Walimwengu dhidi ya binadamu!

Daraja2

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
249
295
Habari zenu wapendwa......!

Duniani kuna walimwengu wa aina 3:-

1.Mlimwengu anayemuunga mkono binadamu kwa mambo yote (mazuri au mabaya).
----Kwa mfano kuna mtu amekudhulumu na umefikia maamuzi ya kwenda kumtenganisha kichwa na kiwili-wili kwa shoka Ukimfuata mlimwengu huyu ushauri wake utakuwa "tekeleza tu mbona hakuna shida"

2.Mlimwengu anayepinga mambo yote liwe zuri au baya.
-----Kwa mfano una Mtaji mzuri tu na unataka kuanzisha biashara Ushauri wake utakuwa "Achana na biashara ndugu yangu akina MENGI wenyewe wanapata hasara"

3.Mlimwengu anayekuunga mkono kufanya jambo ambalo linamaslahi kwake binafsi tu bila kujali madhara yatakayo kupata mbeleni.
-----Mfano wa hili ni pale mtu kukubali kuidhinisha bidhaa feki kutumika uraiani kwa kupokea "mlungula"

----Au ndugu wa karibu kushinikiza wana ndoa kuachana kwa kuona kuna kitu (Mali/fedha) atapata mbeleni baada wa wahusika "kusambaratika"

Swali:-

1.mlimwengu yupi ni mzuri kuliko wote?

2.mlimwengu yupi ni mbaya kuliko wote?

Angalizo:-Hakuna jibu hapana.


Mbona malimwengu!!!!!!?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom