Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 26,103
- 34,063
Habarini Wadau,
Ninaandika habari za huyu jamaa ambaye ni Mbunge jina wa Arumeru Magharibi.
Ninaweza kusema huyu ni Mbunge wa ajabu kuliko wabunge wengine ambao nimewahi kuwafahamu.
Ni Mbunge ambaye tangu apate nafasi ya Ubunge hajazungumzia changamoto zilizopo jimboni kwake. Ama lah, hajawahi hata kubuni au kutengeneza mikakati yoyote ya kimaendeleo katika jimbo lake.
Hajawahi kusimama bungeni aidha kwa kutetea hoja yakinifu (Positive ones) au hata kupinga hoja yoyote iliyo na matokeo mabaya kwa wananchi wake.
GIBSON MEISEYEKI amekuwa akisubiriwa na waliompigia kura angalau aende kujionea adha na matatizo wanayoyapata wananchi wake hasa ya kuwa na Barabara mbovu mno zinazotoka mashambani kuingia mjini (Feeder roads)
Barabara hizi ni za muhimu sana na zipo karibu kabisa na Main roads ya Arusha-Moshi, ndizo zinazotoa Cabbages, Carrots, Viazi/ Potatoes, mahindi mabichi, matango na Vitunguu na kupeleka mjini au soko kuu na katika supermarkets. Mvua ikinyesha barabara hizi hazipitiki kwa miguu wala kwa gari au pikipiki.
Mfano mzuri ni barabara ya kuelekea ILBORU SEC, Sanawari, White Rose n.k
Tatizo lingine ni Ukosefu wa Maji katika maeneo hayohayo.
Huyu Mbunge anachojisifia kila Mara ni urekebishaji wa shule ya sekondari ya Enyoito tu, ilihali hata barabara ya kufikia hapo ni mbovu.
Hata kama si yeye anayetatua tatizo hili straight away lakini hata kuona changamoto hizi na kuzungumzia pia hawezi?
Hawezi hata kukaa na Halmashauri na kujadili namna ya kutatua hizi changamoto hata kidogo?
Alichaguliwa ili adeal na kampuni yake ya Tours tu na biashara zake bila kujali matatizo ya wanajimbo lake?
This is too much kwa Mbunge kijana kama huyu.
Mbona G. Lema na Nassari ni Wapinzani na wamekuwa wakiongelea matatizo ya majimbo yao?