Walokole wamwombea trafiki barabarani

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,400
Walokole waliokuwa katika coaster mbili wakienda kutoa mapepo maeneo ya Kiloleli mjini Mwanza walizua taharuki baada ya kuanza kumwomea trafiki kwa madai ana mapepo baada ya trafiki kulisimamisha gari lao.

Walokole hao waliokuwa wamejawa na roho mtakatifu walianza kunena kwa lugha na kumkemea huku wakimzunguka na wengine wakimkwida na wakitaka kumbeba kwa madai anahitaji maombezi zaidi.

Taharuki ilizidi kuwa kubwa hadi mchungaji wao alivyofika na gari dogo na kuwasihi wamwache kwani siye waliyewaitwa kwenda kumwombea.
 
Huyo trafic alikuwa wapi? Kilichokuonesha kuwa wamejaa roho mtakatifu ni nini.

Weka picha maana ulikuwepo na umepost hapa na smart phone yako
 
Ningeweka clip nadhani mapepo yameidilit, walokole hao walikuwa wa kanisa winners chapel la mwanza walikuwa katika gari mbili za kingdom schools walikuwa wakitokea kanisani.
 
Alikuwepo jamaa sijui ndio katekista? Alikuwa amevaa suruali nyekundu koti jekundu na tai nyekundu huyo jamaa kwa kunena kwa lugha ni mwisho! Trafik alivyokuswa bega akabaki amezubaa huku maombezi yakipamba moto wakimkokota kuelekea ndani ya gari hadi mwenzie alivyokuja kumvuta.
 
Ningeweka clip nadhani mapepo yameidilit, walokole hao walikuwa wa kanisa winners chapel la mwanza walikuwa katika gari mbili za kingdom schools walikuwa wakitokea kanisani.
Winners Chapel Intl hawawezi fanya huo ujinga, na kwa jumapili gari hizo za Kingdom Schools huwa zinapeleka watu makanisani na kuwarudisha makwao kutoka mitaa mbali mbali ya jiji la miamba!!! Perhaps, utakuwa ulikuwa unaota kukwidwa na mapepo yenyewe...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom