Walimu; watumishi waliobeba baraka za taifa lolote

Walimu; watumishi waliobeba baraka za taifa lolote

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,904
Reaction score
3,145
Habarini Wana JF.
Kama Kati Yetu Ni Wafuatiliaji Wazuri Wa Maendeleo Ya Elimu Katika Jamii Ya Ulimwengu, Utaona Thamani Ya Wale Wenye Dhamana Na Taaluma Ya Kuelimisha Jamii (Walimu) Wanavyo Beba Sifa Mbali Mbali Kulingana Na Jamii Waliyopo.

Huwa Naamini 'By Default Ukiwa Mwalimu Wewe Ni Mtumishi Halali Wa MUNGU. Kama Mwanadamu Alipewa Mamlakha Ya Kuunda Serikali Na MUNGU Akabariki Basi Alimpa Pia Heshima Yule Aliyemkabidhi Zawadi Ya Uwezo Na Wito Wa Kustaarabisha Dunia kama Alivyosisitiza Kwenye Kitabu Kitakatifu Cha Biblia, Mithali 4:13.

Hakuna Jamii Inayoheshimu Walimu Na Ikawa Nyuma Kustaarabika, Jamii Yoyote Inayosikiliza Walimu Na Kujali Wito Wao Basi Jamii Hiyo Ina Baraka Kutoka Kwa MUNGU, Jamii Iliyo Nyuma Kuthamini Kazi Na Wito Wa Walimu Ipo Nyuma Kupokea Baraka.

Mwalimu Ni Mlezi, Kiini Cha Ustaarabu Katika Jamii, Chanzo Cha Mgawanyo Wa Maajukumu Kwenye Jamii, Njia Ya Kupitia Kufikia Malengo, Muongozo Wa Kuishi Kwenye Sheria Lakini Pia Ji Jalala La Lawama.

USHAURI KWA JAMII YANGU.[emoji4]

Naamini Kuna Kazi Kubwa Sana Ya Kuwawezesha Watumishi Hawa, Lakini Muendelezo Wa Lawama Zao Kila Kukicha Hauoneshi Dalili Nzuri Ya Kuthaminiwa, Jamii Yetu Inaotoa Thamani Kwa Wafanyakazi Kulingana Na Vitisho Vyao.

Endapo Daktari Hatimiziwi Hitaji Lake Leo, Akigoma Watu Hufa (Ndani Ya Muda Mfupi), Ma 'Engineer' Wakigoma Mifumo Ya Uzalishaji Hufifia. LAKINI je Vipi Kwa Mwalimu? Kuna Mtu Hufa? Kuna Viwanda Vinafungwa? Hapa Ndipo Jamii Haioneshwi Kutishwa Na Watu Hawa.

Lakini Yote Kwa Yote, Daktari Anayeacha Watu Kufa Kwa Maslahi Yake Binafsi Ni Tunda La Mwalimu Aliyeshindwa Kumfundisha Mwanafunzi Huyu 'UTU' Kwa Aidha Kwa Sababu Naye Alilimbikiziwa Majukumu, Au Hakuwa Na Mazingira Mazuri Au Hakuthaminiwa Pia.

Ni Kheri Walimu Wagome Tuone, Kuliko Kuridhia Kuendelea Na Kazi Kumbe Hawafanyi Lolote, Yaani Watoto Wa Watu Wanahudhuria Tuu Ndani Ya Majengo, Pia Naishauri Jamii Yangu, Ithamini Nafasi Aliyekuwa Nayo Mtumishi Huyu Anayefuata Baada Ya Mzazi, Wasisikilize 'KASHFA' kutoka Kwa Wanasiasa Kwenda Kwa Walimu.

All In All, Basi Tusimfanye Mtumishi Huyu Kuichukia Kazi Yake, Mwisho Wa Siku Ni Kama Hivi Tunapata PHD's Zisizokuwa Na Msaada Bali Kuturudisha Nyuma.

Heri Kwenu.[emoji5]
 
Walimu na waheshimiwe,wathaminiwe&wasikilizwe mungu bariki walimu wote
 
kikwete aliwafanyia ustaarabu,mkaishia kumtusi na migomo kibao.
awamu hii atakaeshindwa kazi aache,lazaro mtoza ushuru hajaribiwi,wanaotaka kugoma wagome,watajua maana ya hapa kazi tu.
Hakuna Kiongozi Atayekuja Timiza Matakwa Yote.

Bora Nani, Kati Ya Yule Aliyepokea Malalamiko Na Akatimiza Kisha Kurudisha Watu Kazini Wakiendelea Na Majukumu Yao Kawaida?

Au,

Yule Anayewafanya Kuicchukia Kazi Yao Kisha Kuwafanya Kutimiza Tuu Jukumu Lao Bila Kulea Watoto?

Na Ndio Mana Sifa Nzuri Ya Uongozi Ni Hekima Yako Wakati Wa Maamuzi, Sio Kujikweza Kwa Sababu Ya Cheo UlichoNacho, Huyo Unayemuita Lazaro Mtoza Ushuru Atayaona Haya Matunda Baada Ya Miaka Kadhaa.

Nakuahidi; Wafukuzwe Na Kuja Wengine, Wabadilishwe Hata Mara Ngapi, Watishwe Ila Yeyote Anayefanya Kazi Ya Wito Hatishiki Na Pesa Ila Mazingira Ya Kutolea Huduma.

Usidhani, Padre, Sheikh Na Ma 'Sista' Huangalia Sana Pesa, Ila Ni Namna Watu Wake Wanavyomthamini, Ni Sawa Na Wito Wa Kumjenga Mtu (Ualimu).
 
aliekua na hekima mliishia kumuita dhaifu,lazaro mtoza ushuru hana huo mda wa kusikiliza hekima,hapangiwi.
kama unategemea ufaulu utashuka hilo sahau,mitihani inatungwa kisayansi.
hakuna kiongozi atayekuja kutimiza matakwa yote,matakwa yenu si kipaumbele cha lazaro mtoza ushuru.
awamu iliyopita mlijikweza sana,sasa ni mda wa kuisoma namba,and lazaro doesnt care hizo baraka mlizobeba cause hazimsaidii chochote.
Vizuri[emoji4] [emoji4] .
 
Bila kuwabariki waalimu kwa maslahi mazuri na heshima, tusahau habari za kujikwamua kimaendeleo!
 
Back
Top Bottom