Wameniibia....

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,102
Habari wanajamvi
Nimeiibiwa laptop aina ya lenovo C300 rangi ya shaba: vitu mhimu vilivyomo ni pamoja na software mbali mbali nilizozitengeneza kwa kutumia VB na SQL kama vile School management, Payroll, Inventory, Library, pharmacy…..
Tafadhali ikipita mikononi mwako nitaarifu maana pigo kubwa ni hizo software. Zawadi nono kwa atakaye wezesha kupatikana.
 
Pole sana mkuu
Next time fanya backup ya vitu vyako muhimu sehemu tofauti tofauti, online, flash, external disk, cds nk
 
Pole sana mkuu
Next time fanya backup ya vitu vyako muhimu sehemu tofauti tofauti, online, flash, external disk, cds nk
Asante sana kwa ushauri wako.......Nilikuwa kwenye process za ku-buckup nikaisha ofisini ili iendelee kuhamisha data kwahiyo wamekuja kuiba laptop pamoja na extenal disk......
 
Asante sana kwa ushauri wako.......Nilikuwa kwenye process za ku-buckup nikaisha ofisini ili iendelee kuhamisha data kwahiyo wamekuja kuiba laptop pamoja na extenal disk......
Umeibiwa sehemu gani mkuu
Mimi walikwapua yangu mlimani city kwenye gari, katika kufuatilia walinzi wakaniunganisha na wezi nikainunua tena, nikakuta wamefuta kila kitu, sema uzuri nilikuwa na backup ofisini, desktop ya nyumbani na external disk huwa sitembei nayo na online pia, kwahiyo haikuwa tatizo
 
Mkuu funguza zawadi sasa,maana anaweza akatokea teja akaniuzia kwa laki 2,namie nikaenda kuuza kwa laki 5 faida laki 3,sasa taja mpunga hili uweze kushawishi mtu!
 
Umeibiwa sehemu gani mkuu
Mimi walikwapua yangu mlimani city kwenye gari, katika kufuatilia walinzi wakaniunganisha na wezi nikainunua tena, nikakuta wamefuta kila kitu, sema uzuri nilikuwa na backup ofisini, desktop ya nyumbani
na external disk huwa sitembei nayo na online pia, kwahiyo haikuwa tatizo

Mkuu hapo kwenye red umenipa nukta, kuanzia sasa sitatembea na external hard drive yangu pamoja na laptop!!
 
pole mkuu, mimi mwenyewe nina Back Up kwenye Desktop home na External HDD na hua sitembei nazo
 
Weka dau watu tuingie kazini....kama linalipa mie kama middo man nitakula kamisheni 30% kutoka kwa mnunuzi na 20% toka kwa muuzaji...deal?
 
Kaka pole sana upo sehemu gani?

wewe uko wapi?

Pia sema wapi tukio limetokea na lini...the earlier the better....
Mkuu,
Nadhani umetangaza ili usaidike na wanajamii!
SAsa kama unaulizwa swali kuwa uko wapi na hujibu inakuwa haina maana!
Kuna jamaa alipita Arusha akaibiwa ipad na watoto wa kihuni eneo la maktaba ya mkoa, akapandisha thread hapa, na baada ya watu kuona tulifanya mchakato wa haraka haraka, na kupitia kwa Preta hiyo ipad ilijulikana mahala ilipo, na tukamtuma aliyeibiwa aende akainunue fasta!...japokuwa baada ya kuinunua hakurudi hata kusema neno la shukrani, mbaya zaidi ni member hapa!

Sema uko mkoa gani, na eneo gani!
Kama ni Arusha weka hadharani, watu tuingie mtaa, hizo ndio kazi zetu!

 
Pole.
Backup kwa kutumia cloud kuongeza usalama mimi natumia DropBox na iDrive, tena kama unadevelop sana angalia service kama GitHub hii ni version control sytem ambayo iko hosted bure kwa ajili ya open source projects.
 
mimi juzi nimeji-register kwenye Network flan inaitwa Prey-project inahusika naku-trace stolen laptop! ila cjajua vizur kama kwel inaweza kutrace!
 
Kumbe inawezeka?!

Mimi waliniibia kama 3wks ago (Moshi-mjini) sikuona sababu ya kutangaza hapa maana nilijua imeisha kula kwangu basi, na sasa nipo kwenye mchakato wa kutafuta nyingine.

Anyway, ingawa ni siku nyingi sasa ila kama ikitokea ikapita mikononi mwenu naomba msaada wenu wakuu. Kiukweli nahitaji sana kuipata. Haijalishi ni kwa gharama gani lakini nikiipata nipo radhi kubagain whatsoever.

Inaonekana kama hivi.

Spcs: HDD 500gb, RAM 4gb, Inch 17.3"

Lakini pia kuna mkwaruza upande wa nyuma ya screen. Inapokuwa on, ile chata ya hp nyuma ya screen huwa inawaka.

Natanguliza shukrani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom