Waliohujumu CHADEMA watimuliwa

Waliohujumu CHADEMA watimuliwa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,991
Reaction score
63,866
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.


Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.


Akitangaza uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini, Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao, hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.


“Tuligundua kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile tulilokubaliana,” alisema.


Mbwilo alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.


Akizungumzia vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Chanzo:Habarileo
 
Ni vizuri, vita ya kuiondoa CCM inahitaji watu ambao wanajua ugumu uliopo si watu wanaoogwa kilo moja ya sukari na chumvi na kusaliti chama.
 
Bora ubaki na wawili waliosimama kuliko mia waliolala .
 
Hapo ndipo utakapo wakubali Chadema, Hawakai na uchafu kamwe...!!!

BACK TANGANYIKA
 
Wamefanya vizuri japo wamechelewa! Hujuma kama hizo zimejitokeza sana 2010 hasa kwenye ubunge! Baadhi ya wabunge wa upinzani wanaotoka Kanda ya ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya kusini, Kanda ya nyanda za juu kusini pamoja na Mawakala wao wanatajwa kuhusika kufanya majaribio ya kutuhujumu Wananchi kwa kuuza viti vyao(majimbo) kwa kupewa fedha na wapinzani wao ili wakubali kushindwa! Baadhi walifanikiwa kutuuza wananchi, lakini baadhi walishindwa kufanya hivyo kutokana na intelijensia kutufikia haraka Wananchi tukaweza kuzuia hujuma hizo kwa kuwapa onyo wahusika hadharani!
 
Udini, Ukabila, Vyeo, Ukanda na Ruzuku ndio vinaihujumu chadema!!!
 
Ni Chadema pekee kati ya vyama vyote nchini vyenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu kama hayo tunawajibu wa kujisifia na falsafa ya chama km sio mnafiki km sio mchawi km sio fisadi km sio mwizi wa escrow Epa na Richmond embu tupige makofi wote ya kushangilia Pamoja .
Km aitoshi Katibu mkuu Dk . Slaa siku chache zilizopita wakati akitoa shukrani zake kwa Umma na dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa moja kati ya maelezo yake alisema hivi naomba nimnukuu maelezo yake { Chadema haitasita kuchukua maamuzi magumu kwa kiongozi yeyote aliyechaguliwa kupitia Chadema hiwapo atatekereza wajibu wake ipasavyo kwa Wananchi na kwa Chama } mwisho wa kumnukuu
Sasa ukweli tuuseme wapi ? Umewasikia KINANA au NAPE akisema maneno km haya awawezi kusema kwa 7bu Ccm wanataka ushindi hawataki utendaji wa kiongozi kwa Wananchi waliomchagua
Chadema bora kukosa ushindi lkn kumpata kiongozi muadilifu kwa. Maneno ya Dk . Slaa yanatuaminisha Uadilifu wa Chadema kwa. Wananchi. Ma Ccm hawawezi kutoa kauli hiyo Chadema imewahi kufanya maamuzi kule Arusha ikawatimua madiwani 5. Na uchaguzi ukaitishwa upya wakaelewa. Malengo ya Chadema wakaipatia ushindi Hongera Chadema
 
Mbona hamkumtimua Torongei aliyeihujumu CHADEMA Chalinze? Na kuisababishia kushindwa vibaya?
 
Udini, Ukabila, Vyeo, Ukanda na Ruzuku ndio vinaihujumu chadema!!!

Mwaka 1995 mlitumia hila mbalimbali na nyingi kuidhoofisha NCCR-Mageuzi isiingie madarakani kwavile ilikuwa tishio kwa wakati huo chini ya Augustino Mrema! Mwaka 2000 mlifanikiwa kutuchonganisha Wakristo na Waislamu kwa propaganda za kitoto kuwa CIVIL UNITED FRONT-CUF ni Chama Cha Waislamu, kama vile haitoshi mkatumia Dola kutuaminisha kuwa wameingiza nchini makontena ya majambia(visu) kuvuruga uchaguzi wa wakati huo! Mwaka 2010 mkahamia kwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO-CHADEMA, kutufitinisha Waislamu na Wakristo kuwa aliyekuwa mgombea wa Chama hicho Dr Wilbroad Slaa ametumwa na Mapadri kuja kusimika mfumo Kristo madarakani! 2014 NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA wote wameungana wakiwa ni wahanga wa propaganda mbalimbali kutoka Chama kinachotawala nchi kwa sasa! Kama CUF ni ya Waislamu, CHADEMA ni ya Wakristo(Wakatoliki) na sasa wameungana tuwaiteje!? Na je CCM ni Chama Cha dini gani, wapagani!?
 
Back
Top Bottom