Walinzi wa Amana Hospitali ni tatizo kubwa sana!

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Manyanyaso Amana Hospitali

Sio mahala pake lkn kuna wana habari humu, Viongozi wa Serikali, Vyama mbalimbali, wanaharakati, saidieni kupata ukweli wa haya manyanyaso. Wana habari kupitia kalamu zenu wakubwa wajue, tatizo litafutiwe ufumbuzi. Inauma, inaumiza!

Mheshimiwa RC, sikia kilio cha watu wako ndani ya mkoa wako wa Dar Es Salaam! Wananchi tunateseka, tunateswa, tunanyanyaswa na Walinzi wa Hospitali ya Amana!

Walinzi wamekuwa zaidi ya madaktari, wauguzi na viongozi wa Hospitali ya Amana, anachokiamua mlinzi ndicho kinasimama, rushwa wanaiweka mbele kuliko utu!

Nimefanya uchunguzi kidogo kuhusu walinzi wa Amana kwa baadhi ya Madaktari wa hospitali hiyo, wamekiri walinzi hao ni tatizo, kikwazo kwa wagonjwa, ndugu wa wagonjwa na wao wenyewe madaktari hawaheshimiwi na walinzi hao, pale wanapotoa ushauri wao kwa walinzi hao wamekuwa wakipuuzwa, kudharauliwa na kudhalilishwa mbele ya wagonjwa na ndugu wa wagonjwa! Wameomba wasaidiwe yawepo mabadiliko! "Tukipata wa kuwalipua tukapata mabadiliko tutashukuru, tunataka mabadiliko"

Jana Feb 21, 2017 binafsi ilinitokea mara mbili. Mosi nilifika asubuhi nikiwa nimechelewa muda wa kuwaona wagonjwa saa 12 asubuhi baada ya kuanzia kazini kuajibika kwa ajili ya ujenzi wa Taifa. Nilifika Hospitalini hapo saa 2.05 asubuhi. Mama yangu ni mgonjwa alihitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku hiyo ya jana. Daktari aliyekuwa anamfanyia aliomba nifike asubuhi hiyo ili kabla ya kumfanyia tushauriane jambo. Mimi ndiye pekee namuuguza mgonjwa na Dada yangu ambaye zaidi ya kukaa kwa shida tu na mgonjwa hana lolote analoweza kulifanya kwa umri wake mkubwa!

Nilipofika nilifanikiwa kufika wodini IPPA, VIP room 4 alipolazwa mama yangu mzazi, wakati huo Daktari alikuwa katika majukumu mengine, akanambia katika simu nimsubiri kidogo. Wakati huo Dada anayemwangalia mgonjwa alikuwa hajanywa chai na hata chakula cha usiku wa kuamkia siku hiyo ya jana hakula kutokana na hali mbaya aliyokuwanayo mgonjwa iliyofanya nishindwe kumtafutia chakula! Alilala na njaa!

Pamoja na kwamba muda wa kuwaona wagonjwa ulikuwa umepita, nilimueleza nesi kuhusu appointment yangu na Daktari, na nikamuomba niende kumchukulia Dada chai katika Mgahawa uliopo eneo la Hospitali.

Wakati narudi wodini nikiwa na chai, mlinzi mmoja nyuma yangu hatua chache kuingia wodini aliniita nikasimama. Alipofika mazungumzo yakawa hivi?

Mlinzi: Unakwenda wapi?
Mimi: Wodini IPPA kumpelekea mgonjwa chakula ajala tangu jana.
Mlinzi: Sio muda wa kupeleka chakula, rudi uje saa 6 mchana
Mimi: Samahani mlinzi, mgonjwa hajala tangu jana, naomba uniruhusu nimpelekee chakula asife na njaa, isitoshe Daktari wake kaniomba nimsubiri kuna jambo kuhusu mgonjwa anahitaji kunambia.
Mlinzi: Nimesema rudi uje saa 6 muda wa kuleta chakula.
Mimi: Naomba basi unipelekee hii chai, Daktari nitamtafuta kwa simu.
Mlinzi: Haturuhusiwi, vinginevyo nipe sh 10,000 nikupelekee.
Mimi: Sina hiyo pesa naomba unisaidie.
Mlinzi: Nimekuvumilia sana naona hunielewi, naomba uondoke hapa vinginevyo nitatumia nguvu kukuondoa hapa.
Mimi: Mbona hapa siko wodini, nakuomba wewe unisaidie umekataa na hapa nimesimama tu siendi wodini kwa nini utumie nguvu kuniondoa? Hawa waliokaa hapa chini mbona huwaondoi?
Mlinzi: Hawa wanaenda kwa Daktari wa mifupa, ondoka hapa! Akaanza kunisukuma, chai ikawa inamwagika mmoja wa akina mama waliokaa pale chini ambao hawakuwa na dalili ya kwenda kwa Daktari wa mifupa kama alivyodai mlinzi, kwa hisia zangu kuna mtu walikuwa wakimsubiri akanionea huruma akanambia"Weka chini chupa ya chai, chai inamwagika na inaweza kuvunjika" Nikafanya hivyo.
Mimi: Naomba usinisukume, tafadhali sana, sioni sababu kwa nini unanisukuma kiasi hiki huku ni kuninyanyasa na sidhani umeajiriwa hapa kusukuma watu. Katika kujitetea nikamwambia, "Ukiendelea kunisukuma, tutapigana sasa hivi, kwani ni kuninyanyasa" Alimuita Askari mwingine ambaye nadhani ni boss wake, naye ikiwa hivi:
Mlinzi boss: Kuna nini?
Mimi: Nikamueleza yote niliyomwambia mlinzi wa awali tena kwa unyenyekevu sana nikidhani boss ni boss tu ana hekima na busara kama boss lakini hakuwa tofauti na yule wa kwanza, wakashirikiana sasa kunisukuma! Niliondoka huku tukiendelea kujibizana!
Mlinzi boss: Bahati yako ungetutambua kama ungeendelea kubisha, tungekupiga hapa uwe mfano kwa wengine, mtu mwenyewe mwili wa kupigwa huna, siyo mzima wewe utakuwa na Ukimwi kapime! Jana yake nilikuwa nimepima Ukimwi, ni kawaida yangu kupima afya. Sikuwa na uhitaji wa kwenda kuchukua majibu nikalazimika kwenda kuyachukua. Ninayo, ni mazuri, niko salama!
Mimi: Jaribu kunipiga uone kama sijakuvunja miguu! Wakati huo nikawa nimefika katika Mgahawa eneo la Hospitali! Watu wengi walinionea huruma, mama mmoja akachukua hiyo chai akaipeleka.
Daktari sikuwasiliana naye tena hadi alipomaliza upasuaji nikamfahamisha nilivyozuiwa na walinzi na kwakuwa kulikuwa na jambo la kunishauri akaja nilipokuwa mgahawani kunipa maelezo nini kifanyike kwasababu walinzi hawataki niingie wodini!

Mama alitoka theatre Majira ya saa 7, alisinzia mpaka saa 12 alipozinduka! Nikiwa wodini wakati wa masaa ya kuwaona wagonjwa saa 11 jioni, nikashauriana na Sister wa zamu chakula kipi kinamfaa mgonjwa ili akizinduka aweze kula kwani tangu jana yake alikuwa hajala kwa ajili ya maandalizi ya upasuaji.

Sister alinambia aina ya chakula kinachofaa kwa mgonjwa, nikampigia simu muandaaji ili amletee mgonjwa chakula walichoshauri wataalam.

Saa 1.17 jioni aliyeleta chakula akanipigia simu akanambia walinzi wamezuia kuingia. Nikaongea na sister wa zamu anisaidie kwenda kukichukuwa hicho chakula ili mgonjwa aweze kula! Wakati huo Mimi nilikuwa wodini kwani mama bado alikuwa katika hali yakutokuwa na fahamu vizuri, hakutaka niondoke!

Sister alikwenda lakini akarudi bila chakula akasema walinzi wamesema chakula hakiingii kwasababu wamejibiwa vibaya!

Niliwasiliana na supervisor wa zamu wa wakati huo naye kajaribu lakini ikashindikana. Nikaomba namba ya Mganga Mkuu nikaambiwa na supervisor kwamba haruhusiwi kutoa namba ya simu ya Mganga Mkuu, nikaamua kumpigia RAS simu haikuwa hewani. Nikampigia Afisa mmoja ofisi ya RAS ambaye alinisaidia kwa kunipatia namba ya Mganga Mkuu. Nilimpigia Mganga Mkuu, hakupokea, baadaye akinitumie sms kwamba yuko kikaoni.

