Waliomuibia mke wa Dk Slaa Mbaroni

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
54,299
Reaction score
43,501
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia watu wanane wakiwemo waliomvamia mwanamke wa DK Slaa, Josephine.
Josephine alivamiwa na majambazi hao na kumpora vitu mbalimbali jula 13, mwaka huu saa 11.00 jioni eneo la Mwenge jirani na Suma JKT, akiwa na gari aina ya Harrier.
Katika tukio hilo majambazi hao walifyatua risasi kabla ya kuvunja kioo cha gari hilo kwa nyundo, kisha kummwibia mkoba ulikuwa na vitu mbalimbali. kamanda Kova, alisema kufuatia tukio hilo, wamekamata majambazi watano ambao walihusika na uvamizi.
Pia, polisi imeahidi kutoa Sh3 milioni kwa mtu atayefanikisha kukamatwa kwa majambazi
source:Mwananchi julai 30. 2011
 
Pongezi kwa Jeshi la Polisi kufanya kazi yao kwa umakini
 
watu hao ambao walijulikana kwa majina ya ahmed suleiman,idrissa rashid,bakari idi na mwingine jina lake halikuweza kupatikana mara moja..
 
Qoute: "Polisi imeahidi kutoa Sh3 milioni kwa mtu atayefanikisha kukamatwa kwa majambazi....!?
Duh! Nahisi itakua kulikua na documents za muhimu kwenye ule mkoba wa First Lady Slaa!
 
Sio mwanamke aliezaa na DK Slaa bali ni mke wake,ukisema hivyo anaoneka kama kimada,wakati ni wife na alimtangaza rasmi kwenye kampeni za urais pale jangwani......yaani alikuwa awe first lady wa TZ
 
Hongera Polisi kwa kazi nzuri muendelee kuwalinda raia wote bila ubaguzi.
 
jeshi la polisi tz siliamini kabisa.....ujanja mwingi umewazidi.
 
Sio mwanamke aliezaa na DK Slaa bali ni mke wake,ukisema hivyo anaoneka kama kimada,wakati ni wife na alimtangaza rasmi kwenye kampeni za urais pale jangwani......yaani alikuwa awe first lady wa TZ
huyo dada atakuwa na waume wawili basi. Alimtangaza kama demu wake sio mke wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…