Waliofeli Kidato cha Pili kuendelea na Masomo

Mabele Maduhu

Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
20
Reaction score
4
Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa [REMIDIAL CLASS].

 
duu kazi ipo chacha mkiambiwa mnakuza madudu wanajifanya wajua ndio tabu ya kuongozwa na mafailures..
 
Hiyo amri wapeleke kwenye shule zao ila seminarini hakuna kitu kama hicho! Umefeli rudi nyumbani ukafuge nguruwe wala hakuna kukariri!
 
Hiyo amri wapeleke kwenye shule zao ila seminarini hakuna kitu kama hicho! Umefeli rudi nyumbani ukafuge nguruwe wala hakuna kukariri!

Mkuu,

Sijui kama wengi wanakuelewa hapa. Athari iliyopo ni cream ya watu wa dini moja kusonga mbele alafu upande wa dini nyingine kulalamika. Watataka utawala kuzingatia udini badala ya uwezo wa mtu kishule.
Mthian wa form two aliutoa jk, wameona athari zake baada ya miaka 2 wakaulejesha, kumbe wamerudisha kiini macho tu!
 
matokeo mbona sijayasikia kutangazwa?
 
Kama hayo niya kweli nchi hii kuna viongozi walio kosa akili kabisa. Viongozi wa ccm ni mzigo mzito. Watakuwa wamefanya hivyo kwa sababu wanafunzi wamefeli sana
 
Napata taabu kuamini taarifa hii na kama ni kweli basi taifa litakuwa linaongozwa na watu wenye uendawazimu wa vipindi; mwezi ukiwa mchanga na mtoa maamuzi anatakiwa kufanya maamuzi basi anafanya maamuzi ya kiuendawazimu...au labda tunaongozwa na watu waliokuwa frustrated. Sitamaliza mengi kv taarifa yenyewe inaleta utata wa hapa na pale. Kwa mujibu wa gazeti hilo hilo la Mwananchi; hapa wanaendelea:

Kauli ya wizara


Akitolea ufafanuzi suala hilo, Profesa Mchome alisema, “Suala la wizara kuagiza wanafunzi wote waliofeli kuendelea na masomo ya kidato cha tatu mimi sijalisikia, ninachojua ni kwamba wapo watakaorudia.”


Alisema kuwa tayari wizara imeshapeleka taarifa za matokeo hayo na uamuzi wa Serikali katika kila kanda nchini. “Kila shule ina taarifa hizo. Wapo wanafunzi watakaorudia.”


So, kama ni kweli hakuna mwanafunzi atayerudia basi huyo profesa Mchome ni moja ya majanga ya kitaifa yaliyojificha kwenye taasisi mbalimbali nchini lakini hatujawafahamu kwavile tu huko waliko hakujawadhihirisha. Ni mtu asiyefaa hata kuwa mwalimu wa sekondari achilia mbali kuwa wa chuo kikuu.
 
watapewa remidial classes kwa darasa lipi? ie F2 au F3 maana hawa watu wana zaidi ya asilimi 72 ya content ya F1 na F2 hawajui !!

Sasa wanapoambiwa wapewe remidial hawaoni kuwa wanaongezewa mzigo mkubwa zaidi watu wenyewe ni slow leaners

Mwarobaini wa hawa watu ni kuwarudisha F2 basi !
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa serikali inaweza kurudi kwenye jambo la kipuuzi kiasi hiki.
Mkuu Mkirua, binafsi nimebaki hoi....hakika sitaki kuamini kama tumefikia huko!
 
Last edited by a moderator:
Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa[REMIDIAL CLASS].

Daaa! watoto wetu hadi leo walikaa tu nyumban wanasubiria matokeo wajue kama wanabak form 2 ama la. si wangesema tangia mwaka walipofanya mtihan? acha tu hii wizara apewe mulugo!
 

ntajie shule ya kiislam hata moja ambayo mkristo unaweza tia mgùu. nenda MUM kaone miujiza pale.
 
hili lichama sijui lini mungu atalipeleka kuzimu!tunapojaribu kuliondoa kwa kura wanachakachua..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…