Walimu walioghushi wapelekwa kwa DPP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu walioghushi wapelekwa kwa DPP

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,389
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  HAYA MAJITU MAPUZI KWELI KUNA MAJINA YAMEKUTWA ZAIDI YA 20,000 YA WALIMU FEKI NA YAMEANDALIWA NA WATUMISHI WA WIZARA SASA HAWA NDIO WANAOONEKANA KAZI KWELI KWELI..WAZIRI TUJULISHE YALE MAJINA FEKI MLIOYAGAWIA WATU AMBAO WENGINE WAMEKUTWA WAMEKUFA YAKO PESA ZIKO WAPI NA WATUHUMIWA WIZARANI WAMEPEWA ADHABU GANI????
  Walimu walioghushi wapelekwa kwa DPP  WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, amesema majina ya walimu wanaotuhumiwa kughushi madai mbalimbali itakabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), wachukuliwe hatua za kisheria.

  Profesa Maghembe pia amesema serikali haitasita kuwalipa mara moja walimu wanaodhani kuwa wamepunjwa madai ya madeni yao na walistahili kulipwa zaidi baada ya kuwasilisha nyaraka zao halali.

  Waziri alisema hayo mkoani hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi baada ya kuzindua rasmi wiki ya maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.

  Profesa Maghembe alisema udanganyifu katika kuwasilisha madai, ni kosa la jinai na kwamba waliojihusisha, wizara itakabidhi majina yao kwa DPP wafikishwe mahakamani.

  Kwa mujibu wa Waziri, madai yote yenye nyaraka zilizojitosheleza walimu wamelipwa na ambayo hayakuwa na nyaraka zilizojitosheleza, wamerudishiwa nyaraka zao.

  “Serikali imejitahidi kuwalipa walimu waliowasilisha nyaraka sahihi zilizojitosheleza za madai yao yote. Wenye madai yaliyokataliwa yameonekana nyaraka zake zinatofautiana na zilizomo kwenye mafaili yao. Kuna upungufu na kusigana kwa taarifa,” alisema Profesa Maghembe.
  Alisema walimu hawana sababu za kugoma ama kuendesha mgomo baridi kwa vile serikali imeonesha jitihada za kuwalipa madai yao.

  Hivi karibuni, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alisema madai ya walimu wa sekondari ya Sh bilioni 13.5, sawa na asilimia 52, hayatalipwa kwa kuwa yana upungufu ukiwemo wa kughushi nyaraka.

  Mkaguzi huyo, Ludovick Utouh aliwaambia waandishi wa habari kwamba walibaini upungufu huo baada ya uhakiki alioufanya katika madai ya watumishi hao walio chini ya Serikali.

  Majalada 19,861 yenye madai ya jumla ya Sh bilioni 26.07 yalipokewa. Kati yake, madai ya Sh bilioni 12.5 ambayo ni sawa na asilimia 48, ndiyo yamekubalika.

  Aidha, Waziri alizungumzia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na kusema serikali imejipanga vizuri kuisimamia. Alisema anatarajia wanafunzi wa vyuo vikuu wataendelea na masomo yao kama ilivyokusudiwa
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwanini anaanza na walimu? Wakati kuna wabunge, mawaziri ma wakuo wa mikoa na wilaya ambao wamegushi vteti na ushahidi upo? Kazi kwelikweli.
  zaidi ya hapo wanaoandaa orodha hizo ni maafisa rlimu na wengine sasa na hao watashitakiwa? Na walioandaa orodha feki za walimu hewa?
   
Loading...