Waliochota Pesa ESCROW Stanbic hawa hapa

Sijanufaika sana na taarifa yako, weka mambo hadharani, kama huna hakika subiri, ukipakua chakula kibichi hakitalika, kama unadhani ukimtaja mtu wakati huna uhakika utapata matatizo, bora ukae kimya na kusubiri. Tunataka mwandishi anayejiamini na kusema Chenge alipewa bilioni moja la milioni mia sita na ukweli ukawa ndiyo huo. Una uhakika leta majina, huna uhakika kaa kimya, zama za uwazi na ukweli.
 


Pole naona ulilala usingizi wakati nilishaleta mada iliyomtaja mhusika mada kama ifuatavyo: Mke wa Prosper Mbena (wa Ikulu) Alichukua TZS 2 Billion za ESCROW


Nimekusaidia kuonyesha swali lako lilishajibiwa kwa mada hiyo hapo juu, nini tatizo mdau?
 
magazeti ya bongo yakishaifulia yanakuwa km bongo fleva, na bongo movies,watakuja na vipande vya heading ili kuuza kwa jina la Investigative Journalism.
 
Hi ni nithamu ya uoga umetaja mengine ila kumtaja mke wa kigogo ni kupisha upelelezi kwani wengine hawapelelezwi
 
Mbowe na Lowassa tunataka majina ya waliochota pesa kupitia Standbic Bank issue ya Escorw-hapo tarehe 24/10/2015 jangwani!

Haiwezekani tumechoka kudanganywa!


CC Tumaini Makene aione Lowassa
 
Last edited by a moderator:
Magufuli hebu tutajie japo mmoja ili tuone kama kweli una dhamira ya dhati.
 
Double Standard, Roho Mbaya, Kuabudiana, Uzuzu, Ukatili Na Misamaha Koko
 
Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC. 😭 😭 😭
 
Mh. Mbowe wewe ni Mzalendo halisi..una uchungu mno na mali za nchi hii....ala kumbe majizi bado yanadunda mtaani hadi wa leo!! Hayakamatiki.
 
Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC. 😭 😭 😭
πŸ“Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…