Mjema Vushanje
Senior Member
- Sep 24, 2017
- 158
- 355
WANA CCM WENYE NGUVU LIOKOENI TAIFA!
Naandika hii makala nikijua kwamba watakaonielewa ni WATANZANIA PEKEE, sio watu wa CCM wala watu wa CHADEMA bali WATANZANIA PEKEE.
Ninaposema wana CCM wenye Nguvu simaanishi, JPM, simaanishi Samia, simaanishi Majaliwa na wala simaanishi Bashite, namaanisha wanaCCM wenye nguvu.
Naomba ieleweke kuwa mpaka kufikia 2015 watu waliokuwa na nguvu katika siasa za Tanzania ukiwaacha wapinzani ni Lowassa na Kikwete, nyuma yao kwa mbali alikuwepo BENARD CAMILIUS MEMBE. Leo hii Lowassa yuko CHADEMA na Kikwete amestaafu urais yaani amemaliza muda wake Huku ndani ya ccm Akiwa amebaki Bernard Membe!
Ni nani hasa mwanaCCM mwenye nguvu kwa sasa? Sio mwingine bali ni BENARD MEMBE. Wapo ambao wanaweza wakakataa na kupinga hili lakini nawaambia kuwa JPM anamuhofia B Membe kuliko mwanasiasa mwingine yeyote katika hii nchi! Tuyaache kwanza haya!
Kwasababu naongelea TANZANIA kuokolewa ni lazima niseme Tanzania inaokolewa kivipi na inaokolewa kutoka kwenye nini.
Ni ukweli usiokatalika kuwa nchi yetu iko kwenye hali ambayo sio nzuri, Tanzania iko kwenye hali ambayo ni lazima iokolewe kwa manufaa ya leo na kesho.
Ni nani aliye huru kwasasa?
Wapo wanaoweza kusema kuwa wako huru lakini waupime uhuru wao kwa kusema tofauti na watawala wao na ndio watajua kuwa ninamaanisha nini?
Kuna ambao wapo CCM na wanafikiri kwao sio tatizo lakini nawaambia kuwa kwakuwa kuna makosa mengi tu yanayofanyika ndani ya CCM na ndani ya utawala huu basi wajaribu kukosoa ili waupime uhuru wao, kama Wanadhani kuwa huru ni kukubali bila kukosoa basi nawaambia kuwa huo sio UHURU.
Nina mifano michache ya kuwaonyesha wana CCM jinsi ambavyo nao vilevile hawako huru.
1.Unanjua ni kwanini Nape aliondoka kwenye uwaziri, alijaribu kuonyesha kuwa yuko huru kumbe hayuko huru!
2.Unajua kwanini BASHE, MUSUKUMA na MALIMA waliwekwa ndani wakati wa kikao cha NEC, Walidhani wako huru kama wewe unavyodhani.
3.Umewahi kujiuliza kuhusu SADIFA wakati wa uchaguzi wa UVICCM juzi? Kama hukujiuliza jiulize!
4.Umewahi kujiuliza kwanini Meya wa Jiji la mwanza aliwekwa ndani hadi msafara wa mheshimiwa ukapita kwanza? Jiulize leo.
Unaijua hali ya KINANA?
Ndugu zangu sitaki niseme mengi ila kama tu ndani ya chama kuna hali isiyosemwa waziwazi je kwingine? Ukweli ni kwamba kwasasa kuna haja ya kutafuta watu wenye uwezo wa kubadili mambo kabla hatujajuta zaidi.
Nijuavyo mimi hakuna kitu kikubwa kama uhuru, wakati wakoloni wanatutawala kila kitu tulipata na kama tungewaacha mpaka leo basi tungekuwa na maendeleo makubwa kuliko lakini tulikosa UHURU pekee.
Kwa hali iliyopo kwasasa ni nani yuko salama? Hata kama yuko salama mmoja wetu je? Anafurahi mtindo huu? Anafurahia yeye kuwa salama ilihali taifa liko katika hali hii?
Ndugu zangu ni ukweli usiopingika kuwa katiba ya nchi yetu inamruhusu aliyeko madarakani kuwa kama Mungu wa duniani, kwa hali hii yeyote atakayekuwa tofauti nae awe wa chama chake ama wa chama kingine basi ujue nae hatokuwa salama nah ii maana yake ni kwamba ikiwa kila mtu atataka kuwa salama basi asiwepo mkosoaji hata mmoja.
Sasa namuita MEMBE huko alipo aje, simwambii cha kufanya kwasababu najua anajua cha kufanya, ila asiruhusu ipite 2020 kabla hajajitokeza na kufanya jambo.
Ni wazi kuwa yeye ndie mwenye nguvu kwa wakati huu ya kubadilisha mambo, niyeye pekee ambaye akiinuka leo kutakuwa na msururu wa watu nyuma yake hata hawa watakaopinga andiko langu.
Asifanye hivi kwa manufaa ya chama ama yeye binafsi bali kwa manufaa ya nchi, akisubiri wapinzani wafanye watafanyia wapi? WATAFANYIA WAPI?
1. Hawaruhusiwi mikutano ya hadhara.
2. Wanaondolewa kwenye vyyama vyao kwa mbinu nyingi ambazo zingine siwezi kuzisema.
3. Ukifanyika uchaguzi wowote hawawezi kushinda kwasababu hawatakubaliwa kushinda japo kwa idadi ya kura huwa wanashinda.
4. Wakisema wanawekwa ndani.
Wakisema ni Pyuu, Pyuuuu
Katika hali kama hii nchi haiwezi kuwa na maendeleo na hata yakiwepo kidogo yatakuwa sio ya wananchi na wala hawatakuwa na furaha nayo.
MEMBE ukishindwa mtume hata JANUARY!