Habari Jamii yangu ya humu ndani.
Nasikitika sana baada ya masaa kadhaa kupita ndio napata notification kwamba kuna mtu/kikundi cha watu wameweza kuingia kwenye account yangu ya twitter na kufanya walichofanya then wakatoka.
Nimeshindwa kuscreenshot ule ujumbe kwa sababu zangu binafsi . lakini ujumbe unaonesha aina ya device waliotumia, Location ambayo ni unknown na muda, siku na saa na mwisho wakanishuri kubadilisha nywila/password yangu.
Bado nazidi kujiuliza wanaofanya shughuli hizi/udukuzi wanafanya kwa malengo gani, wanalenga watu gani.
Ndugu zangu nimeleta hili swala mbele yenu nipate mawazo yenu tofauti.
Karibuni sana
Mimi Mwana JF