Walimu wamethubutu

msnajo

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
3,066
1,136
Wakuu salaam,
Taarifa kutoka Wilayani Ujiji (Kigoma), walimu wapya wamewafungia ofisini wakuu wa idara kwa masaa kadhaa. Sababu kubwa ni kutokulipwa mishahara yao ya February.

My Take.
Mbuyu ulianza kama mchicha! Huu mlolongo wa matukio ya namna hii ni ishara kwamba ukombozi wa kweli haupo mbali. Nashangaa baadhi ya watu kudai kuna mahusiano na siasa. Mfano mgomo wa madaktari, wapo wanaosema kiini cha tatizo ni shinikizo la kisiasa! Swali la kujiuliza,, je hawastaili kutimiziwa madai yao? Na je hawa walimu nao ni siasa? Hii serikali mbona inafanyia mzahaha maisha ya watu? Hawa walimu wale nini, au watajikimu namna gani? Kuna kiongozi alijibu, kutokulipwa hawa walimu, eti majina yalichelewa kupelekwa hazina!! Hapa hakuna umakini wowote kiutendaji!
Wito wangu kwa watendaji wenye dhamana, tafadhali acheni uzembe. Mnafanya ofisi kama mali yenu binafsi! Mnaiangusha serikali hata pale inapokuwa na nia thabiti ya kuleta maendeleo.. Fikiria waziri anafanya madudu anakataa kujiuzulu, kama sio kufanya ofisi mali yake ni nini? Kuna maslahi gani ambayo unayapata kama kiongozi kwa gharama za uhai wa watu?

Wakuu nawasilisha tujadili.
 
Walimu wa sekondari tofauti na walimu wa msingi inabidi waelewe kwamba idadi yao inakuwa kwa wingi hasa kutoka university mbalimbali hawana woga wa ndiyo mzee tofauti na msingi huwa na woga wakiwaona maafisa elimu kata tu kama miungu mtu.

Na wanapomwana DEO husi kama vile wamevamiwa na simba.hivyo watawala wasitegemee tena kuabudiwa na walimu wa
sekondari ambao bado vijana na bado wana option kibao kwani hawaoni hatari ya kuacha kazi na kutafuta kungine.
 
Wakuu salaam,
Taarifa kutoka Wilayani Ujiji (Kigoma), walimu wapya wamewafungia ofisini wakuu wa idara kwa masaa kadhaa. Sababu kubwa ni kutokulipwa mishahara yao ya February.

My Take.
Mbuyu ulianza kama mchicha! Huu mlolongo wa matukio ya namna hii ni ishara kwamba ukombozi wa kweli haupo mbali. Nashangaa baadhi ya watu kudai kuna mahusiano na siasa. Mfano mgomo wa madaktari, wapo wanaosema kiini cha tatizo ni shinikizo la kisiasa! Swali la kujiuliza,, je hawastaili kutimiziwa madai yao? Na je hawa walimu nao ni siasa? Hii serikali mbona inafanyia mzahaha maisha ya watu? Hawa walimu wale nini, au watajikimu namna gani? Kuna kiongozi alijibu, kutokulipwa hawa walimu, eti majina yalichelewa kupelekwa hazina!! Hapa hakuna umakini wowote kiutendaji!
Wito wangu kwa watendaji wenye dhamana, tafadhali acheni uzembe. Mnafanya ofisi kama mali yenu binafsi! Mnaiangusha serikali hata pale inapokuwa na nia thabiti ya kuleta maendeleo.. Fikiria waziri anafanya madudu anakataa kujiuzulu, kama sio kufanya ofisi mali yake ni nini? Kuna maslahi gani ambayo unayapata kama kiongozi kwa gharama za uhai wa watu?

Wakuu nawasilisha tujadili.

Kwani siasa ni nini?
Kila kitu ni siasa.Isitoshe mtu anafanya kazi in exchange for a salary/remuneration.Kwanini wasidai haki yao?
 
Tunashukuru kama Wamethubutu, Wameweza na sasa tunawataka Wasonge mbele, maana wamelala mno hawa walimu ndiyo maana wananyimwa hata haki zao za msingi
 
Kwani siasa ni nini?
Kila kitu ni siasa.Isitoshe mtu anafanya kazi in exchange for a salary/remuneration.Kwanini wasidai haki yao?

Hoja yako ni ipi hapo sasa? Sijakuelewa unalalamika au unanilaumu kwa kuleta hii mada?
 
Kama wameweza basi ni jambo la heri tena ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine,watendaji wengi katika nchi hii wamejisahau kiasi kwamba wanaona wao tu ndio wenye haki ya kupata malipo stahili ilhali wenzao wanapata shida.
Tunakoelekea nchi hii haitakalika kama mambo haya ya kuzembea na kudharau haki za watu yataendelea
 
Walimu ni kama mishipa ya damu katika mwili wa mwanadamu, na kwa ccm wanawategemea walimu katika ushindi wao wa kupiga kura kwakuwa wanakuwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura na wanatumia advantage ya wanavijiji wengi wasiojua kusoma kuwapigishia kura kwa ccm sasa kama wataendelea kugundua uovu wa ccm itakua jambo bora
 
Walimu wapya ambao hawajalipwa stahiki zao na mshahara wa mwezi wa pili wamemfungia mkurugenzi ofsini.sakata ili lilianza ijumaa iliyopita baada ya walimu hawa kudai kilichochao.kuanzia jtatu wamejikusanya toka kwenye vituo vyao na kushinda bomani hadi kieleweke.jana walipewa ahad ya kulipwa ijumaa hii.walimu hawa waliamua wajibanze chumba kimoja<chumba watu 5 guest house kama wasomali> ile leo wapambane na mkurugenzi.asubuhi kaendeleza adith za ijumaa,ndipo walifanya kikao na kumwambia kuwa watalala nae ofisini kwake.saa 10 wamepiga lock ofsi yeye akiwa ndani. Sasa hivi ninapoandika ujumbe huu,walimu wako wanalipwa mishahara na stahiki nyingine.nawapongeza wale walimu walioonyesha ungangali hadi wamelipwa.
 
I see!!!safi sana,,,,ila nimeipenda sana ile staili ya kulala kama wasomali vile!
 
safari ijayo wakicheleweshewa wamfungie mlango wammwagie maji ya upu.pu na viboko vya kutosha, itakua fundisho kwake na wengine wenye tabia za kukumbatia mishahara ya watu
 
Back
Top Bottom