Walioichagua CCM wanajisikiaje huko waliko? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walioichagua CCM wanajisikiaje huko waliko?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 5, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Pamoja na mambo yote ambayo husemwa kuhusu wapinzani lakini ukweli ni kuwa nchi yetu imetekeleza na inaendelea kutekeleza sera zilizobuniwa na wana CCM na sheria zilizopitishwa na bunge la CCM na marais wa CCM. Miaka nenda rudi mafanikio yote ambayo tunayaona katika sekta mbalimbali ni mazao ya CCM na serikali yake na kinyume chake pia ni kweli - kwamba madudu yote tunayoyasikia na kuyaona ni mazao ya CCM hiyo hiyo.

  Haiwezekani hata kwa mbali kuilaumu CHADEMA kwa matatizo ya sekta ya afya, kilimo, miundo mbinu n.k Haiwezekani na kwa kweli haiingii akilini kabisa kuilaumu CDM, CUF au chama kingine chochote kwa matatizo mbalimbali tunayoyana nchini - yawe ya hali, utu, nafasi n.k YOte haya yametokeana na yanaendelea kutokea chini ya CCM chama ambacho kimeshikilia Bunge na Urais kwa miaka 50!

  Kama hili ni kweli - na hakuna namna ya kuonesha kuwa siyo - wale ambao waliichagua CCM mwaka 2010 na ambao wanaendelea kuichagua CCM huku wakiona yote haya huwa wanajisikiaje? Hivi wanaweza kulalamika wakiambiwa kuwa serikali haina fedha, au wakiona madudu mbalimbali? Hivi wenzetu hawa huko waliko yawezekana kabisa wanaamini kuwa labda huko mbele ya safari atakuja mwana CCM mwingine kutengeneza kilichoharibiwa na CCM? Kweli ndugu zetu hawa wapendwa huko waliko wanaweza kuamini kabisa kuwa yupo mwana CCM ambaye anaweza kuja na kufanya tofauti na kilichofanywa na wana CCM wenzake kwa miaka hamsini ijayo?

  Kweli kabisa ndugu zetu hawa bado wanaamini na kuombea kuwa uongozi ujao uwe wa CCM? Ni kitu gani kinawapa matumaini hivi wakati wana historia ya miaka hamsini nyuma yao? Sisemi kwamba wana CCM wote ni wabaya au kwamba hawafai lakini bahati nzuri sana tunayo rekodi; angalia wanavyozungumza Bungeni, wanavyoonekana kabisa kuwa wako kwa mujibu wa ibara ya 15.1 (kama siyo ya 14.1) ya Katiba yao kwa kweli.

  Sasa huko waliko wanavyoona yote yanayotokea nchini huwa wanafikiria nini kwamba yawezekana "shetani ameingilia chama" au kuwa ni "bahati mbaya" tu?
   
 2. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Haya ni mwazo tu. Naamini fika kuwa wengi wa Watz wanaopiga kura ni kama vile hawajitambui kama ndio wananchi wenyewe wa Tanzania. Maana wanapopiga kura wanakuwa na mawazo ya karibu si unajua kipindi cha kampeni wengi wanakuwa wanapata ofa kede kede (mf: kofia, vitenge/kanga, T-shirt, ubwabwa, kiti moto nk). Wengi wetu tunajua fika kuwa hali ya nchi yetu ni mbaya sana lkn bado tunarudia makosa yale yale.

  Sitaki niamini kuwa ushindi wa CCM kwa kiasi kikubwa unachangiwa na vyombo vya dola. Ushindi wa ccm unapatikana kwa kwa wananchi hawa hawa wenye matatizo kukichagua hakuna kitu zaidi ya hicho. Na kwa kiasi kidogo vyombo vya dola. Mimi bado nina imani kuwa Rais Kikwete pamoja na udhaifu wake mkubwa anaweza kutupa katiba tunayoitaka Watz; ndipo hapo sasa mbivu na mbichi tutazijua. Kama ndio ccm wanaiba au watz tunawapa kwa hiari zetu.

  Mimi sioni sababu ya watz kulalamika kila kukicha kwa maana makosa tumetenda wenyewe tukae kimya tu. Kama ni kufa kwa njaa wacha tufe. Kuna umuhimu gani wa kulalamika na hali wajibu wetu hatutekelezi? Eti hatuna maji, mfumuko wa bei mkubwa: haya tunamweleza nani?

  Hawa hawa Watz ndio watakao iondoa ccm. Kwa mwono wangu ccm itaondoka tu wala hatuhitajimuda mrefu kuona haya mambo ila hatujui lini. Maana pamoja na kuwa watz ndio wanaoipa ccm kura lkn bado hatashindwa kuipa kura. Wale wakuendelea kuipa kura wataendelea na wale wasio na desturi ya kuipa kura idadi yo itaongezeka na ndio vijana watakaoindoa kwa njia ya kura. Hili ndilo litakalo tokea. Ccm haitaondoka kwa vita itaondolewa na vijana, ambao wengi wao watapiga kura 2015.

  Tuna kila sababu ya kuwalaumu wapiga kura kwa maana yhaya ni makosa yao. Lkn kwa upande mwingine itasaidia nini kuwalaumu wazee, akina mama ambao hawatambui haki zao kama raia mpiga kura? Tunajua kuwa mpiga kura kwa nchi za kidemokdasia ndiye anayeamua nani kiongozi bora wa kuiletae taifa lake maendeleo? Sasa wengi wetu tukiambiwa mkichagua upinzani mtaingizwa vitani, halafu kwa akili yako unaanza kusema ehh! kweli bwana hawa hawatufai.


