Waliovunjiwa Nyumba Bagamoyo wakwaa kisiki Mahakamani

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Huzuni imetawala kwa wakazi wa Mtaa wa Udindivu Kata ya Mapinga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya Mahakama ya Wilaya hiyo kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na wananchi hao katika shauri na 18330/2025.

Wananchi hao wakiongozwa na Agnes Lupembe walilofungua kesi mahamamani hapo wakidai kuvunjiwa nyumba zao na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Bw. Dismas Chandika na wenzake watatu pasina utaratibu kufuatwa, hivyo wakiiomba mahakama itamke kwamba washtakiwa wana kesi ya kujibu na wachukuliwe hatua za kisheria.

Soma pia: Wakazi 700 Bagamoyo wapeleka kesi Mahakamani kudai kubomolewa nyumba zao kinyume cha Sheria

Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo umesomwa leo Oktoba 13, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Vedasto Mwaria akieleza kuwa waleta maombi(Agnes Lupembe na wenzake) hawakutoa muda wa kutosha kwa polisi kuweza kufuatilia madai yao juu ya uvamizi waliofanyiwa na washtakiwa lakini pia hapakuwa na uthibisho wa malalamiko ya waleta maombi kuwa Jeshi la Polisi lilikataa kuwasikiliza walipowasilisha malalamiko yao.

Hakimu Mwaria ameeleza kuwa upande wa waleta maombi ulilalamika kuharibiwa na kuibiwa mali lakini hawakuainisha nani aliiba mali ipi ya thamani ipi katika viapo vyao.

Wakili Revocatus Sedede kwa niaba ya waleta maombi ameeleza kuwa wateja wake wameamua kwenda hatua ya juu zaidi kwa kukata rufaa na hivyo muda usio mwingi kutokea leo watawasilisha rufaa yao katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo.

Naye Bi. Agness Lupembe amesema wanaiomba serikali kuingilia kati hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanawashtaki kwani walivunja na kuchukua mali zao hali ya kuwa ardhi waliyokuwa wakiishi kwa sasa ina mgogoro na kesi ipo Mahakama Kuu ya Tanzania divisheni ya Ardhi.
 
View attachment 3488329

Ndo huku Udundivu kwa kina hydroxo?
 
Back
Top Bottom