Walioficha mabilioni Uswisi wahojiwa!

Walioficha mabilioni Uswisi wahojiwa!

Ni kutajanatajana tu basi! Ikifika uchaguzi tunachagua haohao tunaowataja. Kura zinauzwa na kununuliwa na hela hizohizo za madawa.

Akina Chenge sasa ni Mtemi Chenge kwa sababu ya pesa aliyonayo. Ni Mwenyekiti wa Kamati nzito ya Bajeti ya Bunge. Come 2015, Lowasa Rais, Chenge Waziri Mwandamizi kabisa kama sio SPIKA!
 
Wanaomiliki pesa nje hata kama ni kihalali wanalipia hizo pesa kodi sh ngapi? Je kiongozi wetu mkuu yupo tayari kutupa ushirikiano wake katika hili bila shurti?
 
Hapo ndipo ninapopata mashaka ya hii idara yetu ya usalama wa taifa. Wao wako independent na wanareport direct to the president lakini ndo hivyo kama tunavyoshuhudia hali ni shaghara baghara. Vinginevyo wanatimiza majukumu yao na reports zinafika kwa rais na hakuna hatua inayochukuliwa either nae yumo katika hao wafichaji au wamemsaidia kuipata hiyo nafasi so wanalindana. Nae atakapotoka atamsaidia ajaye na kulindana tena miaka na miaka. Mabadiriko makubwa yanahitajika katika mfumo wa uendeshaji wa hii nchi yetu.

Mkuu tuko pamoja hapa. Kwa ufahamu wangu mdogo, usalama wa taifa wanakusanya habari ambazo serikali kupitia polisi wanapashwa kuzifanyia kazi. Usalama wa taifa hawahusiki moja kwa moja kukamata wahalifu. Kuna uwezekano mkubwa taarifa zao zinakaliwa na "Mkubwa" na hivyo hazifanyiwi kazi. Haiwezekani hata kidogo kwamba mkuu wa nchi hajui Watanzania walioficha pesa haramu nje ya nchi. Nina wasiwasi na yeye yumo hivyo hawezi kuwachukulia hatua "wenzake"

Tiba
 
Tatizo la serikali yetu laweza kuw MFUMO WAKE! vinginevyo madudu hayo yasingekuwepo kwa kiwango kikubwa hivyo.
 
Watoto wa wakulima kama mimi ndo tunahangaika nchi hii, kutafuta mkate wa kila siku. Vigogo kadri wanavyopewa madaraka ndivyo wanavyozidi kuiba zaidi. EE MUNGU TUOKOE NA ROHO YA UBINAFSI KWA VIONGOZI WENYE DHAMANA YA NCHI
 
Unajua kwa hawa jamaa haya hapa chini sio majanga. Pengine kwa fikra zao hiyo sio Tanzania. Haileti picha kikundi kidogo cha watu kinamiliki mabilioni tena nje ya nchi huku wakinamama wa Kitanzania na watoto wako kwenye dhiki ya ajabu.
View attachment 106952
Hizi ndio shule zetu

View attachment 106953
Hii nayo eti ni Hospitali? Haina tofauti na NAZI CAMPS za Hitler.

Halafu magogo ya mbao yanasafiliswa kila uchao nje ya nchi huku vijana wetu wakiendelea kukaa chini ya vumbi halafu wanasema wanataka elimu bora. Na inasemekana magogo yanatumika kusafilishia meno ya tembo na madawa ya kulevya kweli kazi tunayo nchii hii ndani ya miaka 2 hii lazima tuimbe kila lugha.
 
Wataambiwa tu warudishe,huwezi kata tawi ulilokalia

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
likifanyika hata hilo la kurudisha nitashukuru, wasiwasi wangu wakiulizwa watachangia sh ngapi kwenye uchaguzi ujao kwa ajili ya chama chetu.
 
Sawa tumewafahamu, je mtawafikisha mahakamani.!
 
Hiyo ya Kumuondolea Kinga raisi aliyeko madarakani ikaa fresh
 
Huyo Zitto nae ameweka fwedha Uswiss ? kiasi gani?

Bora wanao iba na kuwekeza hapa pesa inazunguka vijana wanapata ajira kuliko hao wanao weka huko uswiss
 
hizi ndie zile thread ambazo Wapenda Nchi wa Lumumba hawaingizi mguu kuchangia..

c.c Ritz (i bet huyu naye yumo kwenye hili kundi), HAMY-D (Hamida,huyu kuna dalili kubwa ana chuki binafsi na Dr.Slaa na Mbowe),
EX-COP a.k.a CHRIS LUKOSI(kibaraka wa CC.M aliye kule ughaibuni,huyu ni kama Karatasi ya maluwatoni ya C.C.M) , UTAIFA KWANZA na the rest of your team.
 
Hapo ndio nachoka kabisa,hao maafisa wa polisi,wapelelezi,usalama wa taifa huwa kazi Yao nini?
Kila tukio likitokea utasikia mwenye ushahidi atuletee,hivi nyinyi kazi yenu kuletewa ushahidi na huko vyuoni kwenu mlikwenda kusomea nini ikiwa hamjui kutafuta ushahidi ambao ni kazi yenu,? Huu ujinga wa siasa kuchanganya na mambo ya msingi ndio unalimaliza hili taifa lisilo na mbele wa nyuma,
 
Kwahiyo ukishahojiwa basi yameisha?
 
Back
Top Bottom