Niliamua kumpigia DC Ilala naye simu haikuwa na majibu, nikalazimika kukupigia wewelakini simu haikupokelewa! Nilikata tamaa, nikamuachia Mungu lolote atakaloliamua na liwe! Kama mama atakufa kwa kukosa chakula ambacho kiko getini kinazuiwa na walinzi, mapenzi yake yatimizwe!

Wakati natafakari yote hayo akanipigia simu Katibu wa Mbunge wa Segerea, ambaye kabla ya kueleza yake nikamuomba anitumie namba ya Mheshimiwa Mbunge. Alinitumia, nikampigia, akasema ngoja alishughulikie!

Yule aliyekuwa na chakula akaamua kujiongeza, akampa chakula mtu mwingine ambaye naye alisema alifukuzwa mara na walinzi hao wakimwambia, "Hata mkibadili watu zaidi ya 10, chakula hakipiti hapa" Baadaye kwenye saa 5. 28 hivi walivyoona watu wanahangaika kupiga simu wakaruhusu chakula hicho kuingia ambacho hata mgonjwa hakula, tayari alilala! Nilimlazimisha sana, akala kidogo mno kwasababu kalazimishwa!

Kabla ya chakula kuletwa Supervisor alikuja wodini na mlinzi Mkuu ambaye tayari asubuhi alishanitukana nina Ukimwi eti tushauriane namna ya chakula kitakavyoingizwa humo wodini! Kwakweli sikuwa na muda wa mashauriano yoyote, kwani nilishindwa kuelewa ni dhambi gani imetendwa kiasi cha kumuadhibu mama yangu kukosa chakula!

Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, walinzi hao wa Amana ni tatizo Hospitalini hapo, fuatilia uwaokoe watu wako. Ni wengi wanafanyiwa mambo makubwa ya ajabu! Mpaka madaktari wanaoomba mabadiliko ya walinzi hao, kwani nao wanakiona cha moto kwa walinzi hao ambao wamekosa hekima na huduma nzuri eneo kama hilo la Hospitali!

Mungu ni mwema, azidi kukulinda, kukuongoza na kukupigania katika kutekeleza kikamilifu majukumu ya kazi yako hasa kwa wanyonge tunanyanyaswa na kuonewa na wenye mamlaka kwa kuyatumia vibaya mamlaka waliyopewa kwa ajili ya watu!

Na Masau Bwire, mkazi wa Dar Es Salaam
 
Duuuhhh...Pole sana mkuuu, tunalalamika kuwa watz hatupendwi nje ya Tz kumbe sisi kwa sisi hatupendani ndani ya Tz
 
Sometimes walinzi wanakuwa kama wamepungukiwa na akili hiv. Ama wanasumbuliwa na tatizo la inferiority complex kwa hiyo wanajaribu kuwa wasumbufu ili waonekane wapo juu.

Hao walinzi hawastahili kuwepo hapo,, maaana huwezi kuhatarisha uhai wa mtu kwa sababu za kijinga kwamba nimeongeleshwa vibaya.

Nimeumia sana kwa maelezo yako. Nina imani viongozi wanaowasimamia watachukua hatua stahiki inayofanana na matendo yao.
 
Lugalo ya kambini jeshini ndani ile ndo hospitali nzuri unakaa na mgnjwa wako mda mwingi ata ukitaka kulala naye karibu ukimuangalia unaruhusiwa.. hawana shida wale.. huduma nzuri, chakula mgnjwa anapata mda wowote, na uzuri hata raia wanaruhusiwa na wanawapokea na huduma zote mule ndani Kama unahudumiwa na Daktari Raia hamna mikwala ya kijinga wala manyanyaso..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa yaliyokukuta. Wakati mwingine wanaoangalia wagonjwa huwa wanazingua..kwanza hawafuati muda pili wanakuja nyomi kiasi amacho nadaktari wanashindwa kutoa huduma kwa wagonjwa wengine..
 
