Waliooa waliowazidi kipato hawana ufanisi

Waliooa waliowazidi kipato hawana ufanisi

CPU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
3,858
Reaction score
688
Hii imefanyiwa utafiti huko nchi za wenzetu lakin naona inatugusa hata sisi.
Inasemekana kwamba wanaume waliooa wanawake wenye mishahara mikubwa au vyeo kuwazidi wao, huathirika kisaikolojia wakati wa tendo la ndoa na wengi wao hutoka nje ya ndoa. Utafiti umebaini.



Utafiti huo uliofanywa katika nchi za Denmark na Marekani umebaini kuwa wanaume wanaopata mshahara mdogo, hawashiriki tendo la ndoa kwa ufanisi na wake zao walio na mishahara mikubwa, ukilinganisha na wanaume walio na kipato kikubwa kuwazidi wake zao.



Msaidizi katika utafiti huo Dk Lamar Pierce ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Mipango katika Chuo Kikuu cha Washington alisema kuwa wanaume huwa dhaifu kiutendaji katika tendo la ndoa, inapotokea mwanamke ana cheo au kipato kikubwa kuliko yeye. Hata hivyo, utafiti huo haukuwahusisha wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa.

Mtafiti huyo alisema kuwa hali hiyo ni mbaya zaidi katika nchi za Afrika, ambapo m mfumo dume umetawala huku mapinduzi ya kijinsia yakianza kushika kasi.

Nime-copy sehemu ya habari iliyoandikwa na Gazeti la Mwananchi.
Je, kuna mtu ameshawahi ku-date na mwanamke wa aina hii na yakamtokea haya mambo??
Je, wanawake, ni kweli mnakuwa hamtoshelezwi na wanaume wa aina hii??
 
Sio kweli,mumewangu wakati kanioa mimi nilikua na mshahara mara3 ya mumewangu na haikumuathiri mpaka sasa amemaliza kusoma anapokea zaidi yangu,na hakukua na tofauti zozote raha mwanzo mwishoo..heshima Kama kawaida..
 
Tatizo litakuwepo kama kutakuwa na kauli za unyanyasaji wa kisaikolojia, kama vile "Umemaliza mafuta kwenye gari yangu"
hahahaha daaah...kweli hii noma...
 
Tatizo litakuwepo kama kutakuwa na kauli za unyanyasaji wa kisaikolojia, kama vile "Umemaliza mafuta kwenye gari yangu"

kila siku nikikuambia naenda kusalimia Moshi wewe utaki sasa itakuwaje tena baba iseee , kwani nauli unanipa wewe?
 
Back
Top Bottom