Hapana, mimi nilipiga kelele sana mpaka nikaleta ushahidi kuwa mbuga za Keystone huko Marekani zinazotanda kati ya majimbo ya Montana, Wyoming na Idaho zina barabara ndefu sana za lami lakini wanyama hawajahi kuhama, na bado mbuga hizo zinahesabiwa kama ni World Heritage. Mimi ni mwanasayansi niliyeiva vywa kutosha, kwa hiyo huwa ninaamini sana matokeo ya kisayansi kuliko kitu chochote kile. Wapiga debe wote waliokuwa wakipinga, hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuleta data za kisayansi zaidi ya speculations na conjectures tu.
Ningekubaliana nao kama mpango ulikuwa ni kujenga hoteli au makazi ya binadamu, lakini barabara inayopita nonstop kama ambavyo ilivyo barabara inayopita humo humo Serengeti kwenda Mugumu (ambayo imekuwapo kwa takriban miaka hamsini) ni madai ya kitoto ambayo eti serikali yetu ya walala hoi imenywea. Ile barabara ya lami kutoka Mwanza kwenda Bunda inapita mbugani ingawa ni nje ya mpaka official. Kila siku kuna wanyama wengi sana wanacross barabara ile kwenda kunywa maji Ziwa Victoria na wala hawajaacha kufanya hivyo pamoja na kuwa magari yanapita pale kila siku.
Kwa vile jamaa wanataka kujenga barabara nyingine siwezi kulalamika sana iwapo barabara hiyo mpya haitaongeza umbali mrefu sana. Pale
Ndugu,
Wewe kweli ni mwanasayansi uliyeiva kama unavyojisema iwapo leo hii unafananisha mbuga za USA ambazo nyingi ni man -made (zenye sisimizi, mijuzi, nyoka, kanga na tujinyama tudogo tudogo ) na serengeti ?. Je unaelewa migration ya serengeti -composition ya wanyama ect mpaka uifananishe na hizo mbuga za kutengeneza ?
Kama unaamini sayansi na umeiva, unajua EIA, na mara ngapi reports za hii kitu zilibainisha kuwa negative impacts ni nyingi kuliko positives ktk huo mradi licha ya juhudi za makusudi za kulazimisha data zichakachuliwe mpaka DG Bigurube akaamua kijistaafia mapema kuachana na pressures hizo za hawa walafi ?? Licha ya juhudi za kushauri sehemu mbadala ambazo barabara hiyo labda ingepitishwa na kuleta minimum impact, mijamaa bado iling'ang'ania ipite hapo hapo wanapotaka... ???
Mjumbe mmoja hapo juu kagusia issue ya wakuu wa nchi kukimbilia kule kupumzika, teta soon baada ya uchaguzi !! Huu mradi wala JK sio kwamba ana nia ya kutaka kusaidia wananchi. Kama ana nia hiyo, basi kwa nini wasiboreshe hata kuweka lami barabara ile ya kwenda Mugumu ? Hao wenye pesa waliowekeza Grumeti, na wenye hiyo miradi kama hiyo hoteli ambayo jamaa ndo huwa wanajirusha kila mara wakiwa kule ndo wapo behind, na god knows wana nia gani haswa...!!
Hizi kelele za AWF sijui kulaumu WWF ni blah blah tu, wezi wanagombana maana mmoja kawahi ambapo mwingine alikuwa anapigia mahesabu kwenda kuiba tuu. Hao AWF wenyewe wana madudu yao pia, na huyo boss wao alikuwa bongo kama peacecorp miaka hiyooo, akafanya kazi zake alizotumwa weee mara ghafla bin vuu akajiunga AWF, mara technical advisor Tanapa, then Nairobi na sasa katulia USA !
In short, hakuna faida yoyote ecologically, economically wala socially ya hiyo barabara kwa taifa. Sana sana ni miradi ya wachache na siajabu badala ya madege kutua KIA kuiba wanyama sasa wanaota kuwafuata huko huko karibu labda na makopta, au kwa kuwasafirisha kirahisi. Kumbuka hao hao ndiyo waliopigiwa chapuo na JK na nadhani bado wana mahesabu ya kujenga uwanja mkubwa wa ndege huko kando kando ya mbuga. Usijeshangaa siku moja kusikia ni hao hao waliomtungua "joji" yule faru ambaye kwa ulinzi wanaopewa na zile tracking divices sio rahisi mkurya jangili wa kawaida aweze kuua na kuondoka na pembe (usanii huu unaweza kuwa ulichorwa ili kuonyesha barabara ni muhimu kwa ulinzi...) hasa baada ya mbwembwe za JK siku alipokwenda kuwapokea wale faru (na hela za kuwanunua % kubwa zilitoka kwa hao hao) !!
Pole sana kama kuna mtu anafikiri JK anaweza buni mradi wowote wenye 100% manufaa kwa wananchi wa Tanzania.......!! Big up Jaluo, kwa kusikiliza kilio cha wapenda mazingira na wananchi ambao wanataka kuona hazina hii tuliyonayo inabaki ilivyo kwa manufaa ya vizazi vijavyo !!