Wewe ndiyo tatizo na mnafiki. Mgonjwa anayefanyiwa upasuaji hapewi chakula chochote siku ya upasuaji mpaka upasuaji UKamilike. Hospital imeweka utaratibu wa Chakula muda mwingine ni wa madaktari kushughulikia wagonjwa sasa mama yangu kavuliwa nguo anaoshwa madonda ya makalioni unataka na wewe uwepo wodini!!!!!! Pumbavu Kabisa.Mlinzi kutumia nguvu ni sehemu yake ya utekelezaji wa kazi ukigoma hata kipigo unakula na kesi juu kufanya fujo hopitali, Acha dharau wewe tumbili kisa unafahamiana na viongozi. Wewe kila kipengele unaeleza kuwa unaomba sasa aliyekuambia kuwa kila ombi linakubalika ni Nani?. Utapata tabu sana kwa wajeda wa suma jkt maana wao wanatekeleza maelekezo na sheria zilizopo hivyo wewe unakwenda kinyume na Sheria za Hospitali halafu unaongeza uongo Eti wanataka rushwa!!!!!? Aliyekuambia rushwa inaombwa hadharani hivyo ni nani? Maana maelezo yako yasomeka kulikuwa kuna wagonjwa wengi wanakwenda kumuona Daktari wa mifupa walikaa na Mlinzi. Kwa ufupi wewe ni muongo kabisa umekwenda hospitalini hapo kufanya fujo tu maana hakuna mahali ulipoonewa bali wewe ulivunja sheria za hospitali hiyo. Ukiendelea na hiyo tabia yako ya hovyo utajikuta upo mahabusu na umechezea kipigo cha mbwa koko. Walinzi waliopo hapo moja kazi yao ni kushughulika na mimbumbumbu kama wewe. Ningekuwa namjua mlinzi ningefika hapo Amana hospital nimpe hela apige heniken bariiiiidi. Maana kawakilisha vizuri kampuni yake.

Jitu limekariri anavyomnyanyasa mlinzi wake nyumbani na kutukuzwa kama mungu anafikiri kila sehemu atatukuzwa Ndugu atakufa bure fuata utaratibu short kati na uzembe wako ni hatari Kwa usalama wako maana kuna walinzi wengine Hawakukawizi utapigwa ufe usije ukafikiri watu wanaopigwa na kufa wanamapembe ni kama wewe na uchunge sana mdomo wako maana utakugharimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes walinzi wanakuwa kama wamepungukiwa na akili hiv. Ama wanasumbuliwa na tatizo la inferiority complex kwa hiyo wanajaribu kuwa wasumbufu ili waonekane wapo juu.

Hao walinzi hawastahili kuwepo hapo,, maaana huwezi kuhatarisha uhai wa mtu kwa sababu za kijinga kwamba nimeongeleshwa vibaya.

Nimeumia sana kwa maelezo yako. Nina imani viongozi wanaowasimamia watachukua hatua stahiki inayofanana na matendo yao.
Huyo mlinzi nae ni mgonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vizuri kia mtu apende kufuata utaratibu uliowekwa na ofisi yoyote.
Kama ni muda wa kuona wagonjwa ni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa mojabasi fima muda huo uliopangwa na ofisi hisika.
Wewe unakuja saa mbili na dakika tano,harafu unaanza kuhalalisha kuchelewa kwako. Operesheni anafanya daktari,sidhani kama na wewe ulitakiwa kuwepo muda wa operesheni.
Kuna mtu anakaa na mgonjwa wako. Wanaokaa na wagonjwa wanapewa vibali maalumu vya kukaa na wagonjwa.
Angeweza kutoka yeye mwenyewe na kuja nje kukutana na wewe na akaenda kunywa chai na kurudi wodini kwa kuwa ana kibali maalumu cha kukaa na mgonjwa ambacho walinzi wanakifahamu,wasingeleta usumbufu.
Heshimu ofisi ya mtu. Naye mlunzi akija ofisini kwako atafuata utaratibu wa ofisi yako bila kuhalalisha sababu za kuchelewa kwake kuja ofisini kwako.
Mengineyo ni wewe umeyaleta baada ya kumprovoke mlinzi.
Wito wa kila mtu kufuata utaratibu wa ofisi unayoenda,siyo ofisi yako ni ya muhimu sana kuliko ya mwengine.
Sjaona sababunya msingi ya KULALAMIKA KWAKO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom