Waliojiuzulu udiwani Meru wabwagwa kura za maoni CCM, wamwangukia Magufuli

Walijiuzulu,tena wanagombea nafasi hizo hizo walizojiondoa ?Wana akili kweli hawa?
Hayo ndio baadhi ya masharti waliyompa Mnyeti , ushahidi wa video unaonyesha kwamba waliahidiwa pia ajira halmashauri , na tayari baadhi wameajiriwa .

Kumbuka sheria inamtaka diwani awe na ajira inayoweza kumpatia kipato cha halali .
 
Katika kata zote ni Emmanuel Mollel peke yake wa kata ya MAKIBA aliyeibuka kidedea, wengine wote katika kata zao wameangukia pua maskini!

Kituko kikubwa ni kata ya Ambureni Japhet Jackson ambaye NAYE alijiuzulu udiwani kupitia CHADEMA kwa ahadi ya kupewa nafasi ya kugombea ndani ya CCM, yeye alipata kura 4 (kati ya hizo 2 alizawadiwa na mwenyekiti wa kikao ili kuficha aibu).

Ndugu huyu sasa anahaha kufanya mazungumzo na viongozi wa wilaya akiwakumbusha ahadi aliyotoa Mwenyekiti wa CCM John Magufuli, stadium kuwa "tutawarudisha hawa hawa" Kura zilipigwa jana lakini leo ameamkia wilayani na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa apate tiketi ya kugombea udiwani aliouachia.

Wajumbe wa kamati ya siasa wana mkejeli kuwa atajiju, lakini wengine wapo bega kwa bega na yeye.

Pia PCCB walifika katika shule yake kuulizia kama kuna nafasi ya kuleta watoto (walijifanya wazazi wahamiaji), jamaa akawaambia shule ilifungwa. Itakumbukwa kuwa moja ya ahadi alizopewa ili kuachia udiwani ni kufunguliwa kwa shule yake ambayo ameijenga kwenye tindiga ambayo serikali waliifungu.

Lakini baada issue ya Nassary kubumburuka, wakaifunga haraka, hivyo PCCB walipokuja kwake aligundua mtego akategua. Balaa hii!!! udiwani hana, shule bado imefungwa.

Nitaendela kuwajuza.

Wana haha nini wakati wamelipwa mafao yao mpaka 2019? Waambieni waache tamaa zao za kimalaya.
 
Kama CCM watawapitisha hawa kugombea nafasi walizojiuzulu kwa hiyari yao, basi huu utakuwa ni udhaifu wa hali ya juu kuwahi kutokea ndani ya chama!!
 
Walijiuzulu,tena wanagombea nafasi hizo hizo walizojiondoa ?Wana akili kweli hawa?
Watanzania wa level ya uongozi wana ujinga kama huu, sasa inakuwaje kwa wengi wetu wa chini zaidi?
Bongo bahati mbaya kweli. Hatuwezi kupona tukiwa na watu wa ajabu sana kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom