamini you cant teach an old dog new tricks na hizi mbinu kama sikosei ni mawazo ya Makamba na Tambwe Hizza maana Hizza alisikika akisema na wao CCM watawahamasisha wanachama wao kujitokeza kwenye mjadala. Wanaiga kunya kwa Tembo, ni aibu kwa chama kikongwe kama CCM kufanya mambo kama haya kwenye masuala ya msingi.

  [​IMG]

  Baadhi ya vijana wakifuatilia mjadala wa wazi wa Katiba mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana.
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  yaani, vitoto vya watu vimechoooooka, hata kinachojadiliwa hapo hawakijui. vingine vimesinzia, sijui njaa? hivi vilipata hata posho ya nauli?

  ila watu wana dhambi sana, haya si mambo ya utumwa haya? na wazazi waliowatoa watoto wao wateseke hivi ili kufurahisha wanasiasa, wana akili kweli? wanwapenda kweli watoto wao?
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo amani na utulivu:tape:
   
 8. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  halafu watasema mijadala ilikuwa na mafanikio makubwa!
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni aibu kwa watu wazima kutumia kodi za wananchi bila aibu kwa jambo ambalo lengo lake ni kufaidisha kundi la wachache!
   
 10. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii inamaanisha wanachama wa CCM ni watoto ndo mana wameleta watoto wachangie
   
 11. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Uf3@xxxo*^sss


   
 12. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni aibu kubwa sana, watu tunaangalia maendeleo ya nchi itoke ilipo isonge mbele halafu wengine wanafanya mzaha, maana hii sasa sio siasa tena, ila ni upumbavu bora ingekuwa ujinga. Hili ni kosa kabisa kisheria,polisi inatakiwa iwahoji watoto hao ili ijue aliyewahonga watoto hao ili waende pale kutibua maslahi ya taifa ili hao watu waliopeleka watoto pale wafikishwe mahakamani.
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana mzaha wa aina hii katika jambo nyeti kama katiba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11

   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,591
  Trophy Points: 280
  Judy inasikitisha mno kuona kwamba mabilioni ya shilingi yatateketea katika mjadala huu ambao utatumika katika kutunga katiba ambayo Watanzania wengi kamwe hatutaikubali maana mjadala wenyewe umeshachakachuliwa na mafisadi.
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  mmh hiyo ndio CCM na Tambwe HIzza wao mzee wa propaganda hata UVCCM na UWT hawalitaki lichama lao wakaishia kubeba wa watoto siku zao zinahesabika
   
 16. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Heee, bado zinahesabika tu!
  "Fisi akaendelea kumfuatilia binadamu yule akidhani mkono ungeanguka"
   
 17. m

  mbungula Member

  #17
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wameshinda dawa yao ni
  nguvu ya uma na maandamano
  tu
   
 18. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msiwalaumu sana CCM wenyewe walituambia kwamba wana wanachama wengi sana watajaza ukumbi so hao ndo wanachama wao...! Sidhani hata kama wamefika 18yrs. So sad
   
Loading...