Mwisho alikuwa ni mchezaji wa yanga hatimae Pan African ya Dar. Alitokea Tumbaku ya Morogoro akiwa pamoja na akina Shillingi na Hussein Ngulungu.
Nilikuwa ninamsikia redioni Enzi hizo wakati mpira ulikuwa unatangazwa kwenye redio za mbao,kuja kumwona uwanjani ilikuwa ni kati ya Enugu rangers ya Nigeria na Yanga mwaka 1975 uwanja wa Taifa sasa hivi uwanja wa uhuru.
Alicheza dakika zote tisini akiwa pamoja na Mzee Jella Mtagwa, Mzee Tenga na Mzee Sunday Manara na kaka yake Kitwana Manara.
Juma Matokeo (mid-field mayestro) kama walivyokuwa wanapenda kumwita alikuwa na kiwango cha juu kabisa cha uchezaji yaani control ball kwa sasa hivi namfananisha na Luka Modric wa Really Madrid japokuwa Juma Matokeo kamzidi kidogo Luka Modric kwa speed na ball control.
Alikuwa ni moto wa kuotea mbali ukiingia uwanjani na ukimkuta anacheza hakika hujutii hela yako ya kiingilio,alikuwa anafanya dakika 90 zinakuwa ni chache sana kiasi kama unavuta sigara waweza kuta inakuunguza vidoleni maana unakuwa umesahau kabisa kama unavuta huku ukiangalia mpira kwa ajili ya mavituzi ya Juma Matokeo.
Mimi Juma Matokeo nimemwona anacheza na wachezaji wa sasa wa ndani na wa nje wanaocheza namba yake namba 8 nimewaona, mpaka sasa sijaona kama Juma Matokeo, kwanza mpira wa inchini niliacha kuangalia miaka kadhaa iliyopita maana siyo kiwango changu, timu zina madaraja na watazamaji nao wana madaraja mpira unaochezwa inchini kwa sasa siyo daraja langu kabisa.
Hata marafiki zangu akina Advocate (wakili ) John Kumwembe na Sengwaji wakifufuka sasa hivi uwapeleke uwanjani kuwe na mpira hususani uwanja wa mashujaa Mtwara haki ya mungu hawawezi kuangalia.
Basi Mpira mwaka 1975 Uwanja wa taifa kati ya Enugu Rangers na Yanga uliisha 1-1 Yanga wakitolewa kwa bao la ugenini. Nilichojifunza ni kwamba mkifungwa kumbe njaa haiumi, ni kwenda stesheni kupanda treni na kurudi Dodoma Mazengo secondary maana safari yenyewe niliondoka na shs 10 ya kiingilio uwanja wa Taifa, nauli mpaka Dar mungu anajua na chakula mungu anajua kama nilivyoisha kuwaambia matokeo yakiwa mabaya wala njaa haiumi.
Mnaosema eti Mbwana Samatta ni mchezaji sijui mngemwona Juma Matokeyo sijui mngesemaje.