WALIO JITOA C.C.J TUWACHUKULlEJE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WALIO JITOA C.C.J TUWACHUKULlEJE?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bujibuji, Jul 15, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,064
  Trophy Points: 280
  Mtikila alikomaa hadi akapata usajili wa kudumu.
  Subira na uvumilivu na ari ya kupambana ndizo zilipeleke D. P kusajiliwa.
  Hawa viongozi wa C . C. J waliojitoa, sidhani kama wana nia ya kudhati ya kuleta upinzani hapa nchini kwetu.
  Hawa ni waganga njaa, wenye uchu na uroho wa madaraka.
  Tuwakatae popote watakapoenda.
   
 2. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  wamegundua ccj hakina mwelekeo
   
 3. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  wanatafuta sehemu nyingine ya kuganga njaa zao
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siasa za Tanzania, bado sana ...
  Tuna safari ndefu mno ya kwenda, ili tupate wapinzani wa kweli.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hapo ndipo CCJ waliponichosha sana .
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CCJ ni tawi B la CCM
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tuwachukulie kwamba wanajua sana maana ya siasa za Bongo. Unadhani kama ungekuwa wewe mkuu ungefanyaje, kama Mtikila? Lengo la ccj labda halikuwa kupata publicity kama Mtikila? Mtikila ameachieve alichotaka - umaarufu. CCJ walitaka kuleta upinzani wa kweli wa kisayansi ambao ulishaona CCM walichanganyikiwa kuona wanazidiwa kete, wakatumia nguvu waliyonayo kuzima progress za CCJ ambao walikwishajizolea ufahamu wa watu kibao wa kuwapo kwao na matumaini ya kisiasa.

  Mwenyekiti wa Chadema alisema openly kwamba siasa ni opportunistic game, hata ukiwa angani unaweza kubadili gear ili kuhakikisha kinaeleweka. Nakubaliana naye. Kama tungekuwa na siasa za kistaarabu ambazo kila mtu anapewa fulsa sawa na mizengwe inadhibitiwa kwa aliyemo na asiyekuwamo, siasa unazotaka tuzing'ang'anie zingefaa. Wamewasoma chadema wakaona angalau kuna lugha wanayoweza kuelewana, wasingeweza kuingia moja kwa moja kwa sababu ya tofauti zao fulani, lakini baada ya kuona wamewekewa nondo wasipite wanakloenda wakaona bora kupitia dirishani kama mlango umezibwa. Huko mbele unajuaje, labda wataendelea na harakati zao?

  SIasa za Afrika ni ngumu sana kwa sababu aliyepata hataki kutoka kwa nguvu zozote hata ikibidi kuua. Hiyo ndiyo Afrika yetu. Siwalaumu CCJ waliojiunga chadema, sijui wangejiunga wapi, maana kwa Tanzania bara chadema ndio angalau wanakubalika zaidi na ushiriki wao. CUF sawa, lakini Visiwani kwanza. UDP kanda ya ziwa kwanza, NCCR bado longolongo nyingi, Jogoo ni chama cha mtu mmoja mmoja, akisema mwenyekiti ni kwisha maneno. Ndio demokrasia yao.

  Ajabu iko wapi kwa walichofanya ccj kutafuta uwakilishi bungeni zaidi kupitia chadema ghafla ghafla? Mbona kina Mtemvu walitoka cuf wakanyaka post ccm chap chap? unamsikia siku hizi mwanasheria machachari aliyekuwa chadema akaingia ccm na kuwa mlinzi wao mara moja? sikumbuki jina - matatizo? Mashaka sielewi. Wengi tu walipohamia ccm walipewa ukuu wa wilaya, vyeo kibao..... Kwa nini isiwe vinginevyo kwa wengine?

  Mimi sina chama chochote kichwani wala mwilini mwangu, navichukulia vyama vyote ikiwemo ccm kwamba ni vyama vya kugangia njaa kwa kila anayeipiga vizuri hesabu ya kuingilia huko. Najua kwa hakika kwamba chama chochote kingekuwa madarakani kingedhibiti wengine wasizoe madaraka kama wafanyavyo ccm. Nyanya zote ni sawa tu, tofauti ni aliyezibeba.

