Wamtumainio Bwana ni kama Mlima Sayuni, kamwe hawatotetereka

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,304
14,194
Najua unapitia magumu katika haya maisha ijapokuwa unajaribu kuonesha tabasamu lako ila moyoni umebeba huzuni kubwa sana!

Magonjwa yanakuandama, mikosi na mabalaa biashara zako hazisongi mbele, kazi hauna, najua unajiona usiye na bahati sana haswa ukizingatia madeni yanayokuandama.

Usichoke kumtumainia bwana wala kukata tamaa maana alisema ombeni nanyi mtapewa, bisheni nanyi mtafunguliwa na tafuteni nanyi mtapata.
 
Maisha ya mwanadamu ni fumbo kubwa sana. Maana ukianza safari yako ya mapambano utatiwa moyo sana na hongera nyingi sana, ila ukionyesha mafanikio tuu utasikia mchawi, freemason, mwizi alimradi vikwazo vya kukukatisha tamaa kabisa. Bali nakusihi usikate tamaa maana manabii wote walipoianza kazi ya Mungu walitiwa moyo ila walipoanza kuonesha mafanikio waliwekewa vikwazo na wengine mpaka kuuliwa!
 
Sio kila mtu anayekuchekea basi ukajua anakupenda bali moyo wa mtu una siri nyingi mno. Unaweza ona jinsi chuki katika dunia ya sasa ilivyotamalaki haswa, maadui ni wengi katika maisha yako ya kila ila kumbuka kumtanguliza Mungu katika kila jambo maana ndiye mkweli pekee na tumaini letu sote.
 
Back
Top Bottom