Wamiminika kutoa ushahidi mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamiminika kutoa ushahidi mauaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Mar 10, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mamia ya wakazi wa vitongoji vya Oloirien na Kijenge Mjini Arusha jana walijitokeza kutoa ushahidi mbele ya Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuchunguza mauaji ya vijana wawili yaliyofanywa na polisi hivi karibuni.

  Wananchi hao wakiwemo wafanyabiashara, walinzi wa taasisi zilizopo karibu na eneo hilo walianza kumiminika katika viwanja vya Kanisa Katoliki ilikojichimbia Kamati hiyo kuanzia saa mbili asubuhi.

  Katika viwanja hivyo vilivyopo karibu na kituo cha mafuta cha Mount Meru ambacho kinahusishwa na mauaji hayo baada ya mhudumu wake kudaiwa kupigia polisi simu akidai kuwa marehemu waliouawa ni majambazi, walionekana viongozi wa kisiasa na watu maarufu jijini hapa wakijaribu galia mambo yanavyojiri.

  Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa ushahidi, baadhi ya mashahidi muhimu wa sakata hilo (majina tunayahifadhi) walisema kuwa waliulizwa maswali kwa kina kuhusu tukio hilo ambapo walidai kuwa walieleza kwa ufasaha jinsi walivyoshuhdia mauaji hayo yanayodaiwa kuwa ya kinyama.

  ``Mimi ndio niliamua ugomvi na kisha nikaondoka muda mfupi niliporudi nikakuta mauaji, nilishangaa sana kwani ugomvi ulikuwa wa chenji, niliwaambia kila kitu shauri lao, mimi nimenawa mikono yangu,``alisema shahidi huyo.

  Shahidi mwingine alidai kuwa mara baada ya vijana hao kuuawa aliiitwa na askari mmoja na kumtaka aandike maelezo ya kuwa biashara yake iliyokuwa karibu na eneo yaliofanyika mauaji ilitaka kuvamiwa na vijana hao, lakini alikataa.

  ``Mimi nilishangaa, nikasema hadharani sitaki, wakamwita mlinzi wangu sijui kilichoendelea, huo ndio ushahidi niliowapa Kamati,`` alisema shahidi huyo.

  Katika hatua nyingine, miili ya vijana hao Shedrack Motika na Ewald Mtui imefanyiwa uchunguzi wa kitaalam na madaktari maalum kutoka Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro na makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam.

  Wakati wa zoezi hilo likifanyika, ndugu wa marehemu walikuwa wametanda katika eneo la Hospitali ya Mkoa Arusha kufuatilia hali ya mambo.

  Hata hivyo, mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa na kwamba taarifa kamili juu ya sakata zima litatolewa mara baada ya Kamati kumaliza kazi zake wiki ijayo.

  Kamati hiyo yenye watu saba inayoongozwa na Mwanasheria wa Serikali Kanda ya Kaskazini, itaendelea tena kupokea maoni na ushahidi wa wananchi kuhusu tukio hilo. Pia itazuru eneo la mauaji yalikofanyika.

  Mauaji hayo yanayodaiwa kuwa ya kinyama, yalifanywa na polisi Machi mosi mwaka huu baada ya mhudumu wa kituo cha mafuta cha Mount Meru kuzozana na marehemu hao.

  Mhudumu huyo alidaiwa kumwarifu tajiri yake ambaye naye aliwapigia polisi simu ambao baadaye waliwaua vijana hao, Ewald Mtui na Shedrack Motika.

  Tukio hili linaelezwa kushabihiana na jingine lililotoea katika Jiji la Dar es Slaam mwazoni mwa mwaka 2006 ambalo polisi waliwaua wafanyabishara watatu na dereva teksi mmoja.

  Polisi walidai watu hao walikuwa majambazi, lakini baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda kwa Tume ya uchunguzi iliyoongozwa, Jaji Kipenka Musa, iligundua kwamba waliouawa hawakuwa majambazi.

  Kutokana na ripoti ya Jaji Musa mashitaka ya mauaji yalifunguliwa dhidi ya polisi 13, kati yao akiwamo aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe, pia akishikilia wadhifa wa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kutokana na fundisho la kesi inayowakabili wakina Zombe, hawa jamaa watakuwa makini sana kwa uchunguzi wao. Yetu macho na masikio si muda mrefu haki itatendeka.
   
