....Walipoenda kutafuta kuni CCM,......CHADEMA wanatoka kukata kamba!

Oti Kate

Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
58
Reaction score
59
Ndugu zangu,

kwa muda mrefu, takribani tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 upite hadi sasa tukiwa tunaeleka mwaka 2015 ambako tutakuwa na uchanguzi mkuu mwingine, kuna kitu nimekiona. CCM kwa ufupi hakujatulia na ni kama vile hawana tena imani ya kurudi magogoni. Yaani wanafanya lolote lile bila kujali faida au hasara yake ili mradi kwao wanahisi litawasaidia kurudi tena magogoni. Ukitaka kujua mwisho wa CCM umefika na wamebaki kutapatapa angalia haya yafuatayo:
1. Jinsi makundi yalivyoongeza malumbano. Zamani tofauti zao zilikuwa zikiishia CHIMWAGA, lakini siku hizi hakuna
CHIMWAGA wala wapi, popote hao ni sawa .....kama kwenye media etc

2. Tazama serikali inayoongozwa na CCM jinsi ilivyokosa umakini......kuna matukio mengi kwa mfano ya utekaji Doctor Ulimboka na Kibanda, kwa serikali makini ingetumia kurudisha imani kwa wananchi wake kwa kusimamia misingi ya haki na kuwatia mbaroni wahusika wote na kushughulikiwa kisheria......lakini tunaambiwa kuwa serikali ndio ilihusika, na yenyewe wala haikupinga badala yake inaunda tume za uchunguzi!

3. Fatilia matamko mbalimbali yanayotolewa na watu wenye dhamana ya uongozi ndani ya chama....kwa mfano Katibu wake wa uenezi taifa, bado utagundua hiki chama kinatapatapa.

Kwa mtazamo wangu, nadhani CCM wamefikia mwisho wa kutawala nchi, so ndio wanatuaga watanzania.....hii ni sawa na kusema CCM walijisaha sana tangu washinde kimagumashi uchaguzi wa mwaka 2010, so CHADEMA wakaanza koukota kuni. Leo CHADEMA wameshamaliza kuokota kuni wanakuja na kamba kufunga mzigo na kuanza safari ya kuelekea magogoni , basi CCM ndio wanaenda kutafuta kuni wakati it's too late.............VIVA CHADEMA!
 
Ila mzigo bado hapo Dar, kwanza ndo hakueleweki kabisaaa!
 
hizi dalili zilishadhihirisha kifo chaja tunasubiri kitakuwa ni kifo cha aina gani,cha mende,kibudu ama cha usingizini
 
Mtenya kuni naye awe makini,wasije wakatenya na kuni zenye mchwa .
 
....ni kama yule mama..."anayekumbuka kumlisha mtoto siku ya Clinic akitegemea ataongezeka uzito"....
 
Ndugu zangu,

kwa muda mrefu, takribani tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 upite hadi sasa tukiwa tunaeleka mwaka 2015 ambako tutakuwa na uchanguzi mkuu mwingine, kuna kitu nimekiona. CCM kwa ufupi hakujatulia na ni kama vile hawana tena imani ya kurudi magogoni. Yaani wanafanya lolote lile bila kujali faida au hasara yake ili mradi kwao wanahisi litawasaidia kurudi tena magogoni. Ukitaka kujua mwisho wa CCM umefika na wamebaki kutapatapa angalia haya yafuatayo:
1. Jinsi makundi yalivyoongeza malumbano. Zamani tofauti zao zilikuwa zikiishia CHIMWAGA, lakini siku hizi hakuna
CHIMWAGA wala wapi, popote hao ni sawa .....kama kwenye media etc

2. Tazama serikali inayoongozwa na CCM jinsi ilivyokosa umakini......kuna matukio mengi kwa mfano ya utekaji Doctor Ulimboka na Kibanda, kwa serikali makini ingetumia kurudisha imani kwa wananchi wake kwa kusimamia misingi ya haki na kuwatia mbaroni wahusika wote na kushughulikiwa kisheria......lakini tunaambiwa kuwa serikali ndio ilihusika, na yenyewe wala haikupinga badala yake inaunda tume za uchunguzi!

3. Fatilia matamko mbalimbali yanayotolewa na watu wenye dhamana ya uongozi ndani ya chama....kwa mfano Katibu wake wa uenezi taifa, bado utagundua hiki chama kinatapatapa.

Kwa mtazamo wangu, nadhani CCM wamefikia mwisho wa kutawala nchi, so ndio wanatuaga watanzania.....hii ni sawa na kusema CCM walijisaha sana tangu washinde kimagumashi uchaguzi wa mwaka 2010, so CHADEMA wakaanza koukota kuni. Leo CHADEMA wameshamaliza kuokota kuni wanakuja na kamba kufunga mzigo na kuanza safari ya kuelekea magogoni , basi CCM ndio wanaenda kutafuta kuni wakati it's too late.............VIVA CHADEMA!

CCM inakufa ni jambo la wazi kabisa , lakini cha kusikitisha zaidi ni kuwa mifumo yetu ya kiutawala haijaandaa utaratibu wa kuachiana serikali kwa chama kingine, aidha ni bahati mbaya pia kuwa vyama vya upinzani pia bado havijawa na mifumo mizuri ya kueleweka kuongoza dola hali inayosababisha wasi wasi mkubwa miongoni mwa wananchi na pengine inapunguza morali ya wao kuchagua mabadiliko.

La muhimu upinzani upiganie ujenzi wa taasisi imara kama tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, nk na serikali lazima itengeneze mifumo imara ya kiuongozi ili chama chochote cha siasa kiweze kuongoza serikali na kuondoa hofu kwa wananchi kuchagua wanayetaka awaongoze.
 
Tungepata watu 10,000.katika Tanzania ya leo tunapotaka mabadiliko ya kweli!?Mungu atujalie hekima na utashi waTanzania,keep it up brother!
 
Back
Top Bottom