Waliokata tiketi Tanzania na Chad kurudishiwa pesa

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Waliokata tiketi Tanzania na Chad kurudishiwa pesa




Kizuguto-pic.jpg

Afisa Habari wa TTF Baraka Kizuguto

TFF inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata tiketi za mchezo huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika vituo walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa TTF Baraka Kizuguto, zoezi la kuwarudishia fedha washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za mchezo kati ya Tanzania v Chad litafanyika katika vituo vinne vilivyokua vikiuza tiketi siku ya Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo wanaombwa kufika na tiketi zao ili waweza kurudishiwa fedha zao.

Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu uliojitokeza na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki ambacho wanasubiria taarifa zaidi kutoka CAF.

Chad imejiondoa jana katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017, ambapo iliku kundi G na timu za Misri, Nigeria pamoja na Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom