Waliotoka upinzani wang’ara CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliotoka upinzani wang’ara CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 27, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  NYOTA za wanasiasa machachari wanaotoka kambi ya upinzani na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinazidi kung’ara kwa baadhi yao kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho tawala.

  Katika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Iringa Mjini uliofanyika juzi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi kwa miaka mingi, Elliud Mvella amechaguliwa kwa kishindo kushika nafasi hiyo.

  Ushindi wa Mvella ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA), unaongeza idadi ya wanasiasa kutoka upinzani waliowahi kupata na wanaoendelea kushika nafasi kubwa ndani ya CCM mkoani hapa na kwingineko nchini kote.

  Mvella maarufu kwa jina la Wamahanji, alichaguliwa kuongoza akipata kura 106 dhidi ya kura 34 alizopata mpinzani wake wa karibu, Gerald Chuwa aliyekuwa pia kada maarufu wa NCCR-Mageuzi kwa miaka mingi. Lucas Mgongolwa alipata kura 16.

  Nafasi ya Mwenyekiti katika jumuiya ilijazwa katika uchaguzi huo baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake Emmanuel Mubamange kuteuliwa kuwa Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

  Shughuli ya kumtangaza Mvella kushinda nafasi hiyo, nusura iingie dosari baada ya wajumbe kutaka kwanza taarifa ya mapato na matumizi ya fedha na michango mingine iliyochangwa na wahisani mbalimbali kufanikisha uchaguzi huo.

  Wajumbe hao 156 walitaka kupata taarifa hiyo baada ya kila mmoja kupewa Sh 1,000 tu ikiwa ni posho ya kushiriki mkutano huo wa uchaguzi uliodumu kwa takribani saa sita.

  Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Sarafina Ngwenga alimuomba Mvella atoe msimamo kuhusiana na ombi la wajumbe hao.

  Mvella alisema kwa wanaomfahamu ni mtu anayependa kufuatilia mambo kwa kina na aliwatoa wasiwasi wajumbe kwa kuwaahidi kwamba hata kama taarifa hiyo haitatolewa katika mkutano huo, atahakikisha wanaipata wakiwemo waliochanga.

  Aidha, Mvella aliwahakikishia wanachama hao kwamba jumuiya yake inaanza kujipanga ili kuzitwaa kwa mara nyingine tena kata mbili za Gangilonga na Miyomboni ambazo madiwani wake kupitia chama hicho walifariki dunia kwa nyakati tofauti mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

  Source: Habari leo
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  TAMBE HIZZA anazidi kuipaisha CCM
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hivi Habari leo ni gazeti gani?
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Sijashangaa kuona hii habari kwenye gazeti hili.Magazeti ya udaku yanajulikana.Vipi uhuru na jambo leo hawajaiona pia??? Au wanakubaliana habari za kuandikwa.
   
 5. delabuta

  delabuta Senior Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani ccm ya wendawazimu kama tambwe hiza umetumwa hatujibu ujinga wako humo
   
 6. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Hatushangai tunasubiri na Jumuiya ya familia ichague M/kiti. Hivi Lamwai jamani ndio kapigwa tope la macho. Kweli alikuwa na njaa.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Ni hafadhali ungeanzisha thread ya Bambo na kingwendu ni maarufu kuliko huyo mtu, kwanza hilo jina mimi ndio naliona leo humu JF.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii thread is by far substandard to be posted here.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Hehehehe hivi unaweza kung'ara kweli kwenye chama ambacho hakikubaliki na Watanzania walio wengi ambacho pia kinaelekea kaburini!?
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni HABARI LEO? Anyways, one huge tree doesnot make a forest!
   
 11. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwongeze Dr. Amman Kaburu Shaibu Akwilombe waliopata kuwa CHADEMA, Lamwai (NCCR) na vibaraka wengine kama Mrema ambaye kujikomba kwake kwa CCM na Kikwete sasa kunatia kichefuchefu.
   
Loading...