sumbai
JF-Expert Member
- Jun 16, 2014
- 18,510
- 41,750
asikuambie mtu swala la kupata kazi haijalishi umesoma chuo gani wala kozi gani ni MUNGU apangaye, nyota yako pia inahusika na juhudi binafsi, NIMEONA UDOM GRADUATE wameajiriwa maeneo mengi gvt. Na private sector, huku UDSM wakilia njaa na wakati walikua wanaponda elimu ya UDOM NA KUA WAHITIMU WAKE HAWAAJIRIKI
binafsi nmemaliza udom 2012 nkapata job gvt. 2014 mwishoni huku chuo nlikua wa kawaida tu, nachemka kwenye Seminar, ila kweli kupata kazi ni bahati, leo waliokua wanancheka sijui hata presentation wako mtaani wana haso, MUNGU awasaidie wafanikiwe plus wale wa udsm waliokua wanaponda udom
Kama msomi hautakiwi kukurupuka, nadhani ungefanya utafiti ili hoja yako ikawa kisomi maana wewe ni mhitim wa chuo kikubwa UDOM
Wasomi wanatumia njia mbadala kujenga hoja na sio kama watu wa mtaani jaribu kujitofautisha katika hilo.
Unauhakika upi kwamba graduate wote UDOM wamepataka kazi? Au udsm wengi hawajapata kazi? Lete data hata kuanzia 2012.
Swala la kupata kazi ni swala mtambuka, swala la kuajiliwa wahitimu wa chuo au fani fulani kwa wingi linategemea na uhitajikaji wa soko la ajira kama unataka kuzungumzia in aggregate.
Swala la wewe mmoja kupata kazi tena serekalin halizuii uvumi kwamba watu fulan fulan from chuo fulan hawaajiriki.
Na pia mfano je ungekuwa umepata kazi zile za kwenye kampuni kubwa na nyeti zinazolipa vzuri ungesemaje?
Mshukuru Mungu kwa kupata kazi, fanya kazi usiwe mzigo huko ulipo
Msomi acha majungu na myth za mtaani, jenga hoja kisomi
La sivyo unatafuta majibishano ya ushindani wa kivyuo ambao ni wa kitoto....mambo ya kiferst year...