Waliorejea mabondeni wapewa siku 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliorejea mabondeni wapewa siku 14

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki


  Serikali imetoa siku 14 kwa wakazi waliorudi katika maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam baada ya kukimbia makazi yao kutokana na mafuriko yaliyotokea mwezi uliopita kubomoa nyumba zao na kuondoka kabla “tingatinga” halijatua huko na kuwavunjia.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, alisema baada ya ugawaji wa viwanja kwa waathirika hao na kuhakikisha kila mmoja amepata serikali itavunja nyumba zote zilizopo mabondeni.

  Alisema siku 14 zitakazotolewa na serikali ni kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi hao kubomoa wenyewe kwa hiari na kubeba milango, mabati, matofali na vifaa vingine wanavyoona vinafaa ili waondoke navyo.

  Aliyasema jana baada ya kupokea msaada wa mabati 500 yenye thamani ya Sh. milioni 11 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

  Hata hivyo, alisema baada ya muda huo kumalizika hawatakuwa na utani na mtu yoyote zaidi ya kuingiza tingatinga na kusawazisha eneo lote.

  Alisema jana kamati ya maafa ilikuwa na kikao maalum kwa ajili ya kupanga siku ya kuwahamisha waathirika hao kwenda Mabwepande na kwamba watakaokaidi kuhama watapewa siku 14 kukaa mabondeni.

  “Hapa hatuna mzaha wala mchezo wa kuigiza katika kuwahamisha wananchi hao wa mabondeni, ni lazima waondoke baada ya kupewa viwanja na kuhamishiwa Mabwepande,” alisema.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...