 3. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huku tukiikemea police na sisi raia tuepuke maugomvi yasiyo ya msingi hasa sehemu za biashara kama hizo ambazo zinaandamwa na majambazi usiku kucha,maana mwizi hana alama ya kumtambua,watu wafuate sheria kama umedhulumiwa fuate taratibu za kudai haki zipo! siyo fujo zisizo na msingi na kukoz umauti,ila yetu macho ngoja tuone
   
 4. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yap watu sasa hivi hawataki utani kabisa hawataki kuona wenzao wanapotea kiuzembe uzembe ni vizuri hivyo walivyofanya kujitolea!!
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu ni wadhaifu sana katika maamuzi, ninadhani muda wa miezi sta CCP hautoshi. Hi ni polisi wa level ipi anayeruhusiwa kutembea na pistol? kinacho nishangaza ni udhaifu wa kuchukua hatua.

  Kwa mfano, polisi walioua Dar hawakukamatwa kwa muda mrefu eti yanasubiriwa mapendekezo ya tume, mpaka Afande alawi (aliyefyatua risasi) akakimbia. Hata hii ya Arusha nasikia polisi hawajakamatwa, hivyo wanaweza kukimbia muda wowote. Tunamatatizo makubwa sana katika maamuzi.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mauaji haya yamenihuzunisha sana na yananikumbusha miaka 90 mwishoni kulitokea mauaji ya vijana sita wa mjini Arusha ambao... huenda walisingiziwa/walihisiwa/walihusika... katika plot ya kuvamia gari la benki kutokea Kiteto, kati yao kulikuwa na mtoto wa Mzee Kileo!!!! Tajiri mashuhuri/maarufu sana hapo Arusha,ambaye anamiliki Hotel na biashara nyingi toka enzi miaka ya 80 mpaka leo aliyekua anaitwa Alfred BABU Kileo huyu alikuwa mtu wa karibu kwangu kwa kipindi fulani... tukiwa teen-agers... Ninapoandika habari hii machozi yananilengalenga kwani nahisi kama nami ningekuwa naishi Arusha na nikawa naye huyo rafiki/ndugu/mshikaji wakati huo huenda na mimi ningekumbwa na dhahama hiyo!!! sikumbuki RPC wa wakati huo alikuwa nani??? lakini nachotaka kusisitizia hapa kama nilivyosema awali "huenda walisingiziwa/walihisiwa/walihusika... katika plot ya kuvamia gari la benki kutokea Kiteto" nakumbuka kusikia walikuwepo katika gari ambalo walichukuana kishikaji tu lakini njiani (nadhani maeneo ya Mbauda kuelekea Oljoro )wakakutana na dhahama hiyo... katika group hiyo mmoja tu ndio alikuwa na Record za ujambazi/wizi/udokoaji... na walipokuwa eneo hilo kati ya (nadhani maeneo ya Mbauda kuelekea Oljoro )walikamatwa na Police wakatiwa jambajamba za hapa na pale... kisha wakapelekwa kituoni... Central ya Arusha wakiwa wazima... Wazazi na wananchi waliwaona wakiingia na pale wakiwa wazima wa afya tena bila ya michubuko... hiyo ilikuwa saa tano au saa sita za mchana... lakini ilipofika jioni UMMA ukataarifiwa kuwa wamekufa kutokana na kipigo cha wananchi waliojichukulia sheria mikononi...Naaam WOTE SITA!!! Ukiachilia mbali yule mmoja aliyekuwa na historia...ujambazi/wizi/udokoaji... ambaye aliwapeleka askari anapo-hifadhi silaha zake wengine waliteswa mpaka kikomo cha maisha yao... Nakumbuka wazazi walifungua kesi ... Hivi Mzee Kileo na wazee wenzako na UMMA wa Arusha kwa ujumla ile kesi ilikwishaje?????????????????????????
  Nadhani Kesi hii ya vijana wawili ambaye mmoja ni kinda ONLY 22yrs old itawafungua macho wakati Babu Kileo na wenzake wanauawa na Polisi huyo Shedrack Olais Motika alikuwa na miaka 8+ ...NO COMMENT
  RIP Babu... and ze fellaz... RIP Shedrack and Edward...

  Nafsi zenu hazikupotea/hazijapotea bure...
   
Loading...