Waliohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wafikia hatua gani?

hajimadogo

Member
Dec 22, 2015
19
6
Wale ndugu zetu 40,000 wa Tanzania waliofungua kesi mahakama ya Afika Mashariki juu ya kuhoji uhalali wa uwepo nchi ya Tanzania wamefikia wapi?

April 26, 2019 Tanzania imeadhimisha miaka 55 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Muungano huo ndio uliozaa Tanzania ambao uliasisiwa na viongozi wawili wakuu wa nchi kwa kila pande. Upande wa Zanzibar kulikuwa na Sheikh Abeid Aman Karume akiongoza Zanzibar kutoka chama cha ASP, Upande wa Tanganyika kulikuwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitoka chama cha TANU.

Tuliambiwa Muungano ulikamilika April 1964 kwa viongozi hao kuuchanganisha mchanga/udongo kutoka Zanzibar na Tanganyika na kuwa mmoja. Kuna habari kua ili Muungano uvunjike kwanza ujibaguwe udongo wa Zanzibar ukae kwake na wa Tanganyika ukae kwake.

Jengine ni kwamba jina TAN (Tanganyika) ZAN (Zanzibar) I (ika) A (ar). Pia neno IA linasemekana lilifuata wigo kwa herufi mbili za mwisho kwa baadhi ya nchi za Afrika. Kwamfano, Nigeria, Namibia, Ethiopia, Mauritania, Algeria.

Sasa ninachotaka nijuwe uhalali upi unaotakiwa kwa huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa hawa watu 40,000 waliyofungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki.

#FUNGUKA TUPATE ELIMU
 
Mkuu kumbe ulikuwa unamfuatilia sheikh ilunga? Mzee alikuwa nondo sana yule.
Nilimfuatilia sana na niliwahi kumsikilizana ana kwa ana kwenye kongamano kipindi nipo Sekondari. Tulimualika akaja kutupa darsa kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo harakati kama zake.

Hayo maneno niliyoyaquote hapo juu, aliuchambua sana Muungano. Kongamano hilo lilifanyikia Zanzibar.
 
Kapambana sana ilunga kuchambua Zanzibar na muungano Wa Zanzibar na Tanganyika wanafanana ujasiri Aboud Rogo Wa Kenya ila Rogo alibezi sana ktk dini na ilunga alishambua ktk dini vilevile ktk siasa alichambua
 
@="hajimadogo,
Wanahangaika bure....Muungano hauvunjiki, na wala hauhojiwi kwenye mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika au Umoja wa Mataifa.

Mahali kote wanako enda hawana uhalali wa kuhoji muungano.
 
Izo kesi ni ngumu sana kwa mazingira kama hayo, Njia pekee ya urahisi ya Zanzibar kuweza kupigiania haki zao katika Muungano ni kwa kupitia serekali yao. Na ndio Mana CCM wanahakikisha Upinzani hauchukui madaraka kule Zanzibar.

Ila naamini wakiamua nakufuata ile mienendo ya waarabu kama Kule Sudan na Misri naamini kitaeleweka. Lakini kama wataendelea kuregea hapana kitu.
 
@="hajimadogo, Tayari kesi ipo kwa mahakama ya Africa mashariki, ilirudishwa mwezi wa April, na niliweka hapa baadhi ya documents zilizo chapishwa na mawakili ambao upande wa kudai uhalal wa muungano.

Wakati wowote mahakama itatoa terehe ya kusikilizwa.

Mnachukulia hili suala kama mzaha, hili linaenda kisheria, sio kama huu muungano wa kuunga unga.
 
Majibu yako haya
tapatalk_1557061381478.jpeg
tapatalk_1557061373310.jpeg
 
Tayari kesi ipo kwa mahakama ya Africa mashariki, ilirudishwa mwezi wa April, na niliweka hapa baadhi ya documents zilizo chapishwa na mawakili ambao upande wa kudai uhalal wa muungano.

Wakati wowote mahakama itatoa terehe ya kusikilizwa.

Mnachukulia hili suala kama mzaha, hili linaenda kisheria, sio kama huu muungano wa kuunga unga.
Ukiwachunguza watanganyika kiundani hasa wanatutegemea wazanzibar kumuondoa nduli mtawala mweusi ccm,wao waoga sana.
 
Jamaa alikuwa njema sana kwenye mbo ya historia .

Alikuwa na convicing power akiongea.

Alikuwa bingwa wa kusimulia historia.lakini nilikuwa najitega nikiogopa asinipeleke kwenye migomo migomo ya ajabu

Allah amrahamu
Kwa heri Ukoloni, kwaheri Uhuru.

Zanzibar tutamuachia nani?

Ulale salama unapostahili Shkh Ilunga Hassan Kapungu
 
Jamaa alikuwa njema sana kwenye mbo ya historia .

Alikuwa na convicing power akiongea.

Alikuwa bingwa wa kusimulia historia.lakini nilikuwa najitega nikiogopa asinipeleke kwenye migomo migomo ya ajabu

Allah amrahamu
Historia ndio inayobeba ukweli wa mambo. Huwezi kujua jambo kwa undani bila kujua asili yake(historia yake).

Hadi sasa hati ya Muungano haijulikani ilipo isipokuwa kwa wachache tu.

Japo alikuwa na madhaifu yake kwenye uchambuzi, aliutendea haki ujuzi wake wa kusimulia historia katika jambo husika alilolichambua.
 
Back
Top Bottom