Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Sote tunaamini serikali ya Tanzania ya sasa haiwezi ikasomesha wananchi wake wote, ijapokuwa ni haki ya wananchi kusomeshwa na serikali waliyoiweka madarakani. Serikali ya Tanzania ilianzisha bodi ya mikopo ili iweze kuwakopesha wanafunzi; gharama ambazo zinapaswa kurejeshwa wakiwa kazini. Bila shaka mpango ulikuwa kupata uwezo kurejesha mikopo hii ili iweze kusaidia wanafunzi wengine kusomeshwa, jambo ambalo halijafanikiwa mpaka sasa.
Ili kujenga ari ya wanafunzi kujituma na kufanya vizuri katika mitihani yao, serikali ya Tanzania ingekuwa ikiwasomesha bure wanafunzi wenye kiwango kizuri cha ufaulu (mfano wanafunzi wote wenye division one). Na wale wasiokuwa na ufaulu mkubwa waweze kupata mkopo kupitia bodi husika.