waliomo kwenye Tume ya Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waliomo kwenye Tume ya Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by friendsofjeykey, Jan 2, 2011.

 1. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mnawajua waliopo kwenye hili jopo ni akina nani?

  haya ndio matatizo ya kutokuwa na open Government
  website ya Wizara ya Sheria haisemi kitu (infact iko down)
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mod hizipo post ziunganisheni zinaboa sasa.
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Watachaguliwa kutokana na ushauri utakaopendekezwa na Lowassa na Rostam! Mark my words... na niko serious!
   
 4. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBONA KWENYE MAGAZETI YA LEO WAMESEMA rAIS KESHAUNDA TUME?
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu unatoka ndani ya system nini?
  Ntajuaje aliyechaguliwa katokana na uliowataja?
   
 6. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Labda tuanze kupredict tu. Vinginevyo, majina bado.
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wanaoendesha nchi ni ra na el kwa hiyo lazima washirikishwe
   
 8. a

  awtu Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....and thier pwan you might add!
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mkuu... hata hili suala la katiba mpya mratibu wa mambo yooooooote ni Lowassa. Lowassa aliongea na Kikwete akamwambia njia nzuri ya kushughulikia hili "tatizo" la katiba mpya ni kujihami. Wawahi mapema kushika usukani kwani wakichelewa na wananchi wakiongozwa na wapinzani wakiushika hawatakuwa tena na "control" ya chombo.
  Na hii tume.. wewe fuatilia.. mambo yoooote yatapelekwa kimpangilio na kiakili.... ili yaifaidishe CCM (soma mafisadi). Na zimetengwa fedha nyingi sana kwa ajili ya ku-influence wajanja wachache watakaopiga kelele mchakato utakapoenda ndivyo sivyo... Tusibiri tuone kwani hizi info nimepewa na mtu "wa ndani" kabisa.
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  By the way si ulisikia siku Lowassa alipoongea kanisani na kusema anamshukuru Mungu kwa kumvusha vikwazo vigumu. Halafu akaenda mbali zaidi na kusema sasa ni wakati muafaka wa kuangalia katiba yetu? Sasa wewe inakujia akilini kweli Lowassa atake kujinyonga mwenyewe.... kwa kudai katiba nzuri? Kwa sababu kama leo itaandikwa katiba inayofaa, na ndoto zake za 2015 zitayeyuka moja kwa moja!
   
 11. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  JK alisema ataunda kama nilimsikia vizuri sidhani kama alisema ameshaunda hiyo kamati maana najua akishaunda tu lazima majina yatakua hadharani sio jambo la siri hilo.
   
 12. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lowassa anataka kuwa Putin...lol
   
 13. D

  DENYO JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Prof issa shivji kusaidiana na dr slaa wanafaa kuongoza tume ya katiba mpya
  Kama jk anataka kweli kuondoa fitina na kulitakia mema taifa hili-basi watu hawa wawili wanafaa kabisa kwa vyovyote na kwa maslahi ya umma kuongoza tume ya katiba mpya.

  1. Prof issa shivji amekuwa katika mchakato wa kudai katiba mpya kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi. Sio mnafiki, hanunuliki kama wasomi wetu wengi -anayetaka ukweli asome raia mwema la wiki ya jana atapata ukweli huu kutoka katika makala yake. Hayumbishwi. Nampendekeza awe mwenyekiti wa tume hiyo

  2. Dr w. P. Slaa ni mtanzania mwenye msimamo aliyesababisha chachu ya katiba mpya, kama ilivyo kwa shivji slaa(phd) hanunuliki na hayumbishwi. Ni mtanzania aliyekuwa anagombea urais agenda yake kubwa ya kwanza ikiwa ni kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Ni mtanzania anayeona mbali na anayeitakia mema nchi hii, mwenye kuchukizwa na umaskini, ufisadi, ujinga, na maradhi ya nchi. Huyu anafaa kuwa katibu wa tume hii -aombwe ashiriki hatakama yeye mwenyewe hakubaliani na approach ya serikali ya jk. Lakini kwa jk kumuomba na kumtumia katika tume hii wote wawili watakuwa wameweka historia ya aina yake kwa maslahi ya umma.

  Tunao watanzania wengine kama jaji kisanga,ulimwengu, ayoub lioba, amiri maneto, bomani -hawa wanaweza kutumika kama wajumbe pamoja na mama nkya, ila hoja kubwa ni kutaka watanzania wazalendo wa kweli -nilisikitishwa na tume ya bomani ya madini ambayo mpaka leo bado wizi wa madini unaendelea -ndio maana slaa(phd) hataki tume hizi kwa kuwa zinakuwa hazipo huru.

  Haya ni maoni yangu na ninaamini wapo wana jf watakubaliana na mimi kwa kupitia reference ya tume zilizowahi kuundwa huko nyuma na matunda yake. ​
   
 14. F

  Fareed JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, ambaye alihoji "Katiba mpya ya nini?" kwa mujibu wa cheo chake kama mshauri mkuu wa masuala ya sheria wa serikali lazima awe mjumbe wa Constitutional Review Commission ambayo Rais Kikwete anatarajia kuiunda.

  “Tunapaswa kujiuliza Watanzania wanahitaji nini? Mimi binafsi ukiweka wadhifa wangu kando, bado sioni haja ya Katiba mpya, lakini kama ni Watanzania wanataka mpya sawa, wakitaka marekebisho pia sawa,” Werema alikaririwa akisema na gazeti la serikali, Habari Leo.

  “Kila mtu anazungumza kama bata, watu wanazungumza kibatabata, lazima tujiulize Watanzania wanataka nini? Wakati fulani iliwekwa vifungu vya haki za binadamu kuanzia kifungu cha 12 hadi 29 kwa kuwa vilihitajika, tuzungumze si kutishana,” alisisitiza Jaji Werema huku akitolea mfano Katiba ya India ya mwaka 1948 iliyofanyiwa marekebisho mara 50.

  Sasa kwa msimamo wake huu, sidhani kama mchango wa AG kwenye tume ya kupitia katiba kama utakuwa na tija.

  Huko kwa jirani zetu kenya, wao waliunda Committee of Experts kuandaa katiba mpya. Bofya hapa ili kupata taarifa za uzoefu wa Kenya kwenye katiba mpya:

  About us

  Wajumbe wa kamati hiyo ya Kenya ya kupitia katiba walikuwa hawa hapa:

  Profiles of members of the Committee of Experts

  Nimevutiwa na kauli mbiu yao -- Katiba mpya ni SASA kama siyo SASA ni SASA HIVI!.

  Katiba Mpya, Tanzania Moja
  ...
   
 15. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Magazeti gani hayo?
   
 16. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Rais kasema juzi tu katika hotuba yake ya kukaribisha Mwaka Mpya kuwa ataunda Tume itakayofuatilia Katiba Mpya. Alisema wadau wote, wakiwemo wanasiasa, wafanya biashara, viongozi wa dini na wananchi wengine watakuwepo. Tumpe muda, na papo hapo tuanze kujiandaa kuchangia wakati hiyo Tume itakapotutembelea.

  Mimi naandaa Mada yangu ya Maboresho ya Katiba nitakayotoa kwa Tume.
   
Loading...