Walimu Wakorofi, Wanoko na Wababe

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,787
3,050
Maisha ya shule yana misukosiko na changamoto sana aisee, tukio la leo limenifanya nikumbuke mbali sana.

Leo katika mishe mishe nimekutana na mmoja wa waalimu wa shule ya msingi niliosoma mkoa fulani.

Nilivyomuona yale mazingira sikuamini kama ni yeye ikabidi nimsalimie na kumkumbusha mimi ni fulani mwanafunzi wako shule fulani, akakumbuka tukasaimiana na ,story kidogo kisha tukaachana.

Ikabidi niulize kwa wenyeji huyu alikuwa mwalimu imekuwaje, wakasema hawaelewi. In short hali yake sio nzuri, ila wenyeji walichosema ni ana maisha ya kudonoa donoa.

Sijui alipatwa na nini maana maisha hayana ramani hujui kesho yako itakuwaje.

Huyu mwalimu bana alikuwa ana kila sifa ya kukufanya uchukie shule.
MBABE /MNOKO iwe zamu yake isiwe yake, ni wale omba usiingie kwenye mikono yake, ukipelekwa ofisini yupo aisee ilikuwa ni balaa.

Alikuwa ni wale waalimu hana mjadala, asikilizi hata ujitete vipi. Uwe umekosea au hujakosea. Binafsi niliangukia mikono yake mara tatu hivi (hapa niseme tu sikuwa nakosa na kilichotokea nakikukumbuka).

Waalimu kama mpo humu jueni maisha hayana formula, hayana ramani, kuwawekea mazingira magumu wanafunzi pasipo sababu sio vizuri.

Tendeni haki, fundisheni kwa upendo, penye mapungufu rekebisheni kwa upendo pia.

Asante.
 
Nkiwa sekondari o level nlipata mwalimu jina la serikali anaitwa Kavishe, lakini jina lake analotamba nalo ni "Red Devil". Huyu alikua mwalim wangu wa darasa.
Siku kama 3 baada ya kuripoti form nyoko, nko na masela tunapiga stori, kumbe darasa iko next to ofisi ya ticha bigi a.k.a mwalim mkuu.
Hyo siku alikua na wageni af mayowe kama yote, akaja chap akamwambia "monta" mmoja kiherehere atoe list ya waungwana wanaopiga mayowe.
Kama kawaida mimi na masela wangu wa back bencher tukatoka mbele kibingwa tukijua hakuna maajabu.
Ile tumetoka nje timepiga magoti kwa mbaaali akaja redi devo.
Mkuu akamwambia, unaona wanao? Wananipigia makelele embu deal nao.
Jamaa akatuchekiii, af akasema subr nakuja. Akaenda ofisini akarudi na mzigo wa kuni.
Akaanza kutembeza kichapo.
Yule fala anachapa sijawahi ona.
Nakumbuka aliniwasha stiki nkaomba poo kwanza. Nkamwambia, aiseee ticha subr kwanza nipumzike hali si hali.
Akadeal na wengine af akaniita, we msanii, unadhani nmekusahau? Kuja hapa senzi sana.
Nkaenda nkamalizia dozi yangu tukarudi klanga lakn maumiv yake sijawahi kusahau.
Sema nin, all in all na kasoro zake alikua na upendo mkuu. Tukienda shamba, tukishamaliza ekari zetu, hakuna kusaidia darasa lolote. Hata aje mkuu kuomba tikawasaide wengine, redi devo yeye anaweka msimamo, "watoto wangu wamemaliza shamba lao lote. Hakuna kusaidia wengine".
Kwaio sisi mapeeeema tinarudi skuli kuiba maji na chakula.
Mungu ampe maisha marefu japo ile Geography yake sikuwahi kuelewa hata chembe nlipita tu kwa kudra za bwana Jesus.
 
Ukaomba upumzike 😂😂😂.

Wako huyu inaonekana ailikuwa na ustaarabu mpka uingie anga zake.
 
Back
Top Bottom