Waliotaka Katiba mpya kumbe wanacheza kombolela tu!

kayogo

Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
75
Reaction score
42
“IF I have told to choose between my country and my party I will choose my country”, ndivyo anavyosema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu.

Alikuwa akimaanisha nini? “Kama ningetakiwa nichague (kitu) kimoja kati ya nchi yangu (Tanzania) na chama changu (cha Chadema) ningechagua nchi yangu”.

Naam. Hilo ndilo jibu la uhakika alilosema profesa huyo kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) cha Mwanza, yule ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba.

Nani alikuwa akijibiwa namna hiyo na Profesa Baregu au kwa nini alitoa jibu hilo na tatu ilikuwaje?

Profesa Baregu aliyekuwa akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Toleo Na. 293 la Jumatano Mei 1 – 7, 2013 aliyasema maneno hayo akitoa msimamo wake madhubuti wa kukataa katakata kujiuzulu ujumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, agizo alilokuwa amepewa kwa mdomo na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa.

“Ni kweli niliitwa na Katibu (wa Chadema) akaniambia Kamati Kuu ya Chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, hivyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko.

“Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili: Kwanza kijitoe (katika mchakato huo) na pili, kikijitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo”, anasema profesa huyo katika mahojiano yake hayo.

Pamoja na kuagizwa kufanya hivyo, Profesa Baregu anasema alipomuomba Dk. Slaa kuwa ampe barua ya kufanya hivyo, pengine ili naye amwandikie Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kumwainishia sababu halisi au za msingi zilizotolewa na chama chake hakupewa, na pia hakuambiwa endapo angepewa na hadi sasa hajapewa hata maandishi ya kipande cha karatasi tu.

Akiwasilisha hotuba mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni kujibu iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda katika bunge la bajeti ya serikali ya mwaka 2013/2014 mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama chake kinajitoa katika mchakato huo na kuanza kulalamikia mambo yasiyokuwa na maana.

Alisema kuwa Chadema inajitoa akidai mchakato huo mzima umetekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), halafu hata Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba “hawana weledi wa kutosha” ili kuifanya kazi hiyo.

Akizungumzia suala hilo pia wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba, Ijumaa iliyopita, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu naye alisema chama chake hakikubaliani kwa namna zote na mchakato mzima wa Mabadiliko ya Katiba na kutaka ufutwe kabisa na kuanza upya.

Katika kuthibitisha ukweli kwamba haungi mkono hoja hiyo yote, Mbunge huyo ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni alimwondolea shilingi Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kutoka kwenye mshahara wake hadi serikali ikubali kwanza kusitisha zoezi hilo.

Alihoji kwamba inakuwaje kuwe na tofauti ya hatua za kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Kata baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, jambo alilosema kamwe haliwezekani na kudai kwamba hiyo ni miongoni mwa kasoro ambazo haziwezi kabisa kuruhusu kuendelea kwa mchakato huo wote.

Baada ya Tundu Lissu kumaliza kusema, Mbowe naye alisimama na kudai kuwa mchakato huo unavyokwenda una sura ya kisiasa, kauli ambayo sikumwelewa kwa sababu hata yeye anafahamu kwamba suala zima la Katiba ya nchi kamwe haliwezi kuwa la kidini, riadha au la kuchezea disko ukumbini.

Mbali na hao wawili, Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam (Chadema), Halima Mdee naye aliposimama alisema hakubaliani na kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Kata huku akidai kwamba yamejaa wanachama wa CCM.

Aliitaka serikali iusitishe mchakato huo sasa, vinginevyo chama chake kitakwenda nchi nzima “kumwaga sumu” kwa watu ili waukatae, kauli iliyopokelewa kwa kejeli na baadhi ya wabunge kwa kumtaka aharakishe kufanya hivyo kwani hakuna mtu yeyote anayeweza kumtisha chochote.

Hivyo ndivyo wabunge na viongozi wa Chadema walivyogeuka kuupinga mchakato huo wakidai hauna maana yoyote. Wanataka zoezi hilo zima lisitishwe, lakini hawana hoja za mashiko isipokuwa kiwewe hasa baada ya kusambaratishwa agenda na mipango haramu waliyokuwa wakiitaka.

Wanaungana kudai kuwa karibu wajumbe wote waliochaguliwa kuingia kwenye Mabaraza ya Katiba ya Kata ni wanachama na viongozi wa CCM, lakini hawasemi kwa takwimu ila mdomoni peke yake na bila kielelezo chochote.

Wanasema Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba “hawana weledi wa kutosha ili kuifanya kazi hiyo”, kauli ambayo tafsiri yake halisi ni kuwa hawana elimu ya kutosha, hawana upeo wowote, hawana ufahamu au kwamba hawajui lolote wala chochote!

Wanaamini kuwa wajumbe hao ni sawa na watu waliookotwa mitaani na hivyo hawana sifa yoyote hasa ya elimu, hawana uzoefu katika uongozi wa umma na shughuli nyingine za kijamii au katika ujumla wao wote hawana uwezo wowote wa kuweza kuifanya kazi hiyo.

Hivyo ndivyo Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akina Jaji Joseph Warioba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Jaji Augustine Ramadhan aliyewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Mwesiga Baregu au Meja Joseph Butiku aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Rais kwa zaidi ya miaka 20 na wengineo!

Hivyo ndivyo wajumbe hao wote wanavyochukuliwa na watu kama Mbowe ama Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika waliohitimu elimu ya kidato cha sita tu au Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), Sylivester Kasulumbayi anayetiliwa wasiwasi hata kwamba amehitimu vizuri elimu yake ya msingi!

Hivyo ndivyo wanavyochukuliwa na watu kama Tundu Lissu au Halima Mdee ambao sasa wana miezi 30 tu katika uongozi wa umma wakiwa wabunge, lakini ambao bado vitendo vyao hasa bungeni vinafanana na vya watu wa kijiweni tu!

Sijui tafsiri sahihi ya kumwambia Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim ama Jaji Augustine Ramadhani kwamba “hawana weledi wa kutosha” wa kuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Siielewi tafsiri zaidi ya “weledi wa kutosha” katika uongozi wa umma au kuhusu elimu aliyonayo msomi wa aina ya Warioba, Augustine Ramadhani, Dk. Salim Ahmed Salim au Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu alivyo Profesa Mwesiga Baregu!

Sifahamu kabisa endapo kuna maana nyingine ya weledi kwa kuwalinganisha watu hao na wabunge kama Freeman Mbowe, Tundu Lissu au Halima Mdee kwa kuangalia elimu zao na hata uzoefu wa uongozi wa umma walionao!

Pamoja na sababu nyingine ama vinginevyo, hata kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji mpaka mtu ahitimu chuo kikuu chochote duniani ndipo aelewe nini kinaendelea hawezi kabisa kudanganyika kwa namna yoyote na uzushi, uongo, uchochezi na hata upotoshaji unaofanywa na wabunge hao kwa niaba ya chama chao au watu wanaowafadhili kifedha!

Kama alivyonukuliwa Profesa Baregu akiliambia gazeti la Raia Mwema, mchakato mzima wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulianzishwa na viongozi wa Chadema wenyewe, lakini hatimaye inaonyesha kwamba walitaka jambo hilo walitumie ili kukidhi matakwa yao ya kisiasa peke yao!

Lilitokana na kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa kwa upotoshaji mkubwa na viongozi waandamizi wa Chadema kama akina Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Tundu Lissu na kadhalika.

“…Mimi tangu mwanzo kabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba Chadema ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya.

“Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 (kwa Chadema) na nilishiriki kuandika Ilani ya Uchaguzi (ule)…hili (suala) la Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu”, anasema Baregu aliyenukuliwa na gazeti hilo la kila Jumatano ya wiki na kuendelea:

“Wakati ule wenzetu (wa CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na Katiba mpya, (wakasema kuwa) iliyopo inatosha. Lakini baadaye serikali ikaona ipo haja ya kuwa na Katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo.

“Muswada ukapelekwa bungeni (na) wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. Chadema tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais (Jakaya Kikwete) kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yalikubaliwa.

“Muswada ukarudishwa upya bungeni, sheria ikafanyiwa marekebisho na kukubaliwa na wabunge wa kambi ya upinzani (wakiwemo wa Chadema). Sasa leo hii, wabunge walewale waliokubali wanataka kukataa mchakato wa Katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe.

“Kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo nisingekuwemo humu (akimaanisha ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba), ningejitoa. Tunatengeneza Katiba ya Watanzania wote na siyo Katiba ya chama fulani (cha siasa)”.

Akizidi kuainisha, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema aliyekuwa mmoja kati ya wawakilishi wa chama hicho waliokwenda Ikulu kuonana na Rais Kikwete anaendelea:

“Lakini pia, Chadema tulipokutana na Rais alitushauri na tukakubaliana naye (kwamba) twende hatua kwa hatua. Kwanza itungwe sheria yenyewe, halafu iundwe tume. Baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa. Tangu wakati huo hadi sasa nadhani sisi kama Tume (ya Mabadiliko ya Katiba) tunafanya vizuri (zaidi) tukilinganishwa na wenzetu wa huko nje waliowahi kuziandika upya Katiba zao.

“Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba. Hatua hii nayo wananchi wametakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ya muundo wa bunge hilo. Ushauri wangu kwa Chadema (ni kuwa) naomba chama chetu (hiki) kikae mkao wa kujenga nchi yetu na siyo mkao wa (kutaka) kuibomoa.

“Kama chama (tunapaswa) tukae na Watanzania (wenzetu ili) kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania (wote) na Tanzania yetu”, anasema Baregu ambaye ni mmoja kati ya wasomi wanaoheshimika kwa kiwango kikubwa nchini na sehemu nyingine duniani.

Akizungumzia kauli iliyotolewa na Freeman Mbowe katika hotuba yake bungeni aliyedai kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina watu weledi, Profesa Baregu ananukuliwa kwa mara nyingine tena na gazeti hilo akisema:

“Sisemi (kuwa) katika hili Chadema imekurupuka (ila) ijishauri upya. Sijui ni weledi gani wanaousema, lakini naamini Tume ya Mabadiliko ya Katiba imejaa watu weledi watupu. Imejaa watu waadilifu na wasiokuwa na matope yoyote na ndiyo maana tangu ilipoundwa, hakuna Mtanzania yeyote ambaye ameiita kuwa ni genge jingine la mafisadi.

“Sitaki kuwasemea wajumbe wenzangu juu ya weledi wao, lakini (mimi) mwenyewe tu mbali na elimu yangu (ya hadi uprofesa), lakini pia nimetumika katika Tume (ya Kimataifa) ya Mo Ibrahim inayotathmini utawala bora wa marais wa Afrika kwa muhula mmoja. Mtu huwezi kuwa katika Tume hiyo kama huna weledi wa kutosha” (mwisho wa kunukuu).

