Waliokufa ajali ya Nzega waongezeka


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
waliotambuliwa hadi jana ni Faustine Simon wa Katesh, Manyara; Pastory Kaiza; Epelanya Mleke; Gerald Nyitwe ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kikosi cha 39 Arusha; Julieth Rupia wa Mwanza na Stephen Malolo wa Shinyanga.

Wengine ni Noel Munisi; Paul Boniface wote wa Manyara; Ritha Thomas wa Moshi; Magreth Asenga (Moshi); Elizabeth Uriki ambaye ni Mtawa wa Kanisa Katoliki (Mwanza); Salome Richard (Babati); Doria Agai (Mwanza); Joachim Paul (Nzega); James Agai (Mwanza); Abeid Ngayanimo (Nzega), Milambo Benjamin (Nzega) na Benson Ochieng.

Aidha, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Dk. John Mombeki, alisema majeruhi wanne waliovunjika miguu na mikono walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza kwa tiba zaidi baada ya madaktari wa hospitali hiyo kukosa uwezo wa kutoa matibabu zaidi kwa majeruhi hao.

Aliwataja majeruhi waliokimbizwa Bugando kuwa ni Nakijiwa Ibinga wa Same Kilimanjaro; Prosper Magacha (Hanang); Joyce Nyanda (Nyakato - Mwanza) na Chega Msila (Mwanza). Dk Mombeki alisema majeruhi wengine wawili waliokuwa wakikimbizwa pamoja nao kwenda Bugando, walifariki dunia njiani, hivyo kufanya idadi yao kuwa 26 baada ya juzi watu 24 kufa papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea kati ya Kitangiri na Migua kiasi cha kilometa 12 kutoka Nzega mjini.

Alisema kulingana na taarifa za kitabibu, majeruhi wengine sita wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Bugando kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia majeruhi waliobaki hospitalini hapo, Mganga Mkuu wa Wilaya alisema wanaendelea vizuri na wamekuwa wakipata tiba kama inavyotakiwa na wakiendelea hivyo, wataruhusiwa kutoka siku chache zijazo.

Katika hatua nyingine, imebainika kuwa mtoto ambaye hajatambuliwa jina, ni miongoni mwa majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.

Dk Mombeki alisema mtoto huyo amepewa uangalizi maalumu kutokana na umri wake kuwa mdogo kuliko wote walionusurika katika ajali hiyo na afya yake inaendelea vizuri. Inahisiwa kuwa mzazi au mlezi wake aliyekuwa akisafiri naye kwenye basi hilo alipoteza maisha.

Alisema pamoja na mtoto huyo, pia watoto wengine mapacha wenye umri wa mwaka mmoja wamenusurika na wamelazwa hospitalini hapo. Mganga Mkuu aliwataja watoto hao kuwa ni Brighton na Brightness Juma ambao wanaishi na wazazi wao Mwanza ambapo pia mtoto mwenye umri wa miaka miwili, Mary Ochieng alinusurika.

Ajali hiyo ilitokea juzi jioni wakati basi hilo aina ya Scania namba T316 AZR, lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mwanza, kupata ajali kutokana na kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi. Hii ni ajali ya kwanza kutokea Tabora mwaka huu na kuua idadi kubwa ya watu.
 

Forum statistics

Threads 1,250,456
Members 481,354
Posts 29,733,684