  Siasa is not really a profession, it is a rough way of life ambayo ukiweza kuwadhibiti watu na akili zao basi wewe umewini. Kama mchezo wa kuigiza vile, ukijua watu wanataka kusikia nini ukakisema hicho umewapata. Ukiwaambia ukweli watu hao usitegemee kuwapata. Mwongo ndiye mtaalam wa siasa za kubadili maneno kila saa kufuatana na upepo.
  Mwanaume mkweli sana ni vigumu kupendwa na watu wengi, hata wengine wanashindwa kupata mke. Waongo wengi wanafanikiwa sana kwenye maeneo yoyote yale - kibiashara, kimaisha, nk. Let CCJ members maximize this opportunity of trial and error in their endevor to achieve their dreams. Nimependa walivyo sharp kufikiri. Kumwiga Mtikila maana yake wangeendelea kuzozana na Tendwa ambaye kashika mpini na nyuma yake kukiwako na dola zito lililoko tayari kummeza yeyote aliye kinyume nao. Vita anayeshinda ni yule mjanja. Retreating doesn't mean a surrender.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,064
  Trophy Points: 280
  Naona umejaribu kutetea hoja yako vizuri.
  Je si kweli kwamba ccj kiliundwa ili kwenda kuughilibu upinzani?
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Naamini CCJ walikuja na mbinu nzuri, ila wali-underestimate capacity ya CCM na agency zake.
  I thought walijipanga kwa kila mtego, wamejaa kwenye kamtego ka kamba laini!!!

  Halafu wamekuwa kimya, hawajasema wanachama wafanye nini!!! Top layer imesepa CHADEMA bila kusema nni kitafuata baada ya TEndwa kuwaTENDA!! CCJ mtuambie what is the way forward?
   
 10. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwisha kazi hao, tamaa za ulaji zinawasumbua. Hakuna chochote ni pumb......v... tu. Waende kutafuata vyeo matopeni. CHADEMA kuna watu walishajipanga iwapo watawaruhusu basi watakuwa wajinga. Walipaswa wajiunge na CHADEMA badala ya kuanzisha sisije? leo ndo wanajua CHADEMA inawafaa? Kombamwiko hao

  Wapi Mwana kjj
   
 11. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kupata upinzani wa kweli kwa kuwa Watanzania wengi hawana vyanzo vyao vya uchumi vinavyotosheleza mahitaji yao na familia zao. Wanaokuwa mstari wa mbele kunanzisha vyama pamoja na kujipambanua kama wapinzani, moyoni mwao wanawaza kupata ruzuku ili maisha yaweze kusonga mbele. Watu kama kina Keneth Matiba, Mwai Kibaki na wengineo waliokuwa wanapingana na Moi tayari wana vyanzo vya mapato vya kuwafanya
  maisha yaende mbele tofauti na kina Kyanabo.
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red, unamaanisha kuwa hao kina Kiyabo ni mende?
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Maneno yote haya ni sababu tu wameamua kujiunga na CHADEMA? we bujibuji ulitaka wajiunge na chama chako? i don't see any point to discuss.

  Nafikiri wewe mleta thread hii ndiyo una njaa zaidi kuliko hao unaowatuhumu tena bila hata kuwa na point za msingi. Wachangiaji wengi hawajui upepo wa SIASA, hasa katika nchi za kiafrika, inakuwa kazi kweli kweli kueleweshana.
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Nafikiri wachangiaji wengi hapa watakusoma hasa kwenye hii pointi yako - good.
   
 15. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  CCJ pia ni strategic - hawawezi kukaa ktrk njozi wakisubiri huruma ya watawala wahusudu mafisadi.
   
 16. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Read between lines, I mean Kombamwiko, by the way what is so called MENDE and KINABO:pound:?
   
 17. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana mbinu nzuri za kisiasa naamini wataweza kusaidia chama,TUACHE WIVU, TAKE EXAMPLE OF KANU,PNU ODM.
   
 18. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Bujibuji,

  Mimi nawapongeza sana kwa kusoma alama za nyakati. CCJ imeshapigwa stop, na itawachukua miaka kupata huo usajili wa kudumu, sasa wakae huko wanafanya nini wakati wameamua kufanya siasa, ni lazima watafute mahali pa ku-practice. Mimi ningewashangaa sana kama wangeenda ccm kwani huko hakuna mabadiliko yoyote.
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wiki iliyopita Mbunge wa Kawe kupitia CCM Mama Rita Mlaki alitangaza rasmi kuwa mwaka huu hatagombea tena ubunge wa jimbo la Kawe na hivyo umfanya mbunge wa Saba kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubunge mwaka huu.

  Leo kwenye kikao cha jioni cha Bunge nimeshituka kumsikia mama Mlaki akitangaza kuwa atarudi tena Bungeni iwapo umoja wa taasisi zisizokuwa za serikali NGO zitampitisha kama mgombea wake!

  Nimejiuliza Maswali kadhaa:
  Hivi taasisi zisizo za serikali NGO zina/zimepewa viti maalumu bungeni?
  Hivi mama alipotangaza kuachia ngazi bungeni na sasa anatangaza kurejea iwapo atapata nafasi inamaanisha alikuwa anaogopa kivumbi ktakachotokea?
  Ina maana alipokuwa anatangaza kujitoa kugombea Ubunge ilikuwa ni 'Nataka Sitaki' ama "Sizitaki Mbichi Hizi"?
  Maswali ni mengi kuliko majibu....
   
 20. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Anataka ubunge ila hataki kugombea!
   
Loading...