Walimu waliokimbia ushirikina watakiwa kurudi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Walimu waliokimbia ushirikina watakiwa kurudi


na Moses Ng'wat, Mbozi


amka2.gif
WAKATI serikali ikiwataka walimu 12 wa Shule ya Msingi Chindi, wilayani hapa kurudi kazini kwa maelezo kuwa matatizo ya kufanyiwa ushirikina yamemalizika, imemuondoa shuleni hapo mwalimu aliyetajwa kushiriki katika vitendo hivyo. Wiki iliyopita kiongozi wa mila wa Wanyamwanga, Chifu Chipwasi Makandi Mkoma wa sita, aliwataja hadharani watu watatu akiwamo mwalimu huyo kuwa ndio wahusika wa kufanya vitendo hivyo vilivyosababisha walimu hao kuacha kazi kwa hofu ya usalama wa maisha yao.
Hatua hiyo ya serikali kuwarudisha kazini walimu hao ilifikiwa juzi, katika mkutano mkubwa wa maombezi kwa ajili ya kukemea vitendo hivyo uliokuwa chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gabriel Kimolo na kuhudhuriwa na wananchi wa Kata ya Msangano na viongozi wa halmashauri ya wilaya.
“Shule zitakapofunguliwa Jumatatu ijayo, naomba walimu wote 12 wawe wamerudi na kuanza kazi, isipokuwa mwalimu mmoja ambaye ni miongoni mwa watu waliotajwa kushiriki mchezo mchafu wa kuwasumbua watumishi wetu,” alisikika akisema Kimolo.
Hata hivyo, Kimolo hakuweza kufafanua wapi watampeleka mwalimu huyo aliyetajwa kuwafanyia wenzake ushirikina na kusababisha adha kubwa katika shule hiyo, wananchi na serikali kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Levson Chilewa, alisema mwalimu aliyetajwa kuhusika na vitendo hivyo hatarejea tena kufanya kazi shuleni hapo na kwamba kuna utaratibu unafanyika wa kuona ataendeleaje na kazi mahala pengine.
 
Back
Top Bottom