Walinzi wa bugando hospital na double standard katika utendaji

OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
693
300
Wiki iliyopita nilipata fursa ya kutembelea Bugando hospital kwa shughuli binafsi.Nilishangazwa kwa kitendo cha walinzi wa Bugando kukataa kuruhusu wanawake waliovaa masuluari ama kuingia kupata matibabu au wale wanaokuja kuona wagonjwa,siku ya pili nilikaa jirani na mlango wa kuingia hospitali na kushitushwa na vituko nilivyoona vikifanywa na walinzi hao,alisimama mlinzi mmoja ambaye nadhani ni incharge lakini kazi yake ni kukagua wanawake wanaoingia hospitali,mara '' wewe mama ondoka uruhusiwi kuingia umevaa suruali.mara wewe ondoka nguo yako ni fupi,na wewe mama nguo yako inapitisha mwanga tunaona under skirt uruhusiwi kuingia etc.Kwa kweli nilisikitishwa sana na udhalilishaji huu kwa wanawake hasa ukizingatia wengine ni wagonjwa waliotoka mbali kuja kutibiwa kwa gaharama kubwa na pengine maisha yao yako hatarini,japo mimi sio mtaalamu wa medicine lakini nadhani sio sahii kabisa kumpa mlinzi madaraka ya kumrudisha mgomjwa nyumbani heti kisa kavaa nguo fupi,pia lugha wanayotumia na sauti mbele ya kadamnasi sio sahii kabisa.Pia wakati wa ndugu kutembelea wagonjwa na kuwapelekea chakula ndio usiseme,walinzi hao utuna gatini na kudemonstrate power yao,wanarudisha wakina mama waliobeba vikapu vya vyakula na pengine madawa waliyonunulia wagonjwa wao bila kujali athali zake kwa mgonjwa atakayekosa chakula siku hiyo na faraja ya kutembelewa ambayo ni psychothelapy.
Utafiti wangu haukuishia hapo niliingia hadi hospitali ambapo nilipata mshituko kukuta ma doctor wa kike wamevaa suruali hizo hizo wasizopenda walinzi,ma nesi ndio balaa kwa vimini na mambo memngine ya aina hiyo.Sasa nikajiuliza kama hiyo ni sheria ya kidini na kimaadili katika hospitali hiyo kwanini iwe kwa wagonjwa na ndugu zao tu?kwanini na ma dokta na ma nesi waliovaa suruali na vimini wasizuiliwe na walinzi kuingia hospitali?je hii sio double standard na unyanyasaji?
MWISHO NAOMBA UONGOZI WA BUGANDO UELEZE UMMA KAMA HAYO MAELEKEZO WALIWAPA WAO HAO WALINZI AU NI SHERIA ZA HIYO KAMPUNI YA ULINZI.NA KAMA NI UTARATIBU WA HOSPITALI UNA LENGO GANI?NA KWANINI MANESI NA MADOKTA WA KIKE WASIHUSISHWE KWENYE HUU UTARATIBU?Vinginevyo huu ni utaratibu kandamizi na inabidi uachwe mara moja.
 
Back
Top Bottom