Mwamaleki
JF-Expert Member
- May 25, 2018
- 696
- 2,956
DaahKiranga,
Umesema kweli kabisa makosa mengi hufanyika na ni vizuri kusikia na mwengine analijua vipi.
Miaka mingi ikipita kumbukumbu hupotea kirahisi sana.
Umenikumbusha mbali sana kaka.
Collection yangu ya ngoma hizo ilikuwa kali sana.
Siku nilipofika Apollo Theatre New York nikakumbuka wakati nina miaka 16 hivi nakua Dar es Salaam mimi na wenzangu tukiziimba nyimbo za Tamla Motown.
Nilisimama kwa muda Broadway nikakumbuka mwimbo wa Wilson Pickett ''Funky Broadway,'' na ikasadifu kuwa barabara nikiipita Manhattan katika shughuli zangu.
Wengi wa hawa ''stars'' walianza ''carrier'' zao hapo Apollo Theatre na tukikuona mbali sana...
Kaka Kiranga Temptations wakaja Paris kufungua Disneyland mimi niko upande wa pili wa English Channel katika kimji kidogo Wales wako mubashara...wazimu kaka sasa tumekuwa watu wazima miaka imekwenda wapi?
Nadhani Temptations aliye hai ni mmoja tu.
Mzee wewe ni legend sana.
Salute