G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,705
- 36,461
Ukimuona kinagonga akitoka rangi nyeusi kwenda ya kijani kama wewe ni zuzu kwa harakaharaka utaamini kuwa umeona kinyonga mwingine. Kinyonga uliyemuona ni yule yule ila amebadili rangi ili kuendana na maficho ya kijani aliyokutana nayo.
Humu JF na mitaani wana CCM ni wakufananishwa na vinyonga, hata hivyo ukweli ni kuwa wao ni vinyonga walio kwenye muonekano wa binadamu. Hawa hawa wana CCM hawajawahi kuja na lolote jipya zaidi ya kumsubiri mkuu wao wa wakati huo aje na jambo kisha wao washangilie na kuitika kwa nguvu zote kuunga mkono. Ni watu wasioweza kutafakari jambo lolote lile wala kuwa na maono.
Naomba nijinukuu "Wanayofanya kina Polepole na Shaka leo hii ni yale yale waliofanya kina Polepole na Shaka wa mwaka 1997-98, tofauti yao ni aina ya maficho waliyopo, ukomavu wa sura, rangi na ukubwa wa miili!
Wana CCM kwa mtu usiyewaelewa basi jitahidi utengane nao, waogope kama ukoma. Kwa sisi tunaowaelewa huwa tunawapuuza huku tukiamini kuwa hawawezi kuja na jipya lolote litakaloleta changamoto chanya ndani ya nchi yetu.
Sisi tunasubiri tu wale wanaoitwa "safe seat" ya CCM wajielewe kisha tuliondoe dude hili nakulitokomeza nchini ili kuleta changamoto ya uwajibikaji na kufanya kila mmoja wetu ajitambue.
Ni aibu na ushenzi kumsikiliza mwana CCM akipongeza leo kwani hawahawa watapongeza kesho lililo kinyume na la leo ili mradi tu kasema "mkubwa", huu ni uwendawazimu wa aina yake.
Hivyo basi ni lazima watu wajitambue na kuwapuuza wana CCM ambao kwa kweli hata kuwatazama tu hawana kipya zaidi ya vurugu zinazobadilika kila uchwao na kuishia kuliharibu na kuligharimu taifa kwa majanga.