Waliokamatwa kwa tuhuma za uongo za kusherehekea Kifo cha Hayati Magufuli walipwe fidia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,428
Hii ni Taarifa ninayoipeleka kwa Tume ya Haki Jinai , kwamba kama kweli tunataka haki basi wale wote waliodhalilishwa na kukamatwa kwa tuhuma za uongo za kufanya sherehe kutokana na kifo cha Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli Walipwe fidia haraka sana na kuombwa radhi .

Naweza kuthibitisha kwamba , aliyekuwa RPC wa Mbeya Ulrich Matei alitangaza hadharani na mbele ya vyombo vya habari , kwamba watu kadhaa kutoka eneo la Mwanjelwa wamekamatwa kwa kukutwa wanakula supu ya mbuzi na kunywa Pombe, na kwamba jambo lile lilitafsiriwa kama kusherehekea kifo cha Magufuli , watu hawa wasio na hatia yoyote walidhalilishwa na kusingiziwa ushenzi huo ambao hawakuhusika nao , jambo lililowadhalilisha wao binafsi na familia zao mbele ya jamii na kuwavunjia heshima, hatujui kilichowakuta huko polisi walikopelekwa , kama waliteswa , waliuawa ama waliachiwa.

Yaani mtu kapata hela yake kwa kuuza viazi na vitunguu alivyolima mwenyewe kwa jasho lake , leo anaamua kujipongeza kwa Supu na pombe zake inaonekana anasherehekea kifo cha Magufuli ! Hii ndio intelijensia ya Polisi wa Tanzania ilipoishia ! lakini wale Matapeli waliojifanya kuzimia huku wameshika mifuko yao ya Sangara mkononi hawakuonekana kufanya kejeli, wakaachwa na maigizo yao ! mtu anawezaje kuzimia huku kashikilia mfuko wenye mali zake mkononi?

Katika_Historia%3A%0APamoja_na_kwamba_ALIZIMIA_baada_ya_kuuona_mwili_wa_mpendwa_wetu_MFUKO_hak...jpg


Tunaomba tume hii ya Haki Jinai ihakikishe inafuatilia Wote waliokamatwa wakati wa msiba wa Magufuli kwa sababu kama hizi za kijinga, waangaliwe kama hawakuuawa na Walipwe fidia stahiki kwa uonevu waliofanyiwa na kama waliuawa basi ni vema Wahusika wote wakakamatwa na kuchukuliwa hatua.
 
Dhumuni la kuundwa kwa hii tume wengi hamjalielewa. Hii tume haipo kwa ajili ya kushughulikia mtu au kikundi cha watu kwenye taasisi za haki jinai ambao walitenda makosa fulani. Lengo la tume ni kukusanya maoni, kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya kuboresha taasisi za serikali zinazohusika na haki jinai kama vile Polisi, Mahakama, PCCB n.k.

Tuweke utaratibu upi ili zitende haki na kuacha kuonea watu? Kama unapeleka maoni jikite kwenye hilo swali. Sio upeleke malalamiko eti askari fulani au afisa wa mahakama alitenda kosa hili hivyo ashughulikiwe. Hiyo sio kazi ya tume. Haipokei malalamiko wala tuhuma dhidi ya afisa/ maafisa fulani. Inapokea maoni ya jinsi ya kuboresha mifumo yetu ili maafisa hao wa taasisi za haki jinai wasiweze kutumia madaraka vibaya. Una nafasi ya kunikosoa.
 
Back
Top Bottom