Vita ya Daktari na Mchungaji nani mkosaji?

Vita ya Daktari na Mchungaji nani mkosaji?

MUWHWELA

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
176
Reaction score
259
Upewe Neema ya UHAI kwa upya!

Salama

Nimejikuta nawaza kwa udogo Lakini nikaona Iko haja ya kuwa na mjadala mdogo tu na ndugu ZANGU wa jukwaa hili ambao kimsingi wanajadili jambo kwa utashi mkubwa.

MCHUNGAJI anachunga kondoo/waamini/waumini, ambao wanaaminishwa kwamba maombi ndiyo msingi wa mafanikio yote, yaani usipoomba Mungu vitu haviwezi kutokea wanaamini hivyo. Ni sawa na pia haki Yao.

Hawa Hawa waamini wakipata shida ya kiafya wanaenda kwanza kwa MCHUNGAJI awaaombee ,watoe na sadaka, lakini mwisho wake MCHUNGAJI mwenye hekima anasema kwa ugonjwa huu nendeni mukamwone DAKTARI.

Daktari,yeye udaktari hajaupata kwa Maombi Bali kwa kufuata kanuni za Dunia, kwa kukesha akisoma na kufanya research at the end amekuwa Dr mwenye MSAADA mkubwa kwa jamii, je huyu naye angekesha na Maombi angekuwa daktari? Jibu ni hapana.

Haya! Mgonjwa amefanyiwa upasuaji na Dr ambaye ni mlevi wa pombe na sigara, Lakini mgonjwa akipona anapeleka sadaka na shukrani kwa MCHUNGAJI. What is this? Thamani ya huyu Dr Iko wapi? Are we serious on it? Okay okay tufanye hivi.

Kama Mungu alimpa uwezo Dr akafanya upasuaji salama na ukapona? Why usimtukuze Mungu wa huyu Dr? Akili tumepewa Bure na Kazi yake inahitaji kuonwa Ili maisha yetu yawe na thamani as true God planned.

(Brainwashed) Ukweli ni kwamba Hawa walioleta hizi Dini wao wenyewe hawafuati hiyo mifumo, wanafuata mifumo inayoleta matokeo kisayansi, na kwa hakika ukifuata mifumo ya Asili, nobody can fool you pia Dunia patakuwa mahala salama kwa mwanadamu.

Kazi afanye Dr fedha za shukrani na sadaka apewe mchungaji, MCHUNGAJI alimwombea Dr mlevi amatibu muumini wake au alimkumbusha Mungu? Which is hakuna MTU anaweza kumsaidia Mungu kazi zake (Play your levels)

IPE TU KAZI AKILI
"Hakuna mfano nyuma ya mfano nyuma ya mfano Kuna Imani"
 
Back
Top Bottom