Walioiba begi la mugabe lililojaa pesa wapandishwa kizimbani

Walioiba begi la mugabe lililojaa pesa wapandishwa kizimbani

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Posts
4,510
Reaction score
6,893
Watu watatu wanaotuhumiwa kupanga na kufanikisha kumuibia Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe begi lililojaa pesa, wamekamatwa na kuburuzwa Mahakamani.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa watu hao ambao mmoja wao ni ndugu yake Mugabe aliyetajwa kwa jina la Constantia Mugabe waliiba begi lenye $150,000 lililokuwa ndani ya nyumba ya mwanasiasa huyo mkongwe.

Wengine waliotajwa walikuwa wafanyakazi wa maeneo ya nyumba ya Mugabe ambao ni pamoja na Saymore Nhetekwa na Johanne Mapurisa waliokuwa wafanya usafi.

Akitoa maelezo mahakamani, mwendesha mashtaka wa Serikali amesema Constantia alikuwa na funguo za baadhi ya vyumba vya nyumba hiyo na kwamba ndiye aliyewasaidia wenzake kuingia ndani.

Imeelezwa kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kati ya Desemba Mosi na mapema Januari. Wanadaiwa kutumia fedha hizo kununua magari, pikipiki pamoja na wanyama wa kufuga.

“Johanne Mapurisa alinunua Toyota Camry, na nyumba moja kwa $20,000 kwa kutumia fedha hizo,” mwendesha mashtaka Teveraishe Zinyemba aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Chinhoyi.

“Saymore Nhetekwa alinunua pikipiki aina ya Honda na wanyama wa kufuga ikiwa ni pamoja na nguruwe na ng’ombe kwa thamani ambayo haijawekwa wazi,” aliongeza

Mugabe mwenye umri wa miaka 94 aliiongoza Zimbabwe akiwa Rais kwa kipindi cha miaka 37.

Mwanasiasa huyo alilazimika kujiuzulu mwaka 2017 baada ya jeshi la nchi hiyo kuingilia kati mgogoro wa kisiasa ndani ya chama cha Zanu-PF.

chanzo:dar24.com
 
Hao kweli mabwege " ..wanaiba kiasi chote hicho cha pesa " halafu wanafanya anasa za wazi wazi ... walikuwa wanasubiri nini kutokomea kusiko julikana " !!?


Kwamba walikuwa wanadhani hawato shtukiwa au ...!!? Kwamba mzee mugabe amezeeka sana kiasi kwamba hana kumbu kumbu za kukumbuka mahali alipo ziacha fedha zake .. !?

Ila wanasiasa waafrica nao ni nyoko yaani mtu anamihela mpaka anafikia kuhifadhi ml400 kasoro ndani ...duhh !!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah...

Ukishatoka madarakani unakuwa kama kuku tu.
Kila mtu anakufanyizia.

Mpaka mfagia nyumba yako anaweza kukufanyizia bila hofu yoyote.
Hahaha mzee ulinzi anaohafifu ....watu wanamchezea tu sharubu dadeki .... ukisikia kila mtume na kitabu chake ndio hiyo sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Days are numbered! no one gonna care when the button of forces and authority is no longer yours!

Unaweza kufa kwa stress kutokana na dharau unazofanyiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisaa ... bora ufe ukiwa kwenye rise ..kuliko u-fall " halafu uanze kupitia zile changamoto zake... weee unaweza kuyatamani mauti ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo la haka kazee kamecherewa sana kufa halafu unasikia sasa hivi ni mwendo wa kujikojolea na kujinyea
Duhh " kwahiyo amewekewa wafanyakazi wakumsafisha !!! Grace itakuwa ameshajitafutia kiben 10 chake chakumpa mautamu kitambo . . Sasa hivi kinamtafuna tu ..huku akisubiri mzee avute kamba .... Hapa ndio napouchukiaga uzee ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom