Uchaguzi 2020 Funzo nililolipata baada ya kupata 0 kwenye kura za maoni za udiwani CCM

Mc PIPI

JF-Expert Member
Feb 25, 2020
319
435
Salamu zenu wakuu,

Kwa mara ya kwanza nami nikiwa Kama kijana nikatia nia ya kugombea udiwani kupitia CCM huko Katani kwetu.

Namshukuru Mungu mwingi wa rehema kwangu kwa kunipa ninachostahili katika zoezi lile la kura za maoni zilizofanyika jana siku ya Jumamosi ya tarehe 25/07/2020.

Kwanza nilijitahidi kukutana na wajumbe kadhaa kuwaeleza dhamira yangu ya dhati ya kuwatumikia maana kata yet in changamoto sugu mno wapendwa,na hii Hali hivyo kutokana na ukweli usiopingika kuwa diwani aliyekuwa akitetea kiti hana siasa zenye manufaa hata kidogo,kwa ufupi tu ni mzee,ameishia darasa la 4,si mzawa wa ile kata na mpaka sasa aslimia 80 ya shughuli na makazi yake yapo nje ya kata yetu.

Basi kwa kaelimu haka nilikopata nilamini kwamba kwa haka ka CV nilikonako basi nikirudi Kule nyumbani kuwa naamua kuiweka rehani ajira yangu kwa kuwaeleza hoja kisomi namna tunavyoguswa na changamoto za katani kwetu maana mkataa kwao ni mtumwa.

Basi kweli nikawaeleza wajumbe wengi tu wakifurahishwa na ujio na wakanipongeza Sana na wakasema hawataniangusha,basi nikawaamini na sikuona sababu ya kutoa rushwa nikiamini kuwa ukweli wangu na uadilifu mkubwa utanipa kura za kutosha kuliko wale wanaomwaga hela mtaani.

Kumbe nilikuwa najidanganya,wagombea tulikuwa 8,watatu tulikuwa watumishi wa umma,mmoja ni mstaafu,watatu ni Drs la 7 kwa elimu yao na mmoja aliishia Drs la 4(mgombea aliyekuwa anatetea nafasi yake)

Baada ya kura za maoni matokeo yakawa kama ifuatavyo:

- Anayetetea kura 23 (Drs la 4)
- Wa pili kura 22 (elimu VII)
- Watatu kura 14(elimu VII)
- Wa nne kura 1(mwajiriwa) nayo alijipigia mwenyewe kwa sababu ni mjumbe.
- Wa tano kura 0 (elimu VII)
- Mstaafu kura 0.
- Mimi na mwenzangu kura 0 (vijana wasomi na waajiriwa)

Wapiga kura walikuwa 63, kura tatu ziliharibika.

FUNZO NILILOLIPATA
1. Katika kugombea kitu Cha kwanza ni MTAJI WA FEDHA KWA AJILI YA RUSHWA.
2. Jambo la pili ni UNAFIKI.
3. CV ni na ukweli ni Jambo la ziada tu.

Nimefurahi kupata hiyo 0 maana hata ningepata kura moja tu ingenisumbua kwa kuanza kujiuliza ni Nani aliyenipa hivyo Kila mmoja angekuja kinafiki kusema amenipigia yeye kumbe ni uongo.

Gharama zote nilizotumia katika mchakato huo nimechukulia kuwa ni sawa na kuwa nililipa ada ya kujifunza siasa kwa vitendo.

Sijavunjika Sana moyo na sirudi nyuma,dhamira ya kuwatumikia wananchi bado ipo hata kwa awamu nyingine huku nikisahihisha makosa yaliyonigharimu awamu hii,nitamuunga mkono yeyote atakayeteuliwa na chama,Wala sihami chama.

Wengi wamenipa pole lakini kiukomavu nimejibu kuwa wasinipe pole Bali hongera,ila pole hiyo itawarudia wao endapo wamepiga kura kinafiki kisa tu wamejazwa minoti na hivyo watakuwa wamesaliti matakwa ya wananchi lakini na endapo kweli wamepiga kura kwa uhalali basi nami naungana nao kwa baraka zote.

Kwa taarifa zilizopo sasa, jana ileile watu walianza kurudisha kadi za chama wanataka kuhamia CHADEMA. Wale wote waliopata kura nyingi Kila mtu alitengeneza kundi lake na hivyo linahatarisha sana uhai wa chama maana wananchi wanatoa kauli za kutotoa ushirikiano endapo yule diwani anayetetea nafasi akirudishwa kuwa mgombea maana hawaoni matunda yake kwa miaka yote 15 aliyotumikia. Wote watatu walitoa Sana rushwa ima walizidiana viwango.

Hii ndiyo ndiyo siasa ilivyo, tukutane 2025.

Ni Mimi niyeyekuwa mtia nia Udiwani CCM.
Kata ya UHENGA
Jimbo & Wilaya ya Wanging'ombe
Mkoa NJOMBE.
 
Tatizo lenu nyie mnaojiita wasomi, huwa mnadharau Sana wajumbe huko mtaani
IMG-20200725-WA0000.jpg
 
Hongera mkuu CCM yote inanuka rushwa na hivyo maendeleo ya nchi hii tutasikia Kenya tunasema kila siku angalau tupunguze huu utopolo lazima tuwe na katiba mpya ambayo itaweka misingi ya maendeleo kuanzia kwenye serikali, mahakama, pamoja na bunge, sasa wewe fikiria wabunge 300 wamehonga wajumbe ili wapate ubunge hivi tunakwenda wapi kama taifa? Hongera kwa kujaribu
 
Hongera mkuu CCM yote inanuka rushwa na hivyo maendeleo ya nchi hii tutasikia Kenya tunasema kila siku angalau tupunguze huu utopolo lazima tuwe na katiba mpya ambayo itaweka misingi ya maendeleo kuanzia kwenye serikali,mahakama,pamoja na bunge ,sasa wewe fikiria wabunge 300 wamehonga wajumbe ili wapate ubunge hivi tunakwenda wapi kama taifa? Hongera kwa kujaribu
Rushwa ipo kila sehemu sio CCM tu, ipo kila chama na karibia kila taasisi. Rushwa ni tabia ya mtu sio taasisi
 
Tatizo lenu nyie mnaojiita wasomi, huwa mnadharau Sana wajumbe huko mtaaniView attachment 1517351
Hahaaaaa, haipo hivyo mkuu, majukumu ya ajira yanafanya kwa kiasi Fulani kutoshirikiana kila Jambo na hao wajumbe na hivyo kuonekana Kama tunawadharau kumbe sivyo. Lakini kwakuwa nimejifunza kitu, 2025 nitakuwa mtu tofauti na 2020.
 
Mkuu pole sana, lakini nimetatizwa na sentensi yako kwamba "sijavunjika moyo, nitajaribu awamu nyingine huku nikisahisha makosa yaliyonigharimu awamu hii" mwisho wa kunukuu. Kwa maelezo yako makosa yaliyokugharimu ni kutokutoa rushwa na kutokuwa mnafiki.Kwahiyo unataka kutuambia awamu ijayo utatoa rushwa na kuwa mnafiki?
 
Back
Top Bottom