Ndugu yangu, nakwambia kazi ni kubwa mwaka huu. Watu wanakufa hospitalini na watoto watafeli mashuleni hadi wakome. Nani atakuwa na muda wa kufundisha kwa moyo katika hali hii? Me nikifika skonga nasaini kitabu cha mahudhurio natoa notsi kwa watoto wanaandika kisha naingia uswazi. Hiyo ndiyo maisha ya kuanzia kesho. Mshahara kweli hautoshi kunifanya nishinde shule kutwa nzima, wala sina muda wa CONSULTATION na wanafunzi, muda wangu mwingi lazima niutumie kwa kazi nje ya kufundisha, pengine maisha yanaweza kwenda kwa mtindo huo. Nawashauri waalimu wenzangu, tunaweza kufanya kazi nyingine nyingi sana nje ya kufundisha, lakini tukiwa waalimu na maisha mazuri yakapatikana. TUJARIBU, TUNAWEZA, NA TUTASONGA MBELE KIMAENDELEO.