Wamiliki wa vituo vinavyouza mafuta machafu wahukumiwa

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..natarajia hukumu hii itakuwa fundisho kwa wengine.


..ziandikwe sheria kali zaidi kwa wanauza mafuta/bidhaa feki Tanzania.


Mwananchi said:
Walipa Sh10 milioni kwa kukaidi amri ya Ewura


Nora Damian


MAHAKAMA Kuu imewaamuru wafanyabiashara wawili wa mafuta kulipa faini ya Sh10 milioni na kifungo cha miezi sita nje, baada ya kukaidi amri ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ya kufunga vituo vyao.

Wafanyabiashara hao ni Mohamed Nahdi na nduguye Abdulatif Nahdi ambao ni wakazi wa Morogoro.



Vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na Abdulatif Nahdi ambavyo vimefungiwa ni Kobil Msamvu Petrol Station na Abdulatif Petrol Station, wakati vituo vya Nahdi vilivyofungwa ni Mohamed Twalib Petrol Station, Oilcom Kihonda Petrol Station na Mohamed Twalib Oilcom Petrol Station.



Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki baada ya Jaji Thomas Mihayo wa mahakama hiyo, kanda ya Dar es salaam baada ya kuwatia hatiani wafanyabiashara hao kwa kosa la kudharau amri ya Ewura.

Katika hukumu hiyo, Jaji Mihayo alionya kuwa yeyote atakayekiuka amri ya mamlaka atachukuliwa hatua kali za kisheria na kwamba, aliamua kutoa adhabu nafuu kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa sheria hiyo ya Ewura bado ni mpya na kuwataka wajirekebishe na iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye tabia kama hiyo.

Jaji Mihayo aliwataka wafanyabiashara hao kutotenda kosa kama hilo ndani ya miezi sita na kutoa muda wa wiki mbili kila mmoja awe amelipa faini ya Sh5 milioni.



Ewura ilifungua maombi mahakamani hapo ikiomba wafanyabiashara hao waitwe na kujieleza kwa nini wasifungwe gerezani kutokana na vitendo vyao vya kuchana karatasi zilizoandikwa amri hiyo, kung'oa lakiri na kuendelea kuuza mafuta yasiyostahili kinyume cha sheria.



Kwa mujibu wa hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na wakili James Kabakama, Ewura ilitoa amri hiyo Septemba 19 mwaka jana kwa wafanyabiashara hao ya kuwataka kufunga vituo vyao baada ya kukutwa wakiuza mafuta yasiyostahili.



Ilidaiwa kuwa Ewura walifanya ukaguzi wa vituo vyote vya mafuta mkoani Morogoro kati ya Septemba 13 na 14 mwaka jana na kubaini vituo vya wafanyabiashara hao kuwa vilikuwa vikiendelea kuuza mafuta yasiyostahili.

Kitendo hicho kiliifanya Ewura kufunga visima hivyo kwa kutumia lakiri maalum.


Hata hivyo wafanyabiashara hao waling'oa lakiri hizo na kuendelea kuuza mafuta machafu kwa muda wa wiki mbili, hali iliyoifanya Ewura kutumia polisi kufunga vituo hivyo kwa nguvu na kuwatoza faini ya Sh 66 milioni.
 
Back
Top Bottom