Walinzi wa Viongozi Wetu: Tahadhari inahitajika.......

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,789
470
Wadau, sina taarifa za ndani sana kuhusiana na uchunguzi au uhakiki wa misimamo/mitazamo au imani binafsi za walinzi mbalimbali wa viongozi wetu, whether toka TISS or wherever.....historia inaonyesha kwamba kuna viongozi ambao wamewahi kuuawa na watu waliopewa jukumu la kuwalinda, e.g Ghandhi, Kabila, na hili tukio lilinifanya kuandika thread hii, i.e, mauaji ya gavana wa Punjab, Salman Taseer, a very influential figure in Pakistani politics..mlinzi huyu, Malik Mumtaz Hussein Qadri, ameanzishiwa page ktk facebook na watu wanaoamini katika jambo alilofanya, gonga http://www.facebook.com/Malik.Mumtaz.Qadri?v=wall ...Naamini kama vyombo vya usalama vya Pakistani vipo makini, kuna uwezekano mkubwa wa kuwapata wahusika wengine, hasa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii na ku-single out walinzi au marafiki wa walinzi wenye muelekeo huo..je, kama misimamo yake ilikua inafahamika,halikua kosa kumpanga zamu ya kumlinda mtu ambae kauli zake za karibuni kabisa ni kinyume na mafundisho ya Mtume, gonga hapa http://www.bbc.co.uk/news/world-south-asia-12111831 ......au ulikua ni mkakati wa vyombo vya usalama kama ambavyo Marekani wamekua wakilalamika kwamba vinashirikiana na fundamentalists??

Anyway, ya juu hayahusiki sana, ni scenario tu...Concern yangu kubwa ktk hili ni usalama wa viongozi wetu hasa katika kipindi hiki ambapo mitazamo ya kidini na kisiasa imeanza kuonyesha nyufa katika Taifa letu lenye amani na mshikamano ulioachwa na baba wa taifa..Maswali yangu ni kama ifuatavyo...

1. Nani anawahakiki vijana wanaowalinda viongozi?

2.Vigezo gani vinatumika kuwapata?

3.Maisha gani wanaishi?

4.Mambo gani wanaruhusiwa kufanya na yepi hawaruhusiwi?

5.Uangalizi upi wanapewa?

6.........

Naomba wahusika, ambao naamini ni watu makini sana kwa majukumu waliyonayo, watafakari na kuongeza mengine katika haya yanayotokea...
 
vijana wenyewe wamechoka...ngoja na hapa kwetu yatatokea maana kwa hali ninayoiona..mmhhhh!!!
 
Ni kweli kabisa,

tena kuwauwa sio lazima kuwapiga risasi. Wanaweza kulishwa sumu pia. Ni vyema hawa viongozi wakawa makini sana katika vyakula wanavyokula au vinywaji wanavokunywa. Kuna kundi la watu siku hizi wanalipwa kwa ajili ya kufanya mauaji ya viongozi au watu maashuhuri kwa kuwatengesha sumu za kuwaua taratibu i.e. slow dying poison ambayo inaweza kuchuka hata wiki nzima kumuangamiza mtu moja kwa moja...! Akina Kolimba na Prof. Malima waliondolewa hivi hivi...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom