Walter Reed Tanzania, kwa anayeifahamu

Walter Reed Tanzania, kwa anayeifahamu

Kazegunga

Member
Joined
Jun 24, 2014
Posts
58
Reaction score
3
Naombeni sana wana jamii forum kunijuza hii walter reed kimalipo kwa mtu mwenye degree analipwaje?
 
mshahara ni matokeo ya mambo mengi ikiwamo ujuzi na uzoefu wako,kiwango cha elimu,mshahara wako wa sasa nk.hivyo ni suala la majadiliano tu kati yako na mwajiri.
 
nenda ukakubaliane nao, na si hapa, maana mshahara inategemea hata kama una degree lakini uzoefu wako ni miaka 4, na mwingine ana degree lakini hana uzoefu, hamuwezi kulipwa sawa, kikubwa kafanye kazi uendeleze career yako.
 
Nenda kama mshahara hautakidhi matakwa utaendelea kutafuta marisho bora kabisa
 
nawafahamu wapo vizuri...kima cha chini mshahara ni milioni na nusu...wengine wanalipwa hadi milioni 6 ...kuna mchanganyiko wa wafanyakazi...kuna wabongo waliosoma nje, kuna wakenya na wazungu. wanafanya kazi chini ya mfuko wa rais wa marekani. wanasimamia mshirika yanayojihusisha na mambo ya ukimwi na ukatili wa kijinsia mikoa ya mbeya, rukwa, songea, na katavi
 
Wapo vizuri si wametupatia landcruisuer Mpya tushughulikie masuala ya ukimwi ila wameifunga GPS
 
Nawafahamu vizuri sana. Itoshe kukuambia kuwa kile ni kitengo che jeshi la marekani hivyo hela kwao sio issue. Issue ni uwezo wako wa kuwaconvice kuwa unauwezo wa kuderiver and unavigezo vya kupata hiyo kazi. Halafu mtu unatakiwa ujue bei yako dunia ya leo. Useme kabisa kuwa mimi ukinivuna kwa mwezi nitakupa matokeo haya ambayo thamani yake si chini ya kiasi kadhaa. Full stop.
 
mkuu kama umeitwa huku njoo wanalipa posho nzuri mke wangu anafanyia hapo yupo kitengo sha laboratory tecnision. so ww piga kazi. mbeya nzima hii ndio mradi inayolipa vizur. mm ninaijua vilivyo
 
Japo hii Thread ya siku nyingi, Ila nami wameniita tarehe 9 June, next week alhamisi, huko mbeya; Wamenipigia simu, pia wametuma email yenye maelekezo mengi yu ikiwamo kurudishiwa gharama za usafiri na malazi nitakapokwenda kwenye usaili wao huo.
Mwenye Update mpya za mwaka huu atujuze jamani. Naomba kuwasilisha
 
Japo hii Thread ya siku nyingi, Ila nami wameniita tarehe 9 June, next week alhamisi, huko mbeya; Wamenipigia simu, pia wametuma email yenye maelekezo mengi yu ikiwamo kurudishiwa gharama za usafiri na malazi nitakapokwenda kwenye usaili wao huo.
Mwenye Update mpya za mwaka huu atujuze jamani. Naomba kuwasilisha
Vipi mkuu ulifanikiwa kupata kazi?
 
Back
Top Bottom