Ingawa Baregu amejitolea mfano wa yeye peke yake kwamba amekuwa ndani ya Tume ya Mo Ibrahim, Mtanzania mwingine aliyemo katika chombo hicho kinachoheshimika zaidi duniani kote ni Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim.

Nimesema na pia nikahoji kwa namna moja ama nyingine juu ya weledi alionao Mbowe kama Mbunge, Kiongozi wa Upinzani Bungeni au Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, na pili nikahoji elimu na uzoefu wa uongozi wa umma walionao wabunge kama Tundu Lissu au Halima Mdee kumshinda Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim, Jaji Augustine Ramadhani, Profesa Baregu au wajumbe wengine wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Nikauliza tena “weledi wa kutosha” wasiokuwa nao na sasa ninaomba kujua uadilifu gani asiokuwa nao Warioba, Augustine Ramadhani, Salim Ahmed Salim au Baregu unaotiliwa mashaka na Mbowe ambaye ni mchezeshaji wa disko wa zamani ama Dj mstaafu, mmiliki wa klabu ya usiku ya Billicanas & Cassino au Tundu Lissu na Mdee waliokosa adabu hadi bungeni.

Naiangalia elimu ya kidato cha Sita aliyonayo Mbowe na kuilinganisha na ile waliyonayo akina Jaji Joseph Warioba, Jaji Augustine Ramadhani, Dk. Salim Ahmed Salim, Profesa Mwesiga Baregu au Meja Joseph Butiku mbali na wajumbe wengine mbalimbali wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hadi wakadhalilishwe bungeni kwa hotuba iliyosheheneza uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa.

Namwangalia Tundu Lissu alivyomhusisha kwa uzushi hadi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Siasa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kuhusiana na suala zima la mchakato wa Mabaraza ya Katiba ya Kata, madai ambayo hata kama yana ukweli bado hakuvunja Katiba ila anapaswa apongezwe kwa kufanya kazi nzuri kabisa kwa chama chake.

Nampongeza kwa sababu hata Tundu Lissu na viongozi wenzake wa Chadema walifanya kila mbinu na maarifa yao yote; kuhangaika kuwaweka wanachama na viongozi wa chama chao katika vyombo hivyo kwenye kata lakini wakasambatarishwa vibaya.

Waliwafanyia kampeni mchana kutwa na mpaka usiku wa manane ikiwemo kuwatembeza hadi ndani ya makanisa na misikitini ili kwenda kuwaombea ushindi kwa kutumia udini, siasa chafu kabisa ambazo ziliasisiwa na Dk. Slaa alipogombea urais mwaka 2010.

Pamoja na kufanya hivyo kote, malengo ya Chadema yalishindwa baada ya idadi kubwa ya wanachama na viongozi wake waliogombea ujumbe huo wa Mabaraza ya Katiba ya Kata kusambaratishwa kama kishada kilichokwenda harijojo!

Katika hali hiyo ndipo wabunge wa Chadema akina Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Halima Mdee walipokosa adabu hadi bungeni na kuanza kuweweseka huku mmoja wao akitishia eti “watamwaga sumu” kwa wananchi wa nchi hii!

Walikuwa wakiropoka namna hiyo kwa sababu walichanganyikiwa kutokana na kwenda kinyume kwa malengo waliyodhani wangeyapata, yale ambayo kwa hakika yalilenga zaidi kukidhi matakwa yao ya kisiasa.

Walitaka wajaze wanachama na viongozi wa Chadema ndani ya Mabaraza ya Katiba ya Kata ili wakabariki utawala haramu wa majimbo na kuleta ubaguzi wa kikanda.

Walitaka wajaze wanachama na viongozi wa Chadema ili wakatumike kupangua muundo mzima wa viongozi waandamizi wa umma wakiwemo Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Spika wa Bunge, Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na kadhalika.

Baada ya kushindwa kuuteka mchakato huo muhimu wa Katiba, kazi iliyolenga kuwatumia wananchi kuwa mihuri ya kubariki matakwa yao, viongozi wa Chadema waliokuwa mstari wa mbele kudai Katiba mpya ya nchi ndio ambao hivi sasa wanafanya kinyume chake.

Ni wao waliodai kwamba iliyopo haifai na kuanzisha kampeni kubwa ya kuwapotosha wananchi.

Ni wao waliokwenda kila mkoa na kutumia mikutano yao ya kampeni za urais kupotosha watu kuwa Katiba hiyo ya sasa inaifanya CCM iendelee kutawala, jambo ambalo ni uzushi na uongo kwa asilimia 100.

Baada ya serikali kukubali na kuanzisha mchakato wa kuandikwa Katiba nyingine kama walivyokuwa wakiitaka, leo kwa kuona agenda zao zimekwama wameanza kuweweseka hadi bungeni kuipinga.

Tayari wamesahau kuwa wao ndio waliokuwa wakiitaka kwa juhudi na maarifa yao yote, lakini hivi sasa tena wanaipinga kwa nguvu zao zote kwa sababu wanacheza kombolela tu!

Kombolela Baregu....... kombolela mbowe...kombolela slaaa............................
 
Huu ushuzi .. mbona kama wa Le Mutuz ?
 
Slaa alijaribu kutikisa kiberiti Cha Prof akaona kimejaa, sasa ameomba Poo mpaka CC ya kina Mtei iamue kama wajitoe or not bt inaonekana wanazuga baada ya watu kuwapotezea na kuwaona wapuuzi wamejirudi kwa style eti Cc haijaamua, sasa nani aliamua Mzee Baregu arudishe Ndinga na mkwanja? Hawa jamaa wanahitaji vichwa Ngumu kama Zitto, Shibuda na Prof. Ili wawe challenged na kuwa Makini!
 