  Kwa vijana wengi wanaoibukia hizi ni stori na kupitia kwao hii nchi itkombolewa kutoka mikono ya ccm.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Swali lako ni kama vile kusema unajisikiaje kuchagua huyo mwanandani wako??? hata wajutao hukaa kimya (in most cases)
   
 4. D

  DOMA JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mpaka najisikia kinyaa maana nilijua nawakomoa wafuasi wa chadema kumbe najikomoa mwenyewe 2015 sirudii tena
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  .....Mimi naamini hawakuchaguliwa bali walichakachua uchaguzi katika majimbo mengi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na tume ya uchaguzi ya magamba.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  BAK, ili kuweza kuchakachua CCM ilihitaji walau kura chache za kuanzia! In 2015 under normal circumstances I would expect CCM to get 0 votes, otherwise in a few places wapate kura 10-15 kwa maana ya mgombea, mkewe na small house kuipigia ccm!
  Suala ni je, watz wangapi wana akili ya ku-connect matatizo yao na uchaguzi wao? Ama wanaskia tu kelele za 'msiwachague wapinzani, amani itatoweka'
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kamanda, ukishaona baba ana-declare mbele ya mama na watoto katikati ya mwezi kuwa nimefulia, ilhali katoka kwenye besdei ya rafiki yake wa kazini ujue kimeumana. Hapo mwanamke mwenye akili anajua hakuna mume hapa, na watoto watasema dingi vipi? Halafu baba hana solution, anasema tu anachekacheka anakuwa kamaliza! Hasemi hata tulime mchicha, tuuze maji etc! Kugugumia choice kuna mwisho wake banaa ndo maana kuna divorce!
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,389
  Likes Received: 3,711
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa ni kuwa kuna watu wanaiona CCM ni kama timu ya mpira wa miguu, hata ifungwe vipi hawahami..!! Sema toka moyoni kwako, ulishawahi kuhama kushabikia timu? Kazi tuliyonayo ni kuwahamisha watu wa sampuli hii.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,450
  Trophy Points: 280
  Ni kweli usemacho Kin'gasti...maana wengi wakishapewa pilau, soda na beers, fulana, kofia na kanga za magamba pamoja na vijisenti vichache basi wanajiona wamepata sana na kusahau maisha yao duni miaka nenda miaka rudi na kuwapigia tena kura magamba...na wengine wakiamini kabisa kwamba CHADEMA ni chama cha kikabila na pia cha kidini....kauli ambayo ni uzushi mtupu.

   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  BAK, kama kuna mtu nina hamu ya kuongea nae ni yule mzee aliyefiwa na mwanae kwa kugongwa na gari kwenye mkutano wa ccm kule igunga! Alithubutu kusema on tv ataipigia ccm kura manake wameonesha kujali kwa kutoa rambirambi sh 1M, na aliikebehi wazi rambirambi ya chadema. Natamani anaiambie mafanikio ya hali yake enzi za RA na sasa mbunge wao mpya kama anakumbuka hata jina manake hata sijawahi muona akiongea bungeni! Shida haijakolea sawasawa, tutajiamsha usingizini!
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mzee MM mimi natamani ccm nchi iwashinde zaidi ya hapa na hali iwe ngumu mara kumi zaidi, ikiwezekana ipite hali ile ngumu ya 1980 baada ya vita ya Kagera.. hawa wahongwa pilau huwa hawaelimiki kwa mikutano ya hadhara na elimu ya uraia ila linapokuja swala la ugumu wa maisha wanaingia darasa la nguvu.. najua tutaumia sana lakini ni njia ya kutufikisha pazuri. Wenzetu wanaumia kwa mapambano ya mtutu wa bunduki lakini hilo la ugumu wa maisha naliona ni bora zaidi na litafungua wengi akili.
   
 12. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huu ni mchanganuo mzuri sana ambao unaweza kuendana na maswali makuu mawili ya msingi ili kupata jibu. Wapo waliofanya hivyo kwa sababu mbalimbali, lakini la msingi ni Je wale walioshinda CCM walishindaje kuanzia kwenye kura za maoni mpaka uchaguzi mkuu? Kumbuka hapa kuna majimbo yenye wananchama wa CCM 7000 halafu mshindi anapata kura za maoni ya CCM 20,000. Hizo nyingine alizipata wapi? Uchaguzi mkuu tukienda taratibu angalia Rukwa, Shinyanga hata Dar ambako mnasema kuna wajanja waulize kina makongoro wameshindaje utapata jibu la wengi wa walioichagua CCM. Elfu 2015 inaweza kuwa hivi hivi halafu tukajiuliza tena swali hili hili. La msingi, Je waliowashinda CCM walifanyaje? Angalia kwanini Wenje alimshinda mtu maarufu kama Masha na kwanini Shibuda aliyetakiwa sana ashindwe Maswa alishinda utapata la jibu nini kifanyike ifikapo 2015
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  there you go.... mie siku zote naanzia analysis za maisha yetu ndani ya familia kwani ndio the nucleus ya maisha yetu

  rais wangu amenitia aibu, anazunguka na tiara, anarudi anakuta mama na watoto wa shida nyingi, anaingia ndani, anachukua gazeti na kunong'ona na mama maneno yasiyo na msaada kwa family... si ajabu akaanza na kuomba penzi, ilhali mama ana fadhaa moyoni na mwilini kwa ujumla

  HUYO KWANGU NI SAWA NA BABA ****......... ALIYE OUT OF TOUCH NA FAMILIA YAKE, HUTOKA AMEVAA KITANASHATI NA MANUKATO YA KUUA MTU, WAKATI WATOTO WANASHINDWA HATA KUJAZA MATUMBO ILI WAENDE CHOONI

  I READ SOMEWHERE KWAMBA MTU WA NAMNA HIYO NI KAMA ANA LAANA FULANI
   
Loading...