Kuna wakati ililetwa habari humu kwamba hao wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba inakadiriwa watatengeneza milioni 200 na ushee kila mmoja katika huo mchakato wa hayo mabadiliko.

Sasa kweli tujiulize ni nani anayeweza kuachia fursa kama hiyo kirahisi rahisi tu namna hiyo?
 
Tanzania haiendelei kwa sababu watu wenye akili finyu kama muanzisha mada na hii maiti ya Songoro.

Uchaguzi wa mabaraza ya kata ulifanywa kwa wananchi kupiga kura kuwachagua wawakilishi 8 kwa kila mtaa. Wawakilishi hao ni wa makundi mbali mbali ya kijamii, kama vijana, wazee na wanawake.

Baada ya mtaa kuwapitisha watu wanaowataka, kukazuka UPUMBAVU ULIO WAZI kwamba wenyeviti wa Serikali za mitaa wanajumuika ktk ofisi za kata na kupitisha baadhi ya majina kati ya wale watu waliochaguliwa na wananchi.

Ndugu yangu Marehemu kayogo, nia hasa ya CDM kupigia chapuo uundwaji wa katiba mpya ni kuondoa huu utaratibu mchafu na wa kijinga kabisa wa mtu mmoja kuwachagulia watu 2,800,000 kiongozi (RC, DC n.k) kwani ni upuuzi wananchi kujichagulia mbunge wa jimbo halafu mtu mmoja anamchagua rafiki yake kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye ana madaraka makubwa zaidi ya mbunge aliyechaguliwa na wananchi wengi.

Kama serikali yenu ya CCM ilikuwa na nia njema ya kuunda hii katiba, basi na isingeiambatanisha na hila. Nikichukulia mfano wa kata ninayotoka mimi, ina wakazi takriban 13,960 (kwa hesabu za kipindi kile cha kuandikisha vitambulisho vya Taifa) ambao kati ya hao, kama robo yake tu walifanikiwa kupigia kura wajumbe wa kuingia kwenye baraza la kata, basi watu hao ni wengi zaidi ya WATU 24 waliokaa baadaye na kubadili matakwa ya wananchi kwa jina la taratibu na kanuni. Au wewe kwa akili yako unaamini hawa watu 24 wana akili saaaaana hapa kwenye kata yetu kuliko sisi wote tuliowachagua wale tulioona wanatufaa?

Unapotafuta SIFA ZA KIPUMBAVU hapa jukwaani, basi kumbuka pia Taifa hili linakutegemea ili listawi. Imekuwa sasa ni mazoea ya kipumbavu ya watu kushangilia kila udhalimu kwa kuwa tu umefanywa na CCM. Hata walipoomba 1bn ya kununulia makaburi walipata mashabiki, mbaya zaidi baadhi yetu tu wahanga wa huduma mbaya za afya vijijini kwa kuondokewa na wapendwa wetu kwa kukosa huduma ndogo tu ya dripu.

Mimi nikushauri tu kuwa, hata kama unaona sifa ni muhimu kwako, kumbuka Mungu hapendi dhuluma na ufidhuli. Kama una dini jitazame kabla hujaandika mambo ya kipumbavu
 
Last edited by a moderator:
Nampongeza kwa sababu hata Tundu Lissu na viongozi wenzake wa Chadema walifanya kila mbinu na maarifa yao yote; kuhangaika kuwaweka wanachama na viongozi wa chama chao katika vyombo hivyo kwenye kata lakini wakasambatarishwa vibaya.

Waliwafanyia kampeni mchana kutwa na mpaka usiku wa manane ikiwemo kuwatembeza hadi ndani ya makanisa na misikitini ili kwenda kuwaombea ushindi kwa kutumia udini, siasa chafu kabisa ambazo ziliasisiwa na Dk. Slaa alipogombea urais mwaka 2010.

Pamoja na kufanya hivyo kote, malengo ya Chadema yalishindwa baada ya idadi kubwa ya wanachama na viongozi wake waliogombea ujumbe huo wa Mabaraza ya Katiba ya Kata kusambaratishwa kama kishada kilichokwenda harijojo!

....

Mwandishi anachuki sana,
Ila kwa aliyo yaandika hapo ipo siku tutafika,
Mungusaidia,
Inaonekana hata namna ya kuchagua hawa wajumbe hajuhi huyu jamaaa.
 
“IF I have told to choose between my country and my party I will choose my country”, ndivyo anavyosema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu.

Alikuwa akimaanisha nini? “Kama ningetakiwa nichague (kitu) kimoja kati ya nchi yangu (Tanzania) na chama changu (cha Chadema) ningechagua nchi yangu”.

Naam. Hilo ndilo jibu la uhakika alilosema profesa huyo kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) cha Mwanza, yule ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo Mwenyekiti wake ni Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba.

Nani alikuwa akijibiwa namna hiyo na Profesa Baregu au kwa nini alitoa jibu hilo na tatu ilikuwaje?

Profesa Baregu aliyekuwa akihojiwa na gazeti la Raia Mwema Toleo Na. 293 la Jumatano Mei 1 – 7, 2013 aliyasema maneno hayo akitoa msimamo wake madhubuti wa kukataa katakata kujiuzulu ujumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, agizo alilokuwa amepewa kwa mdomo na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa.

“Ni kweli niliitwa na Katibu (wa Chadema) akaniambia Kamati Kuu ya Chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, hivyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko.

“Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili: Kwanza kijitoe (katika mchakato huo) na pili, kikijitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo”, anasema profesa huyo katika mahojiano yake hayo.

Pamoja na kuagizwa kufanya hivyo, Profesa Baregu anasema alipomuomba Dk. Slaa kuwa ampe barua ya kufanya hivyo, pengine ili naye amwandikie Mwenyekiti wa Tume hiyo kwa kumwainishia sababu halisi au za msingi zilizotolewa na chama chake hakupewa, na pia hakuambiwa endapo angepewa na hadi sasa hajapewa hata maandishi ya kipande cha karatasi tu.

Akiwasilisha hotuba mbadala ya Kambi ya Upinzani Bungeni kujibu iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda katika bunge la bajeti ya serikali ya mwaka 2013/2014 mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alisema chama chake kinajitoa katika mchakato huo na kuanza kulalamikia mambo yasiyokuwa na maana.

Alisema kuwa Chadema inajitoa akidai mchakato huo mzima umetekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), halafu hata Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba “hawana weledi wa kutosha” ili kuifanya kazi hiyo.

Akizungumzia suala hilo pia wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba, Ijumaa iliyopita, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu naye alisema chama chake hakikubaliani kwa namna zote na mchakato mzima wa Mabadiliko ya Katiba na kutaka ufutwe kabisa na kuanza upya.

Katika kuthibitisha ukweli kwamba haungi mkono hoja hiyo yote, Mbunge huyo ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni alimwondolea shilingi Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kutoka kwenye mshahara wake hadi serikali ikubali kwanza kusitisha zoezi hilo.

Alihoji kwamba inakuwaje kuwe na tofauti ya hatua za kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Kata baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, jambo alilosema kamwe haliwezekani na kudai kwamba hiyo ni miongoni mwa kasoro ambazo haziwezi kabisa kuruhusu kuendelea kwa mchakato huo wote.

Baada ya Tundu Lissu kumaliza kusema, Mbowe naye alisimama na kudai kuwa mchakato huo unavyokwenda una sura ya kisiasa, kauli ambayo sikumwelewa kwa sababu hata yeye anafahamu kwamba suala zima la Katiba ya nchi kamwe haliwezi kuwa la kidini, riadha au la kuchezea disko ukumbini.

Mbali na hao wawili, Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam (Chadema), Halima Mdee naye aliposimama alisema hakubaliani na kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Kata huku akidai kwamba yamejaa wanachama wa CCM.

Aliitaka serikali iusitishe mchakato huo sasa, vinginevyo chama chake kitakwenda nchi nzima “kumwaga sumu” kwa watu ili waukatae, kauli iliyopokelewa kwa kejeli na baadhi ya wabunge kwa kumtaka aharakishe kufanya hivyo kwani hakuna mtu yeyote anayeweza kumtisha chochote.

Hivyo ndivyo wabunge na viongozi wa Chadema walivyogeuka kuupinga mchakato huo wakidai hauna maana yoyote. Wanataka zoezi hilo zima lisitishwe, lakini hawana hoja za mashiko isipokuwa kiwewe hasa baada ya kusambaratishwa agenda na mipango haramu waliyokuwa wakiitaka.

Wanaungana kudai kuwa karibu wajumbe wote waliochaguliwa kuingia kwenye Mabaraza ya Katiba ya Kata ni wanachama na viongozi wa CCM, lakini hawasemi kwa takwimu ila mdomoni peke yake na bila kielelezo chochote.

Wanasema Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba “hawana weledi wa kutosha ili kuifanya kazi hiyo”, kauli ambayo tafsiri yake halisi ni kuwa hawana elimu ya kutosha, hawana upeo wowote, hawana ufahamu au kwamba hawajui lolote wala chochote!

Wanaamini kuwa wajumbe hao ni sawa na watu waliookotwa mitaani na hivyo hawana sifa yoyote hasa ya elimu, hawana uzoefu katika uongozi wa umma na shughuli nyingine za kijamii au katika ujumla wao wote hawana uwezo wowote wa kuweza kuifanya kazi hiyo.

Hivyo ndivyo Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba akina Jaji Joseph Warioba aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Jaji Augustine Ramadhan aliyewahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Mwesiga Baregu au Meja Joseph Butiku aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Rais kwa zaidi ya miaka 20 na wengineo!

Hivyo ndivyo wajumbe hao wote wanavyochukuliwa na watu kama Mbowe ama Mbunge wa Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika waliohitimu elimu ya kidato cha sita tu au Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), Sylivester Kasulumbayi anayetiliwa wasiwasi hata kwamba amehitimu vizuri elimu yake ya msingi!

Hivyo ndivyo wanavyochukuliwa na watu kama Tundu Lissu au Halima Mdee ambao sasa wana miezi 30 tu katika uongozi wa umma wakiwa wabunge, lakini ambao bado vitendo vyao hasa bungeni vinafanana na vya watu wa kijiweni tu!

Sijui tafsiri sahihi ya kumwambia Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim ama Jaji Augustine Ramadhani kwamba “hawana weledi wa kutosha” wa kuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Siielewi tafsiri zaidi ya “weledi wa kutosha” katika uongozi wa umma au kuhusu elimu aliyonayo msomi wa aina ya Warioba, Augustine Ramadhani, Dk. Salim Ahmed Salim au Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu alivyo Profesa Mwesiga Baregu!

Sifahamu kabisa endapo kuna maana nyingine ya weledi kwa kuwalinganisha watu hao na wabunge kama Freeman Mbowe, Tundu Lissu au Halima Mdee kwa kuangalia elimu zao na hata uzoefu wa uongozi wa umma walionao!

Pamoja na sababu nyingine ama vinginevyo, hata kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji mpaka mtu ahitimu chuo kikuu chochote duniani ndipo aelewe nini kinaendelea hawezi kabisa kudanganyika kwa namna yoyote na uzushi, uongo, uchochezi na hata upotoshaji unaofanywa na wabunge hao kwa niaba ya chama chao au watu wanaowafadhili kifedha!

Kama alivyonukuliwa Profesa Baregu akiliambia gazeti la Raia Mwema, mchakato mzima wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulianzishwa na viongozi wa Chadema wenyewe, lakini hatimaye inaonyesha kwamba walitaka jambo hilo walitumie ili kukidhi matakwa yao ya kisiasa peke yao!

Lilitokana na kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa kwa upotoshaji mkubwa na viongozi waandamizi wa Chadema kama akina Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Tundu Lissu na kadhalika.

“…Mimi tangu mwanzo kabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba Chadema ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya.

“Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 (kwa Chadema) na nilishiriki kuandika Ilani ya Uchaguzi (ule)…hili (suala) la Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu”, anasema Baregu aliyenukuliwa na gazeti hilo la kila Jumatano ya wiki na kuendelea:

“Wakati ule wenzetu (wa CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na Katiba mpya, (wakasema kuwa) iliyopo inatosha. Lakini baadaye serikali ikaona ipo haja ya kuwa na Katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo.

“Muswada ukapelekwa bungeni (na) wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. Chadema tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais (Jakaya Kikwete) kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yalikubaliwa.

“Muswada ukarudishwa upya bungeni, sheria ikafanyiwa marekebisho na kukubaliwa na wabunge wa kambi ya upinzani (wakiwemo wa Chadema). Sasa leo hii, wabunge walewale waliokubali wanataka kukataa mchakato wa Katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe.

“Kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo nisingekuwemo humu (akimaanisha ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba), ningejitoa. Tunatengeneza Katiba ya Watanzania wote na siyo Katiba ya chama fulani (cha siasa)”.

Akizidi kuainisha, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema aliyekuwa mmoja kati ya wawakilishi wa chama hicho waliokwenda Ikulu kuonana na Rais Kikwete anaendelea:

“Lakini pia, Chadema tulipokutana na Rais alitushauri na tukakubaliana naye (kwamba) twende hatua kwa hatua. Kwanza itungwe sheria yenyewe, halafu iundwe tume. Baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa. Tangu wakati huo hadi sasa nadhani sisi kama Tume (ya Mabadiliko ya Katiba) tunafanya vizuri (zaidi) tukilinganishwa na wenzetu wa huko nje waliowahi kuziandika upya Katiba zao.

“Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba. Hatua hii nayo wananchi wametakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ya muundo wa bunge hilo. Ushauri wangu kwa Chadema (ni kuwa) naomba chama chetu (hiki) kikae mkao wa kujenga nchi yetu na siyo mkao wa (kutaka) kuibomoa.

“Kama chama (tunapaswa) tukae na Watanzania (wenzetu ili) kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania (wote) na Tanzania yetu”, anasema Baregu ambaye ni mmoja kati ya wasomi wanaoheshimika kwa kiwango kikubwa nchini na sehemu nyingine duniani.

Akizungumzia kauli iliyotolewa na Freeman Mbowe katika hotuba yake bungeni aliyedai kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina watu weledi, Profesa Baregu ananukuliwa kwa mara nyingine tena na gazeti hilo akisema:

“Sisemi (kuwa) katika hili Chadema imekurupuka (ila) ijishauri upya. Sijui ni weledi gani wanaousema, lakini naamini Tume ya Mabadiliko ya Katiba imejaa watu weledi watupu. Imejaa watu waadilifu na wasiokuwa na matope yoyote na ndiyo maana tangu ilipoundwa, hakuna Mtanzania yeyote ambaye ameiita kuwa ni genge jingine la mafisadi.

“Sitaki kuwasemea wajumbe wenzangu juu ya weledi wao, lakini (mimi) mwenyewe tu mbali na elimu yangu (ya hadi uprofesa), lakini pia nimetumika katika Tume (ya Kimataifa) ya Mo Ibrahim inayotathmini utawala bora wa marais wa Afrika kwa muhula mmoja. Mtu huwezi kuwa katika Tume hiyo kama huna weledi wa kutosha” (mwisho wa kunukuu).

Ingawa Baregu amejitolea mfano wa yeye peke yake kwamba amekuwa ndani ya Tume ya Mo Ibrahim, Mtanzania mwingine aliyemo katika chombo hicho kinachoheshimika zaidi duniani kote ni Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim.

Nimesema na pia nikahoji kwa namna moja ama nyingine juu ya weledi alionao Mbowe kama Mbunge, Kiongozi wa Upinzani Bungeni au Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, na pili nikahoji elimu na uzoefu wa uongozi wa umma walionao wabunge kama Tundu Lissu au Halima Mdee kumshinda Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim, Jaji Augustine Ramadhani, Profesa Baregu au wajumbe wengine wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Nikauliza tena “weledi wa kutosha” wasiokuwa nao na sasa ninaomba kujua uadilifu gani asiokuwa nao Warioba, Augustine Ramadhani, Salim Ahmed Salim au Baregu unaotiliwa mashaka na Mbowe ambaye ni mchezeshaji wa disko wa zamani ama Dj mstaafu, mmiliki wa klabu ya usiku ya Billicanas & Cassino au Tundu Lissu na Mdee waliokosa adabu hadi bungeni.

Naiangalia elimu ya kidato cha Sita aliyonayo Mbowe na kuilinganisha na ile waliyonayo akina Jaji Joseph Warioba, Jaji Augustine Ramadhani, Dk. Salim Ahmed Salim, Profesa Mwesiga Baregu au Meja Joseph Butiku mbali na wajumbe wengine mbalimbali wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hadi wakadhalilishwe bungeni kwa hotuba iliyosheheneza uzushi, uongo na upotoshaji mkubwa.

Namwangalia Tundu Lissu alivyomhusisha kwa uzushi hadi Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Siasa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro kuhusiana na suala zima la mchakato wa Mabaraza ya Katiba ya Kata, madai ambayo hata kama yana ukweli bado hakuvunja Katiba ila anapaswa apongezwe kwa kufanya kazi nzuri kabisa kwa chama chake.

Nampongeza kwa sababu hata Tundu Lissu na viongozi wenzake wa Chadema walifanya kila mbinu na maarifa yao yote; kuhangaika kuwaweka wanachama na viongozi wa chama chao katika vyombo hivyo kwenye kata lakini wakasambatarishwa vibaya.

Waliwafanyia kampeni mchana kutwa na mpaka usiku wa manane ikiwemo kuwatembeza hadi ndani ya makanisa na misikitini ili kwenda kuwaombea ushindi kwa kutumia udini, siasa chafu kabisa ambazo ziliasisiwa na Dk. Slaa alipogombea urais mwaka 2010.

Pamoja na kufanya hivyo kote, malengo ya Chadema yalishindwa baada ya idadi kubwa ya wanachama na viongozi wake waliogombea ujumbe huo wa Mabaraza ya Katiba ya Kata kusambaratishwa kama kishada kilichokwenda harijojo!

Katika hali hiyo ndipo wabunge wa Chadema akina Freeman Mbowe, Tundu Lissu na Halima Mdee walipokosa adabu hadi bungeni na kuanza kuweweseka huku mmoja wao akitishia eti “watamwaga sumu” kwa wananchi wa nchi hii!

Walikuwa wakiropoka namna hiyo kwa sababu walichanganyikiwa kutokana na kwenda kinyume kwa malengo waliyodhani wangeyapata, yale ambayo kwa hakika yalilenga zaidi kukidhi matakwa yao ya kisiasa.

Walitaka wajaze wanachama na viongozi wa Chadema ndani ya Mabaraza ya Katiba ya Kata ili wakabariki utawala haramu wa majimbo na kuleta ubaguzi wa kikanda.

Walitaka wajaze wanachama na viongozi wa Chadema ili wakatumike kupangua muundo mzima wa viongozi waandamizi wa umma wakiwemo Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Spika wa Bunge, Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na kadhalika.

Baada ya kushindwa kuuteka mchakato huo muhimu wa Katiba, kazi iliyolenga kuwatumia wananchi kuwa mihuri ya kubariki matakwa yao, viongozi wa Chadema waliokuwa mstari wa mbele kudai Katiba mpya ya nchi ndio ambao hivi sasa wanafanya kinyume chake.

Ni wao waliodai kwamba iliyopo haifai na kuanzisha kampeni kubwa ya kuwapotosha wananchi.

Ni wao waliokwenda kila mkoa na kutumia mikutano yao ya kampeni za urais kupotosha watu kuwa Katiba hiyo ya sasa inaifanya CCM iendelee kutawala, jambo ambalo ni uzushi na uongo kwa asilimia 100.

Baada ya serikali kukubali na kuanzisha mchakato wa kuandikwa Katiba nyingine kama walivyokuwa wakiitaka, leo kwa kuona agenda zao zimekwama wameanza kuweweseka hadi bungeni kuipinga.

Tayari wamesahau kuwa wao ndio waliokuwa wakiitaka kwa juhudi na maarifa yao yote, lakini hivi sasa tena wanaipinga kwa nguvu zao zote kwa sababu wanacheza kombolela tu!

Kombolela Baregu....... kombolela mbowe...kombolela slaaa............................

Je umefanya tafiti za uhakika za haya uyasemayo? Una uhakika kuwa ndicho kinachoendelea? Je unajua kiuhalisia kinachoendelea kule mitaani kuhusu michakato ya kupata mabaraza ya katiba? Je, ni kweli kwamba hapo ulipo unaona maisha ya kuridhisha kwako binafsi, kwa mtoto wako na hata wajukuu wako kwa miaka ya baadae baada ya wewe kutoweka hapa duniani? Je uliwahi kukaa na kutafakari uwiano wa rasilimali za nchi hii na hali ya kiuchumi tuliyonayo? je uliwahi kujiuliza kwa nini Tanzania inasuasua sana kukua kiuchumi licha ya kuwa na rasilimali lukuki? Au ni kweli kwamba umeridhika na hali halisi? Unaweza kataa haya yote na kupuuzia lakini naamini moyo wako hauwezi kukudanganya na kukusaliti hata siku moja. Hebu fanya tafakari na tafiti za kina kabla hujaleta mada huku jamvini; ni muhimi sana kwa ustawi wa taifa letu na kizazi cha leo na hata baadae. Katiba si kitu cha kufanyia mchezo mchezo wa aina yoyote kwani ndiyo uhai wa taifa lolote lile, ni lazima iangaliwe si kwa macho ya kawaida ya nyama tu bali hata macho ya rohoni, kwani uhai wa katiba ndio uhai na ustawi wa taifa lolote lile; tafakari ndugu, weka ushabiki wa chama pembeni katika hili na simamia utaifa zaidi.
 
Slaa alijaribu kutikisa kiberiti Cha Prof akaona kimejaa, sasa ameomba Poo mpaka CC ya kina Mtei iamue kama wajitoe or not bt inaonekana wanazuga baada ya watu kuwapotezea na kuwaona wapuuzi wamejirudi kwa style eti Cc haijaamua, sasa nani aliamua Mzee Baregu arudishe Ndinga na mkwanja? Hawa jamaa wanahitaji vichwa Ngumu kama Zitto, Shibuda na Prof. Ili wawe challenged na kuwa Makini!

Kiongozi!

Suala sio kichwa ngumu. Muhimu ni kuwa na POITS. Unacho kiona kwa Prof Baregu ni kama udhaifu mwingine tunao uona kwa wasomi wetu wengi Tanzania. Kwamba wanaamua kuweka ufahamu na weledi wao mifukoni na kuwasaliti waTanzania ili kulinda ulaji wao.

Hivi hata sisi huku vijijini, ni nani asiye ona kwamba mchakato wa kuandika katiba mpya umetekwa na CCM? Kama Ma-DC na Ma-RC ni wajumbe na makada wa CCM na wakati huo huo wamejiingiza kwenye zoezi zima la mchakato wa kuandika Katiba mpya, unategemea kupata matokeo ya namna gani kama si kile wanacho kitaka CCM?

"UKISHAONA ADUI YAKO AMEKUSIFIA FAHAMU UMESHAVURUNDA". Vivyo hivyo na kwa Prof Baregu kusifiwa na CCM, ajue historia ya mabadiliko ya nchi hii ita muhukumu.
 
umejitahidi kujifanya huwezi kutumia akili yako kuuona umhimu wa baregu na busara zake ukaegemea kundi la wahuni kwa maslahi unayoyaajua wewe.
 
Lumumba 1 -upeo wao wa kufikiria huwa haujifichi!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
umejitahidi kujifanya huwezi kutumia akili yako kuuona umhimu wa baregu na busara zake ukaegemea kundi la wahuni kwa maslahi unayoyaajua wewe.

Kiongozi!

Mimi ni mwana kijiji tu. Bahati nzuri maslahi yangu ni kuiona na kupata Tanzania yenye kuheshimu na kujali maslahi ya waTanzania wote bila kujali vyeo, jinsia, familia, kabila, kanda, na mambo yanayo fanana na hayo. Sijui kama wanao toa picha halisi ya kinacho endelea kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya ni wahuni wachache.

Kila aliye weka akili yake katika mchakato huu anajua nini kinacho endelea na hasa mapungufu yanayo endelea kujitokeza. Hivi unataka kuniambia kwamba idadi ya walio changia kutoa maoni ya katiba mpya ni kielelezo sahihi cha kuwakilisha idadi ya waTanzania zaidi ya Milioni 45? Ni ukweli usio pingika kwamba hatuwezi kutoa maoni wote, lakini angalau kuwepo na uwiano ambao ungeleta picha ya uwakilishi unao pimika ki sayansi!

Hivi unataka kutuambia kwamba hujui ni jinsi gani Ma-Dc na Ma-RC walivyo ingilia mchakato mzima wa kuandika Katiba Mpya? Unataka kusema kwamba hujui jinsi walivyo ingilia baadhi ya mikutano ya kutoa maoni kwa kuwa wasemaji wakuu kwenye baadi ya maeneo na kuwafanya wananchi wengi kuhofia hata kushiriki kwenye mikutano?

Kwamba hujui WDC zimetawaliwa na Uchama zaidi huku watendaji karibu wote wakiitikia maagizo kutoka kwa wakuu wa wilaya?

Yapo mambo mengi tu ambayo yanaonyesha wazi kwamba katiba inayo andikwa si ya waTanzania bali ya watawala na hivyo kuuweka mustakabali wa taifa katika kiza kinene badala ya kuliandalia Taifa hili mwanga wa Maendeleo ambayo yamekuwa ni bidhaa adimu.

Hapa suala si umuhimu au busara za Prof Baregu. Suala muhimu ni kuungalia mustakabali wa Taifa la waTanzania. Prof. Baregu naye ni binadhamu kama wengine. Pamoja na hizo busara unazo sema anazo na umuhimu wake (kama upo), anaweza kupata kichocheo ambacho kika mfanya asione/ asijali hatari itakayo likabili taifa hili pale tutakapo pata Katiba ambayo si ya waTanzania bali ya wanao ongoza waTanzania.

Tusubiri tuoni kwani HISTORIA NI MWALIMU MZURI.
 
"IF I have told to choose between my country and my party I will choose my country", ndivyo anavyosema Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Baregu.

Alikuwa akimaanisha nini? "Kama ningetakiwa nichague (kitu) kimoja kati ya nchi yangu (Tanzania) na chama changu (cha Chadema) ningechagua nchi yangu".

Wacha urongo...
Baregu hawezi kuongea kiingereza kibovu namna hii... Bora hata usingemquote...
 
Back
Top Bottom